Shambulio la bomu arusha ni kushindwa kwa ulinzi wa taifa.

Fue Fue

Senior Member
Jan 6, 2013
107
128
Nawapa pole wananchi, wakazi wa Arusha, wanachama na mashabiki wote wa Chadema, Viongozi wote wa Chadema na wote wenye mapenzi mema na Tanzania.

Natoa pole za dhati kwa wafiwa wa mlipuko huu na majeruhi Mungu awape uponyaji wa haraka.Nawapa pole watoto, akina mama na wazee kwani wameathrika zaidi.

Tukio la bomu la Arusha ni kielelezo cha kushindwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kusimamia usalama wa wananchi na mali zao. Mkutano huu ukiwa unalindwa na jeshi la polisi, usalama wa taifa imekuwaje tukio kama hili lijirudia ndani ya siku arobaini? Zaidi ya yote tukio hili likiambatana na kupigwa risasi zikielekezwa kwa raia.

Matukio haya hayaipi afya amani, mshikamano wala demokrasia chanya bali inadhoofisha taifa. Utawala wowote unaotaka kuendelea kukaa madarakani kwa vitisho, mauaji na kuumiza wananchi wake kamwe hauwezi kufanikiwa.

Kauli za Nape Nnauye na ile ya serikali inakatisha tamaa sana. Kusingizia wahanga na waathirika, badala ya kuita uchunguzi wa kina inatia shaka kubwa na kuaminisha kuwa serikali ya CCM inawea kuwa nyuma ya shambulio hili.

Matukio haya sasa yanaanza kuota mizizi, na si wakati wa kutoa kauli nyepesi, za kihuni na zilizokosa staha. Kama Nape na serikali wanajua nani kalipua kwanini serikali yao haiwakamati? Je matukio ya kigaidi yana siasa?

Taifa haliwezi kujengwa katika hali tete ya amani na kuanza kuwafundisha wananchi matumizi mabaya ya nguvu na uuwaji. Jeshi la polisi haliwezi kukwepa lawama hizi za kufa kwa raia wasio na hatia. Usalama wa taifa lazima wakubali kuna ufa mkubwa sana wa utendaji kazi.

Tukiacha haya matukio yaendelee itafikia hatua hakuna kiongozi yeyote atakayeweza kusimama mbele ya umati wa Watanzania kwa hofu ya kushambuliwa. Sio matukio ya kuyashangilia wala kukebehi uhai wa raia na binadamu.

Lazima wananchi tuamua ama kuwa na wauaji ama na watanzania. Serikali imeshindwa chama tawala kinaendesha siasa chafu za vitisho na kutesa wananchi. Matukio ya kuuwa wananchi hadharani kwa mkono wa serikali yapo bayana hasa lile la mwandishi wa habari wa iringa aliyeuwawa na polisi kwa kupigwa bomu la machozi hadharani akiwa ameshikwa na polisi. Hii inatisha na kusikitisha.

Je kwanini serikali mpaka leo haijaleta majibu ya wapi haya mabomu yanapatikani? Arusha tayari matumizi ya mabumu kwa raia yametumika mara tatu kwa kumbukumbu zangu, mara ya kwanza alishambuliwa shekh nyumbani kawke, Kanisani olasit na sasa mkutano wa Chadema. Je haya mabomu chanzo chake wapi?

Siasa za CCM zinasikitisha sana, hasa matukio ya kuuwa raia, Uchaguzi wa arumeru ulisababisha wanaCCM kumwua kwa mapanga kamanda wa Chadema bwana mbwambo wa usa river, Igunga alikufa mtu mapaka leo hakuna majibu. Morogoro walikufa wananchi bila majibu mpaka leo. Arusha polisi waliuwa raia kwa risasi kwa kisingizio cha maandamano. Na wiki hii wamekufa raia wasio na hatia mbele ya polisi kwa shambulio la bomu na risasi, walengwa wakiwa Mwenyekiti wa taifa wa chadema, Mbunge wa Arusha na wagombea udiwani kwa tiketi ya chadema kata nne za Arusha mjini. Huu ni unyama na ukosefu mkubwa wa utu, ubinadamu na haki za binadamu.

