Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,542
- 2,172
Kwenye muundo wa serikali, yeye ni nani? Wadhifa wake?
Serikali ni mtoto wa Chama hili nalo hujui?
Kwenye muundo wa serikali, yeye ni nani? Wadhifa wake?
|Nawasalimu kwa jina la JMT,
|Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kuhamasisha uhai wa Chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kupokea taarifa za mashina na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika Mkoa wa Mtwara|
|Shaka ameonekana kutoridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025,Pamoja na serikali kutoa 157.8BL kwaajili ya Ukarabati wa bandari ya Mtwara kwaajili ya kutoa ajira mpya kwa Watanzani mradi bado unasuasua hali iliyopelekea Shaka kutoa Kalipio kali kwa Uongozi wa Mkoa wa Mtwara|
|Shaka amewaonya vikali watendaji wa Serikali wanaotaka kukwamisha maendeleo ya Watanzania na kwakufanya hivyo Wanamkwamisha Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuharakisha na kurahisisha maendeleo ya Wanamtwara na Watanzania kwa ujumla wake |
Kwani nani aliipoteza CCM kwa wananchi? CCM bila Polisi na tume ya uchaguzi+wakurugenzi hatuna uwezo hata wa kushinda majimbo matano.Huyu jamaa nauhakika atairudisha CCM kwa watu zaidi,
Shaka amekuwa too humble down the earth,
View attachment 1943168
Ndilo jibu la swali langu?😳Serikali ni mtoto wa Chama hili nalo hujui?
Nimekwambia serikali kivuli, Umesahau Kinana na Mama Migiro vyeo vya awamu ile ya nne?. CCM ndio mmiliki wa ilani inayotumiwa na serikali kuu.Kwenye muundo wa serikali, yeye ni nani? Wadhifa wake?
Mbona sielewi, yaani kucheza ngoma na wananchi ndio maendekeo. wananchi wanataka results sio eti kiongozi kukaa na wananchi kijiweni kunywa kahawa ndio mumsifie
Mbona alichokisema kipo hapo kwenye hiyo video umeifungua kwani?mbona sielewi, yaani kucheza ngoma na wananchi ndio maendekeo. wananchi wanataka results sio eti kiongozi kukaa na wananchi kijiweni kunywa kahawa ndio mumsifie
|Nawasalimu kwa jina la JMT,
|Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kuhamasisha uhai wa Chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kupokea taarifa za mashina na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika Mkoa wa Mtwara|
|Shaka ameonekana kutoridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025,Pamoja na serikali kutoa 157.8BL kwaajili ya Ukarabati wa bandari ya Mtwara kwaajili ya kutoa ajira mpya kwa Watanzani mradi bado unasuasua hali iliyopelekea Shaka kutoa Kalipio kali kwa Uongozi wa Mkoa wa Mtwara|
|Shaka amewaonya vikali watendaji wa Serikali wanaotaka kukwamisha maendeleo ya Watanzania na kwakufanya hivyo Wanamkwamisha Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuharakisha na kurahisisha maendeleo ya Wanamtwara na Watanzania kwa ujumla wake |
Ondokana na uchama kwanza, hana mamlaka yoyote kwenye serikali ya JMT. Kama ana-issues na watu wenye kadi za chama walioko serikalini, awaite chamani na ku-deal nao kichama. Muundo wa dola hauna Katibu mwenezi wala KM CCM.Nimekwambia serikali kivuli, Umesahau Kinana na Mama Migiro vyeo vya awamu ile ya nne?. CCM ndio mmiliki wa ilani inayotumiwa na serikali kuu.
Akili chafu ya kwako mkuu inaishia kulalamika kuanzia January mpaka December. Haina jipya hata moja.Ondokana na uchama kwanza, hana mamlaka yoyote kwenye serikali ya JMT. Kama ana-issues na watu wenye kadi za chama walioko serikalini, awaite chamani na ku-deal nao kichama. Muundo wa dola hauna Katibu mwenezi wala KM CCM.
Zaidi, chama kilichokuwa madarakani miaka 60, kinachopiga maTrilioni ya shilingi za waTZ, kimeshindwa kuujenga hata mji mmoja ukakamilika, yaani chukulia mfano, wangeamua kuwa kila mwaka tunakamilisha sekta moja ya mkoa wa Dar, kwa hiyo miaka 60, unadhani tatizo la usafiri Dar lingekuwepo? Mafuriko jangwani yangekuwepo kila mwaka? Tatizo la maji safi na salama lingekuwepo? Makazi holela na ardhi isiyopimwa ingekuwepo? Yaani Dar tu peke yake, ikiwa ndio kamkoa kadogo kabisa kuliko vyote na kenye population kubwa zaidi na mapato ya juu kabisa TZ, imewashinda, ni maendeleo yapi mnaweza kuyasema kuwa yanabeba taswira ya utawala wa chama chenu kwa miaka 60? Wizi uliofanywa na wanachama ukijumlisha, ni zaidi ya bajeti ya nchi kwa miaka 10 taslimu.
