SHAKA: Zitto Acha Ulalamishi na Siasa za Kitoto

Chama Cha Mapinduzi kimesema Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameanza kutapatapa na kutafuta mchawi baada ya kuona Jahazi la Chama chake likienda mrama kufuatia matokeo ya awali katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe, ambapo CCM imeongoza kwenye Vituo vilivyokwishatangaza matokeo kwa zaidi ya asilimi 90.

Mwenezi Shaka amesema uzushi wa Zitto ni kuelekea kufilisika kisiasa na kwamba hautakinusuru chama chake, kwani Wananchi wamemkataa Mgombea wa Chama hicho na pia hakikuwa na mtandao wa kisiasa unaoweza kukipa kura za ushindi.

Shaka ameongeza kuwa propaganda za kale anazofanya Zitto haziwezi kubadili matokeo ya wapiga kura ya jimbo la Muhambwe na Buhingwe.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema hayo jioni hii kufuatia madai ya uzushi yaliyosambazwa na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Act Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe katika mitandao ya kijamii.

Shaka alieleza kuwa ikiwa Zitto alishindwa kupata ushindi jimbo la Kigoma mjini mwaka 2015 anaweza vipi kuwashawishi wananchi wa Buhigwe na Muhambwe kukiamini Chama chake.

Aidha, Shaka amemtaka Zitto kukomaa kisiasa na kuonyesha kupevuka, kwani kudai kuna kura feki na kwamba amevamiwa na mapanga ni propaganda nyepesi na haziwezi kukisaidia chama chake ikiwa kimeshindwa kujiandaa mapema kunadi sera, kupata Mgombea anayekubalika na kuwa na mikakati ya kampeni na ushindi.

“Chama chake kimeshindwa kuingiza timu uwanjani iliyojiandaa vizuri... sisi tumejiandaa muda mrefu na wagombea wetu wanakubalika bila shaka yoyote” alisema Shaka.

Aidha amesema wanajiandaa mara baada kutangazwa rasmi matokeo hayo na Tume ya Uchaguzi kuwasindikiza Wabunge wao kutoka Buhigwe na Muhambwe kwenda kuapa Bungeni kama itakavyoelekezwa na mamlaka zinazohusika.

MWISHO.View attachment 1787713
Atwambie kama amesha hama mombasa
 
Tuchukulie Zito anapiga propaganda, sasa tuwekeeni idadi ya wapiga kura ili tuone mnavyokubalika na wananchi wa huko. Idadi ya wapiga ndio italeta uhalali wa kukubalika baina ya ndugu waliokuwa wanashindana.
Ccm hawawezi kuweka idadi kamili ya wapiga kura ya halali.
Lazima wachakachue
 
Pigeni kura ni vijiji vingapi havina maji miaka 60 sasa.

Nini umuhimu wakulumbana wakati hakuna huduma.Tumeshinda miaka yote nisifa zakijinga
 
Kuna wakati namdharau Zito. Maana hana msimamo unaoeleweka. Alisema hawatashiriki uchaguzi mpaka kuwepo na tume huru ya uchaguzi. Mara, tutashiriki uchaguzi wa Muhambwe.

Asilalamike, apokee chochote kinachomjia maana ameridhika na kila kitu.
 
Jamaa yupo huko twitter anajikosha. Anatengeneza mazingira ya Mama Samia kumuita kwenye mkutano na wapinzani. Nawaonea huruma sana ACT, huyu jamaa anapigania tumbo lake tu!
IMG_9315.JPG
 
Tuchukulie Zito anapiga propaganda, sasa tuwekeeni idadi ya wapiga kura ili tuone mnavyokubalika na wananchi wa huko. Idadi ya wapiga ndio italeta uhalali wa kukubalika baina ya ndugu waliokuwa wanashindana.
Bwashee subiri matokeo yatatangazwa na wasimamizi wa uchaguzi
 
Ukitaka idadi ya wapiga kulaa. Kawaulize tume ya uchaguzi au nenda kwenye vituo vyakupigia kura utasikia matangazo yote hadi kula zilizo haribikaaa utaaambiwaaa.
Kama tume wameshindwa kuweka matokeo ya ule uchaguzi mkuu ndio wataweka sasa? Ama bado tume inatumia mifumo ya kizee ya kuweka kwenye daftari la quire 3?
 
Ccm hawawezi kuweka idadi kamili ya wapiga kura ya halali.
Lazima wachakachue

Wamekaa na Zito wakubaliane idadi ya kuweka. Halafu wakitoka hapo watamsifia Zito kuwa ana siasa za kistaarabu.
 
Kama tume wameshindwa kuweka matokeo ya ule uchaguzi mkuu ndio wataweka sasa? Ama bado tume inatumia mifumo ya kizee ya kuweka kwenye daftari la quire 3?
Simulisema matokeo halali mnayo na mkatutapeli wanainchi eti mnaenda kushitaki tume kwenye mahakama za kimataifaaa. Au ilikua KIIKI zenu kama kawaida yenuuu
 
Wamekaa na Zito wakubaliane idadi ya kuweka. Halafu wakitoka hapo watamsifia Zito kuwa ana siasa za kistaarabu.
Exactly huo ndiyo mpango wao na Zitto siyo mjinga maana anavuta mpunga mrefu
 
Na yule tapeli wenu aliyegaragazwa na kutimkia ugaibuni kukwepa aibuu ya kugaragazwaaa

Ingia tovuti ya tume ya taifa kama matokeo yamewekwa, na kama yamewekwa niambie, kisha nitakupa Majibu yaliyotolewa wakati ule na hiyo list mpya kama iko huko.
 
Back
Top Bottom