Wananchi ni wajibu wetu kukataa hali hii kwa gharama kubwa. Matukio haya yanadhoofisha uchumi, uwekezaji na hayaleti afya kwa taifa hasa sura ya amani ndani na nje ya nchi. Ni vigumu sana wananchi kujiletea maendeleo kama demokrasia inageuzwa vita , uhasama, chuki na uaduai. Hakuna Taifa lolote duniani liloweza kujipasua likakua.

Siasa ajira ndio sababu ya vita kwenye mataifa mengi. Ukosefu wa uzalendo, mapenzi ya dhati ya familia, wananchi, majirani na ustawi wa nchi ndio chanzo cha ukatili na ukosefu wa utu hasa uhai wa mwanadamu.

Lazima kuunda tume huru ya ndani na nje inayohusisha wataalamu mbalimbali wa milipuko, ugaidi, kutoka kada zote. Tume hii lazima iwe na nguvu ya kimahama ya ndani na ya kimaifa ICC ili kuweza kuwashitaki wote waliopo nyuma ya matukio haya ya kigaidi bila kujali nyadhifa zao na bila kumuonea mtu.

Usafi wa serikali ni pale itakapokubali uchunguzi huru wa swala hili.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Naxhani tumeshindwa kulinda taifa letu kiasi kwamba hata Obama anakuja n walinzi wake. Kama ndege ya jeshi ya nchi nyingine inaweza kutua nchini na kuchukua twiga walio hai bila kuonekana bado utasema kuna ulinzi? Hakuna ulinzi wo wote ingawa kuna waziri wa ulinzi na mwingine wa mambo ya ndani.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Kuna tatizo kubwa kimfumo, naamini tuna watu wazuri tu, ila uongozi au kwa hila au kwa uwezo mdogo wameharibu mfumo wa usalama, na matokeo ndio hayo. Nahisi mabaya zaidi yatatokea, hasa ukizingatia ndani ya CCM yenyewe Hamkani si swari tena. Wajirekebishe spidi kwa mslahi ya umma wote.
 
Nawapa pole wananchi, wakazi wa Arusha, wanachama na mashabiki wote wa Chadema, Viongozi wote wa Chadema na wote wenye mapenzi mema na Tanzania.

Natoa pole za dhati kwa wafiwa wa mlipuko huu na majeruhi Mungu awape uponyaji wa haraka.Nawapa pole watoto, akina mama na wazee kwani wameathrika zaidi.

Tukio la bomu la Arusha ni kielelezo cha kushindwa kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kusimamia usalama wa wananchi na mali zao. Mkutano huu ukiwa unalindwa na jeshi la polisi, usalama wa taifa imekuwaje tukio kama hili lijirudia ndani ya siku arobaini? Zaidi ya yote tukio hili likiambatana na kupigwa risasi zikielekezwa kwa raia.

Matukio haya hayaipi afya amani, mshikamano wala demokrasia chanya bali inadhoofisha taifa. Utawala wowote unaotaka kuendelea kukaa madarakani kwa vitisho, mauaji na kuumiza wananchi wake kamwe hauwezi kufanikiwa.

Kauli za Nape Nnauye na ile ya serikali inakatisha tamaa sana. Kusingizia wahanga na waathirika, badala ya kuita uchunguzi wa kina inatia shaka kubwa na kuaminisha kuwa serikali ya CCM inawea kuwa nyuma ya shambulio hili.

Matukio haya sasa yanaanza kuota mizizi, na si wakati wa kutoa kauli nyepesi, za kihuni na zilizokosa staha. Kama Nape na serikali wanajua nani kalipua kwanini serikali yao haiwakamati? Je matukio ya kigaidi yana siasa?

Taifa haliwezi kujengwa katika hali tete ya amani na kuanza kuwafundisha wananchi matumizi mabaya ya nguvu na uuwaji. Jeshi la polisi haliwezi kukwepa lawama hizi za kufa kwa raia wasio na hatia. Usalama wa taifa lazima wakubali kuna ufa mkubwa sana wa utendaji kazi.

Tukiacha haya matukio yaendelee itafikia hatua hakuna kiongozi yeyote atakayeweza kusimama mbele ya umati wa Watanzania kwa hofu ya kushambuliwa. Sio matukio ya kuyashangilia wala kukebehi uhai wa raia na binadamu.

Lazima wananchi tuamua ama kuwa na wauaji ama na watanzania. Serikali imeshindwa chama tawala kinaendesha siasa chafu za vitisho na kutesa wananchi. Matukio ya kuuwa wananchi hadharani kwa mkono wa serikali yapo bayana hasa lile la mwandishi wa habari wa iringa aliyeuwawa na polisi kwa kupigwa bomu la machozi hadharani akiwa ameshikwa na polisi. Hii inatisha na kusikitisha.

Je kwanini serikali mpaka leo haijaleta majibu ya wapi haya mabomu yanapatikani? Arusha tayari matumizi ya mabumu kwa raia yametumika mara tatu kwa kumbukumbu zangu, mara ya kwanza alishambuliwa shekh nyumbani kawke, Kanisani olasit na sasa mkutano wa Chadema. Je haya mabomu chanzo chake wapi?

Siasa za CCM zinasikitisha sana, hasa matukio ya kuuwa raia, Uchaguzi wa arumeru ulisababisha wanaCCM kumwua kwa mapanga kamanda wa Chadema bwana mbwambo wa usa river, Igunga alikufa mtu mapaka leo hakuna majibu. Morogoro walikufa wananchi bila majibu mpaka leo. Arusha polisi waliuwa raia kwa risasi kwa kisingizio cha maandamano. Na wiki hii wamekufa raia wasio na hatia mbele ya polisi kwa shambulio la bomu na risasi, walengwa wakiwa Mwenyekiti wa taifa wa chadema, Mbunge wa Arusha na wagombea udiwani kwa tiketi ya chadema kata nne za Arusha mjini. Huu ni unyama na ukosefu mkubwa wa utu, ubinadamu na haki za binadamu.

Wananchi ni wajibu wetu kukataa hali hii kwa gharama kubwa. Matukio haya yanadhoofisha uchumi, uwekezaji na hayaleti afya kwa taifa hasa sura ya amani ndani na nje ya nchi. Ni vigumu sana wananchi kujiletea maendeleo kama demokrasia inageuzwa vita , uhasama, chuki na uaduai. Hakuna Taifa lolote duniani liloweza kujipasua likakua.

Siasa ajira ndio sababu ya vita kwenye mataifa mengi. Ukosefu wa uzalendo, mapenzi ya dhati ya familia, wananchi, majirani na ustawi wa nchi ndio chanzo cha ukatili na ukosefu wa utu hasa uhai wa mwanadamu.

Lazima kuunda tume huru ya ndani na nje inayohusisha wataalamu mbalimbali wa milipuko, ugaidi, kutoka kada zote. Tume hii lazima iwe na nguvu ya kimahama ya ndani na ya nje ya nchi ili kuweza kuwashatiki wote waliopo nyuma ya matukio yote haya ya kigaidi bila kujali nyadhifa zao na bila kumuonea mtu.

Usafi wa serikali ni pale itakapokubali uchunguzi huru wa swala hili.

Mungu ibariki Tanzania.
Mkuu, kwa mtazamo wako unadhani kuwa ccm na serikali ndo chanzo cha yote haya. Lakini ukumbuke kuwa ni serikali hii hii ya ccm ndiyo imeweza kudumisha amani na utulivu wa taifa hili kwa muda mrefu. Ukumbuke kuwa matukio haya ya mabomu ni mageni hapa nchini na kila mtanzania ana haki ya kujiuliza chanzo cha yote haya bila ya kuingiza ushabiki wa kisiasa.swali ambalo nilidhani utajiuliza ni kwa nini matukio haya yameongezeka sasa mara tu baada ya chadema kutangaza kuwa nchi haitatawalika mpaka kieleweke. Ni vema pia ukatafakari kauli za baadhi ya viongozi wa chadema juu ya amani ya nchi hii. Kuwa amani ya tanzania ipo mikononi mwa chadema. Kinyume chake ni kuwa kuvunjika kwa amani ya nchi hii chanzo chake ni chadema. Pia unapaswa kijiuliza kwa nini matukio hayo ya mabomu uliyoorodheshwa yanatokea Arusha tu wakati ccm ipo kila kona ya nchi hii. Chukulia mfano kule pemba ambako CUF wameshika hatamu. Mbona hatujasikia matukio ya kufedhehesha kama yale ya Arusha? Kwa mtu mwenye kutumia chembe ya akili yake kufikiri, atakubaliana nami kuwa siasa za Arusha zinatakiwa kuhojiwa na kila mmoja hususan uwezo wa mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema. Ni wakati wa ubunge wake ndo tunashuhudia matukio mengi ya kufedhehesha kiasi cha kuharibu taswira ya mji wa Arusha. Kwa upande wangu nadhani serikali ingeanzia kumchunguza huyu mtu kwani uwezekano wa yeye kuwa nyuma ya matukio haya ni mkubwa
 
