Shakira Aingizwa Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shakira Aingizwa Mjini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wanamuziki maarufu duniani wa muziki wa Pop, Shakira ambaye anajulikana sana kwa kunyonga kiuno chake, ameibiwa pete yake ya thamani wakati alipokuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake waliohudhuria shoo yake nchini Mexico.
  Shakira mwenye umri wa miaka 34, alikuwa akipafomu kwenye shoo yake katika chuo kikuu cha University of Monterrey kilichoko kwenye mji wa Monterrey, Mexico siku ya alhamisi wakati kibaka mmoja alipofanikiwa kuivua pete ya nyota huyo wa muziki wa Pop.

  Shakira ambaye alikuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake, aligundua muda mfupi baadae kuwa pete yake ameishavuliwa.

  Tukio hilo la wizi lilinaswa live na mpiga picha za video katika shoo hiyo hata hivyo Shakira hakukatisha shoo yake na wala hakumkamata mwizi wake.

  Hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa kutokana na tukio hilo.

  Wakati huo huo, mpenzi wa Shakira, nyota wa soka beki wa timu ya Barcelona ya Hispania, Gerard Pique amesema kuwa ingawa anafurahia kuwa kwenye mahusiano na Shakira lakini bado hajazoea maisha ya kufuatiliwa kila kona na paparazzi ambao wamekuwa wakimfuatilia nyota huyo wa soka tangu ilipojulikana kuwa anatoka na Shakira.

  "Huwa wanakuja kundi kubwa, inabidi kuzoea hali hii ya kufuatwa mitaani kila kona", alisema Pique.
  5602770.jpg
   
Loading...