Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

Hivi hii nchiiii tulikosea wapi??Yaani yanayoendelea Kenya CCM hawayaoni bado wanawaza kutuchagulia viongozi.
 
Ndani Ya Chama Uhuru Unatakiwa
Watu Waombe Form, Siyo Eti Maneno Ya Ally Kessy Tutamlazimisha
Mambo ya kijinga sana. Eti wa-print Fomu moja tu. Sasa kama Mgombea Ni Mmoja ndani ya Chama unatoa Fomu ya nini? Hivi maana ya Fomu Ni nini? Au hatuelewi maana ya Fomu? Hivi Hawa watu walisomea Ujinga?
 
Me nafikiri wawe wanasema panapo majaaliwa, Mungu akipenda, mapenzi yake mola, hiki/huyu atakuwa hivi au vile. Sote tu wanadamu hatuijui kesho yetu.
 
weka akiba ya maneno kijana,kuna watu walishakufulu na kutaka kumchagua kiongozi mmoja awe rais wa milele,ila Mungu akaingilia kati akaamua ugomvi
 
tabia ya shaka niyakukemewa watanzania huwezi kuwaamulia hata siku moja labda ni raisi wa ccm hadi 2030 nachojuwa watanzania wataamua nani awe raisi wao
 
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka. Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongeza Rais Samia huko Unguja leo hii, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025, inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za mwenyezi Mungu mpaka 2030. Ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba, desturi, utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Ni kweli Rais Samia na Mwinyi ni watulivu.Lakini maoni aliyotoa katibu ni ya chama kimoja na ni ya kizamani.Angesema hivi "Natamani kuona watanzania wakiwachagua tena......"2025
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom