Elias Misinzo Maligo
Senior Member
- Apr 7, 2019
- 129
- 104
Robot la Matope, Shaka Zulu nijuavyo mama yake alitengwa hapo kijijini na kwenda ufalme wa jirani siyo kwa sababu Mfalme Senzangakhona alimuoa Nandi ( mama yake Shaka) kuwa kabila tofauti na Wazulu, bali kwa sababu Mfame alimpa ujauzito Nandi kwenye sherehe za mavuno zilizokuwa zinafanyika usiku.
Na kwa mila za Wazulu za wakati huo, mwanamke akibeba mimba kabla ya kuolewa anauawa, kabla ya kuuawa kwanza amtaje aliyempa hiyo mimba naye auawe! Sasa aliyevunja sheria hiyo ni mfalme Senzangankhona mwenywe!
Ili kuepusha aibu hiyo, mfalme aliongea na mfalme mwenzake wa jirani Nandi akatoroka kijijini akamzalia huko Shaka. Lingine, Shaka mwisho wake haukuwa mzuri kutokana na mama yake kumfundisha ushirikina toka akiwa mdogo, ambapo alichanjwa madawa ya ushujaa vitani, madawa ambayo muda wote yalihitaji kuua, yalihitaji damu. Kutokana na hilo, Shaka aliongoza mapambano mengi ya kivita, na furaha yake ilitimia pale anapoua. Falme jirani zote zilikimbia zisikiapo jeshi la Shaka Zulu, Shaka akakosa maadui wa kupigana nao.
Kwa kuwa dawa zake zilikuwa na masharti ya kuua kila wakati, Shaka akaanza kuumwa, kuumwa kwa kukosa wa kuua! Ikafikia sasa Shaka akaanza kuua watu wake, na anapoua kwa mkono wake watu wanne au watano, afya ya mwili wake inarejea bukheri wa afya! Moja ya mbinu aliyoitumia kuua kwa urahisi anapohisi kuumwa kwa kuteswa na madawa ni kuitisha sherehe ya vyakula na pombe ambapo wanakijiji hulewa na kuimba nyimbo, ndipo Shaka huinuka na kuagiza aletewe watu wanaoimba vibaya na hutumia mwanya huo kuwaua, na anapoua afya yake inarejea!
Mwisho Shaka aliuawa na ndugu zake wawili wa mama wengine lakini baba mmoja waliomtembelea na akawaamini kuongea nao kwenye ikulu yake huku walinzi wakiamini mfalme yuko na ndugu zake!