Shaka: Watanzania zindukeni kujua malengo na muelekeo wa Rais Samia

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SEHEMU YA NUKUU ZA KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI SHAKA HAMDU SHAKA WAKATI AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO

"Watanzania zindukeni kujua malengo na muelekeo wa Rais Samia katika kujituma kwa juhudi, bidii na maarifa, kazi iwe kuajiriwa au kujiajiri humpa mtu hadhi na heshima, uvivu adui wa maendeleo , utegemezi na ni utumwa" - Shaka Mwenezi Taifa

"Iwapo kila Mtanzania atawajibika na kufanya kazi kama yalivyo malengo, mipango na mikakati ya Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania itapaa na kuwa nchi yenye uchumi unaojitegemea" - Shaka Mwenezi Taifa

"Uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita kuendeleza kauli mbiu ya ‘kazi iendelee’ ni kumtaka kila mtu anayeishi mjini na kijijini atambue wajibu wa kujituma, kufanya kazi, kuzalisha mali na kuitumikia nchi yake" - Shaka Mwenezi Taifa

"Siku moja ikitoke Watanzania tukayaelewa malengo ya kisera na kimkakati ya serikali ya awamu ya sita, yanayotaka watu kujituma, ndipo tutakapoondokana na kadhia ya umasikini. Binadamu anapoamini kufanya kazi ni kama adhabu au utumwa huo ni mtazamo hasi usiofaa kufuatwa," - Shaka Mwenezi Taifa.

"Katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Samia ameakisi mambo yaliyokuwa yakitamaniwa na jamii yatokee, sauti ya Rais Samia imetoa mwangwi ili kuwazindua waliotaka kukata tamaa ambapo fikra, akili na mioyo ya Watanzania imepata ratiba mpya kwa kuzingatia mambo ya msingi yanayotamaniwa na kutoa uamuzi wa haki" - Shaka Mwenezi Taifa

"Tulipopata uhuru na kufuzu Mapinduzi ya Zanzibar, kaulimbiu za marais na waasisi wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume, ilimtaka kila mtu afanye kazi" - Shaka Mwenezi Taifa

"Nyerere na Karume wakaeleza kazi ni kipimo na thamani ya utu wa mtu. Tafsiri ya uhuru ni kufanya kazi. Watu walishiriki kwa pamoja kufanya za maendeleo, leo hii Rais Samia anaendeleza maono ya waasisi wetu hasa katika suala la uchumi wa kipato kwa Watanzani," - Shaka Mwenezi Taifa

" CCM inaridhishwa jinsi wananchi wanavyofanya shuhuli zao za uzalishaji na kuipongeza Serikali inayongozwa na Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii na miundombinu ya kiuchumi ili kuharakisha maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi kukiwa na amani na utulivu" - Shaka Mwenezi Taifa.

20211130_184435.jpg

20211130_184436 (1).jpg

20211130_184436.jpg

20211130_184435 (1).jpg
 
Aanze na wazanzibar wenzake ni wavivu kupita kiasi, pia wanaishi bure kwenye nyumba za Karume hawapipi kodi, bill maji wala umeme.
 
Kuna mfumuko mkubwa wa bei, yeye amekalia kupiga propaganda mfu.
 
Shaka anapaswa kuzinduka yeye kujua nchi hii inaelekea siko! Kwanza aache kuwaingilia CDM kwenye sare yao. Vipi ccm mmeichoka kijani siku hizi mpaka muwaige Chadema?
 
Back
Top Bottom