Asante kwa mchango wako. Serikali iliyoko madarakani popote pale duniani inawajibika kwa ulinzi wa wananchi wake na mali zao na mipaka yake.

Amani ya Tanzania kwa miaka mingi ni tunu na tabia ya watanzania. Uongozi wa chama kimoja haukuwa na ushindani wala udadisi, ulikuwa wa kimabavu, usio na demokraisia. elimu ya raia ilikuwa haitolewi na habari zote zilikuwa za kufurahisha watawala.

Ushindani wa demokrasia na vyama vingi huitisha serikali dhaifu kwa kuogopa kutoka madarakani. Nchi nyingi za kiafrika zinaathirika na uchu wa madaraka ya viongozi wengi hasa waliopo madarakani na hivyo kuzuia kila aina ya upinzani pale unapoonyesha kukubalika kwa wananchi kwa hila zozote zile, mfano serikali ya Mugabe, Yoweri Museni, Hosni Mubaraka, Gaddafi wa Libya, Tunisia, Congo Kinshasha nk . Ukimfanya mwananchi wako mtumwa ndani ya yake unakaribisha matatizo.

Miaka ya hivi karibuni matukio ya kigaidi yameongezeka sana, na linalosikitisha ni serikali kuyafumbia macho au kuyasahau na kushindwa kuwaaminisha wananchi kwamba serikali yao ipo kwa ajili ya uhai, utu ulinzi wa wananchi wake na mali zake.

Zanzibar, wameuwawa wananchi kwa kupigwa risasi kwa matukio ya kigaidi, Padre kupigwa risasi ,Shekh kumwagiwa tindikali, shekh kuchumwa kisu, Padre, Buseresele amechinwa mtu, Arusha mabomu, Iringa Mwandishi kapigwa bomu na polisi hadharani, Morogoro polisi wamepiga mwananchi risasi. Mtwara wananchi napolisi wamekufa mpaka jeshi likaingilia kati, nk nk haya matukio yote ni ukosefu wa ulinzi, usalama wa taifa kupata au kutoa habari za kiusalama na kufanyiwa kazi kabla ya matukio, udhaifu wa serikali.

Watawala wamekuwa wa kutoa matamko , keeli, matusi na kauli nyepesi. Ukuaji wa uchumi, ungezeko la watu, elimu, na ukosefu wa ajira vinakuja na gharama zake moja wapo ni kuongezeka kwa uhalifu wa hali ya juu. Upatikanaji wa malia asili kama gesi, mafuta, madini wanyama adimu huongeza shauku ya wawekezaji wema na wabaya ambao wote lazima vyombo vyetu vya ulinzi viwe hatua kadhaa mbele kunusa hatari.

Matukio mengi yanayotokea kwenye mikutano ya siasa hasa wakati wa chaguzi ni kazi ya chama tawala kwa kuogopa kushindwa hivyo kutumia vitisho dhidi ya wananchi. Hili haliwezi kubalika. Ukitetea eti kwasababu wewe unakipenda chama chako bila kuangalia ukweli utakuwa hulitendei taifa lako haki.

Tunataka serikali ikamate, na kuwafikisha wote mbele ya sheria wanahusika na matukio yote ya kigaidi, mauji, uvunjivu wa amani bila kujali uwezo, vyeo, dini, taifa nk .

Sitakubali wale wanaotakiwa kutulinda kuanza kushutumu nataka wachukue hatua, na watupe majibu yenye akili waache kucheza maagizo wakati wananchi wasio na hatia wanapata vilema na kupoteza maisha.
 
Back
Top Bottom