SHAKA: Zitto Acha Ulalamishi na Siasa za Kitoto

budget

Member
Feb 23, 2015
41
125
Chama Cha Mapinduzi kimesema Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameanza kutapatapa na kutafuta mchawi baada ya kuona Jahazi la Chama chake likienda mrama kufuatia matokeo ya awali katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe, ambapo CCM imeongoza kwenye Vituo vilivyokwishatangaza matokeo kwa zaidi ya asilimi 90.

Mwenezi Shaka amesema uzushi wa Zitto ni kuelekea kufilisika kisiasa na kwamba hautakinusuru chama chake, kwani Wananchi wamemkataa Mgombea wa Chama hicho na pia hakikuwa na mtandao wa kisiasa unaoweza kukipa kura za ushindi.

Shaka ameongeza kuwa propaganda za kale anazofanya Zitto haziwezi kubadili matokeo ya wapiga kura ya jimbo la Muhambwe na Buhingwe.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema hayo jioni hii kufuatia madai ya uzushi yaliyosambazwa na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Act Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe katika mitandao ya kijamii.

Shaka alieleza kuwa ikiwa Zitto alishindwa kupata ushindi jimbo la Kigoma mjini mwaka 2015 anaweza vipi kuwashawishi wananchi wa Buhigwe na Muhambwe kukiamini Chama chake.

Aidha, Shaka amemtaka Zitto kukomaa kisiasa na kuonyesha kupevuka, kwani kudai kuna kura feki na kwamba amevamiwa na mapanga ni propaganda nyepesi na haziwezi kukisaidia chama chake ikiwa kimeshindwa kujiandaa mapema kunadi sera, kupata Mgombea anayekubalika na kuwa na mikakati ya kampeni na ushindi.

“Chama chake kimeshindwa kuingiza timu uwanjani iliyojiandaa vizuri... sisi tumejiandaa muda mrefu na wagombea wetu wanakubalika bila shaka yoyote” alisema Shaka.

Aidha amesema wanajiandaa mara baada kutangazwa rasmi matokeo hayo na Tume ya Uchaguzi kuwasindikiza Wabunge wao kutoka Buhigwe na Muhambwe kwenda kuapa Bungeni kama itakavyoelekezwa na mamlaka zinazohusika.

MWISHO.​

IMG-20210516-WA0068.jpg
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,625
2,000
Tuchukulie Zito anapiga propaganda, sasa tuwekeeni idadi ya wapiga kura ili tuone mnavyokubalika na wananchi wa huko. Idadi ya wapiga ndio italeta uhalali wa kukubalika baina ya ndugu waliokuwa wanashindana.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,085
2,000
Shaka alieleza kuwa ikiwa Zitto alishindwa kupata ushindi jimbo la Kigoma mjini mwaka 2015 anaweza vipi kuwashawishi wananchi wa Buhigwe na Muhambwe kukiamini Chama chake.
Je 2020?, 2019? We kijana nawe acha propaganda za kitoto kama umri wako
 
SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
365
1,000
Na Mwandishi wetu, Kigoma.

Chama Cha Mapinduzi kimesema Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameanza kutapatapa na kutafuta mchawi baada ya kuona Jahazi la Chama chake likienda mrama kufuatia matokeo ya awali katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe, ambapo CCM imeongoza kwenye Vituo vilivyokwishatangaza matokeo kwa zaidi ya asilimi 90.

Mwenezi Shaka amesema uzushi wa Zitto ni kuelekea kufilisika kisiasa na kwamba hautakinusuru chama chake, kwani Wananchi wamemkataa Mgombea wa Chama hicho na pia hakikuwa na mtandao wa kisiasa unaoweza kukipa kura za ushindi.

Shaka ameongeza kuwa propaganda za kale anazofanya Zitto haziwezi kubadili matokeo ya wapiga kura ya jimbo la Muhambwe na Buhingwe.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema hayo jioni hii kufuatia madai ya uzushi yaliyosambazwa na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Act Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe katika mitandao ya kijamii.

Shaka alieleza kuwa ikiwa Zitto alishindwa kupata ushindi jimbo la Kigoma mjini mwaka 2015 anaweza vipi kuwashawishi wananchi wa Buhigwe na Muhambwe kukiamini Chama chake.

Aidha, Shaka amemtaka Zitto kukomaa kisiasa na kuonyeshe Kupevuka, kwani kudai kuna kura feki na kwamba amevamiwa na mapanga ni propaganda nyepesi na haziwezi kukisaidia chama chake ikiwa kimeshindwa kujiandaa mapema kunadi sera, kupata Mgombea anayekubalika na kuwa na mikakati ya kampeni na ushindi.

“Chama chake kimeshindwa kuingiza timu uwanjani iliyojiandaa vizuri... sisi tumejiandaa muda mrefu na wagombea wetu wanakubalika bila shaka yoyote” alisema Shaka.

Aidha amesema wanajiandaa mara baada kutangazwa rasmi matokeo hayo na Tume ya Uchaguzi kuwasindikiza Wabunge wao kutoka Buhigwe na Muhambwe kwenda kuapa Bungeni kama itakavyoelekezwa na mamalaka zinazohusika.

MWISHO.
IMG-20210516-WA0071.jpg
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,085
2,000
Tuchukulie Zito anapiga propaganda, sasa tuwekeeni idadi ya wapiga kura ili tuone mnavyokubalika na wananchi wa huko. Idadi ya wapiga ndio italeta uhalali wa kukubalika baina ya ndugu waliokuwa wanashindana.
tindo sjakuelewa? ukipata iddi ya wapiga kura unapataje kuona kukubalika kwa candidate?
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
4,035
2,000
Zito wa ajabu, anakusanya na kupiga kampeni na watoto kisha anaji-mwambafai eti ndio watakao mpatia ushindi.😂😂
E1cf-X4XoAIdQco.jpeg
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,085
2,000
Kama wapiga kura ni laki 1, natarajia kuona wangalau wapiga kura 50,000 kujitokeza kupiga kura. Kama wapiga kura hawajafika hata 10,000 hapo utasemaje unakubalika?
Very correct, nimekuelewa. Kwani wameshatangaza mshindi?
 
Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,748
2,000
Tuchukulie Zito anapiga propaganda, sasa tuwekeeni idadi ya wapiga kura ili tuone mnavyokubalika na wananchi wa huko. Idadi ya wapiga ndio italeta uhalali wa kukubalika baina ya ndugu waliokuwa wanashindana.
Ukitaka idadi ya wapiga kulaa. Kawaulize tume ya uchaguzi au nenda kwenye vituo vyakupigia kura utasikia matangazo yote hadi kula zilizo haribikaaa utaaambiwaaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom