Shamba la wafu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,794
Hivi una habari ya kuwa ardhi ndio kila kitu duniani unapokuja kwenye vitu yabisi? Na maji ndio kila kitu duniani linapokuja suala la vimiminika. Basi heshimu sana hivi viwili.

Kuna somo muhimu sana lenye maarifa tele alilotoa lifecoded kule intelligence.. Kwamba maisha yetu yamejawa na mifumo, mipangilio, hesabu na nywila.

Ardhi na maji ndio vimebeba mifumo yote ya uhalisia wetu.

Tunatambua shamba ni nini na linatarajiwa liwe na vitu gani. Ni mazao ya kuliwa ama mazao kwa matumizi ya binadamu na ubunifu wake. Hakuna mashamba ya hewani. Hata zile bustani zinazoning'inia za Babiloni zina udongo juu yake.

Shamba linalolimwa mazao yasiyozaa hilo ni sawa na shamba la wafu, yaani makaburini walipolala waliokuwa hai kabla. Shamba la wafu halizai. Shamba la wafu halivunwi. Shamba la wafu hata likitoa matunda basi ni matunda mwitu.

Maisha yako hapo yalipo na hivyo yalivyo ni kwa sababu ya mifumo na nywila. Mifumo ya kujiundia na mifumo asilia
Katika kupita huku na kule kutafuta mafanikio, unafuu wa maisha, kutatua changamoto zako. Unatengenezewa mifumo bila kujua. Mifumo yako ikiwa chanya na kuendana na mifumo asilia mambo yako hukunyookea na kuwa kama Mondi japo haiwezi kuwa timilifu.

Tunapotafuta hii nafuu ya changamoto zetu hata kama ni kiroho bado ardhi inahusika na kutumika pakubwa tu. Hapa ukikosea tu hesabu zake unajikuta unazalisha shamba la wafu kwa mikono yako mwenyewe.

Shamba la wafu unalozalisha litakuzalia MAPOOZA.. Na matunda yake yatakuwa matunda pori yasiyolika na mimea yake itakuwa magugu yasiyofaa hata chakula cha mifugo
Utapata kazi lakini hutafanya lolote la manufaa na utakuwa mtu wa madeni mengi
Utafanya biashara lakini itadumaa.. Haikui wala faida yake huoni
Utaingia kwenye mahusiano lakini changamoto hazikuishii..
Mtatamani kupata watoto lakini mimba zitaishia kuharibika ama ukizaa watoto wanakufa
Utapata pesa lakini zitakakoishia hujui..

Ukiona haya tafakari ramani uliyopita kufika hapo na wapi ulikosea.. Ni lini na wapi ulienda kupata ushauri wa kusafishwa nyota na wataalamu wa nguvu za giza
Ni wapi ulienda kuzindikwa
Ni wapi ulienda kupatiwa tiba za kilozi
Ni wapi ulienda kutafuta kinga ama ulienda kumumuuza mtu

Ardhi tuliyomo ni madhabahu.. Madhabahu inaweza kuwa chanya au hasi.. Kiasili ardhi sio chafu tunaichafua wenyewe kwa mazindiko na ibada za kilozi huku tukiangamiza roho zisizo na hatia
Unahitaji kuitakasa ardhi
Unahitaji kujitakasa binafsi
Unahitaji kutakasa umiliki wako
Unahitaji kutakasa kila ulichonacho

Ili mahusiano yako yawe ya furaha
Ili kazi yako iwe na mafanikio
Ili biashara yako ikue
Ili pesa yako ionekane na kufanya maendeleo
Na hapo ndio kutakuwa hakuna kuzaa MAPOOZA tena na maisha yako utayaona katika mwanga tofauti ... Kwakuwa sasa shamba lako si shamba la wafu tena...
Kanunue chumvi yako ya mabonge leo.. Itumie kama tulivyokwisha elekezana... Matokeo utayaona
 
Kuna somo la Christopher Mwakasege linasema iombee ardhi uliyo inunua kabla hujajenga nyumba ya kuishi hapo,maana ktk ardhi hiyo kuna miungu ya kale ya wamiliki wa eneo, kizazi na kizazi mahala hapo, ngoja na hapa nisikilize.
 
Mshana Jr nimenunua kilo nzima ya chumvi ya mawe iko hapa bafuni, sasa sielewi cha kusema mtani, lugha ngumu.

Hata hivyo mwanga fulani umeanza kuonekana.
Kazi za chumvi hizi hapa
Inakinga.. Nuia ikukinge
Inatakasa nuia ikutakase
Inasafisha nuia ikusafishe
Ina ladha nuia ilete ladha kwenye maisha yako
Inavuta nuia ilete mvuto kwenye maisha yako
Inategemewa na wengi.. Nuia uwe tegemeo kwa wengine na sio tegemezi
 
Mkuu unajua ukweli wa nguvu za Jina la Yesu na jinsi damu ya Yesu inavyotakasa uovu wote. Watu watumie makuu haya kufukuza nguvu za giza na sio kingine.
 
Mkuu unajua ukweli wa nguvu za Jina la Yesu na jinsi damu ya Yesu inavyotakasa uovu wote. Watu watumie makuu haya kufukuza nguvu za giza na sio kingine.
Elisha akaenda kwenye chemchemi ya maji, akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa; tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba.”
 
Nini madhara ya dawa za kusafisha nyota???

Nini madhara ya dawa kuongeza bahati ?

Nini madhara ya kukinga vitu vyako visiibiwe?

Nini madhara ya kukinga nyumba yako isilogwe na wanga?

Ikiwa vitu vyote hivyo unafanya sio kwa nia ya kumuumiZa mtu yaani nyota iwe safi tu,wezi wasiibe tu bila kumdhuru,wanga wasiwangee tu bila kumdhuru mwanga..

Nina vitu flan vya thamani sana vipo sehemu hatarishi na inabidi vikae pale maana hakuna namna ya kuvitoa na kuvirudisha SITAKI viibiwe na sitaki kumdhuru mtoto wa ntu....
 
Back
Top Bottom