Akili chafu za kilafi za kichama ndio umasikini wa ngozi nyeusi. Kwa akili za weupe, leo tuna maeneo kama Upanga, Masaki, Mbezi beach, Mikocheni, Posta, Kariakoo ambayo yamepangiliwa toka enzi za "Black n white", akili za mkoloni mweupe zimetupa barabara ya kwanza mpaka ya 13 Tanga kwa mpangilio maalumu.
sawia bwana Shaka...irudishe tu kwa wananchi.Kwani nani aliiondoa huko kwa watu?Huyu jamaa nauhakika atairudisha CCM kwa watu zaidi,
Shaka amekuwa too humble down the earth,
View attachment 1943168
Katibu mwenezi wa CCM chama ambacho ilani yake inafanyiwa kazi nchi nzima kwa sasa. Kwa maneno mengine huyo ni bosi kivuli wa serikali yote iliyo madarakani kwa sasa.
Katibu mwenezi wa CCM chama ambacho ilani yake inafanyiwa kazi nchi nzima kwa sasa. Kwa maneno mengine huyo ni bosi kivuli wa serikali yote iliyo madarakani kwa sasa.
Mkuu wewe ni mgeni wa Tanzania yetu hii?. Unaandika kama vile kipindi kile Mama Migiro na Mzee Kinana wanazunguka nchi nzima kuisema serikali wewe haukuwa unaelewa nini kinaendelea hapa TZ.Haiko sawa kabisa.
Link ya chama na serikali ni waziri au baraza la mawaziri. Pia maRC na maDC. Hao ndio wateule wa kisiasa wenye dhamana na nyenzo za kuhakikisha kuwa ajenda/ilani ya chama tawala inazingatiwa kwa ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za serikali.
Watendaji wa chama tawala hawana dhamana (mandate) ya kuagiza au kuhoji watendaji wa serikali moja kwa moja kuhusu shughuli za serikali. Hawana undani wa shughuli hizo. Wanatakiwa kuwahoji mawaziri, maRC na maDC katika VIKAO VYA CHAMA kuhusu mapungufu wanayoyaona kwenye maeneo yao.
Muhimu zaidi, ieleweke kuwa watendaji wa serikali HAWATEKELEZI ilani ya chama chochote cha siasa. BALI wanatekeleza sera, mipango na miradi iliyoidhinishwa na Bunge na Halmashauri katika ngazi ya serikali kuu na serikali za mitaa. Chama tawala hakiwakilishi muafaka (consensus) wa kitaifa kuhusu maendeleo ya nchi bali ni Bunge na mabaraza ya uwakilishi kama halmashauri. Serikali ni mtekelezaji wa consensus hiyo. Hata ilani za vyama vingine nazo huchangia katika muafaka huo kupitia Bunge/halmashauri.
Wafanyakazi wa serikali wanatakiwa kuwa neutral kwa vyama vya siasa wakati wote. Muhimu kwao ni maazimio ya Bunge, sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa rasmi kwa kadiri zilivyotafsiriwa na kuainishwa katika maeneo yao ya kazi, period.
Chama tawala kupitia mawaziri wake kinatakiwa kuandaa mapendekezo ya sera, mipango na miradi, kuiwasilisha Bungeni na kuitetea katika mijadala husika. Inatarajiwa watakuwa wamefanya mawasiliano ndani ya chama chao kuhusu vipengele vya ilani vya kuzingatiwa katika mapendekezo hayo. It’s a matter selling your agenda to obtain the necessary legislative mandate. Yale yatakayokubaliwa na kuidhinishwa na Bunge ndiyo hupelekwa serikalini kwa utekelezaji. Yatakayokataliwa huwekwa kapuni au kurudishwa kwa marekebisho au kuahirishwa.
Tatizo kubwa la Tanzania ni kubomolewa kwa misingi ya mgawanyo wa madaraka, mamlaka ya taasisi muhimu za maamuzi na utendaji na ubinafsishaji wa mamlaka yote kwa Rais na chama tawala. Ndio kinachopelekea huu upuuzi wa watendaji wa chama tawala kufokea watendaji wa serikali, vyombo vya dola na makandarasi kuhusu kazi na miradi ya serikali ilhali hawana madaraka wala uwezo huo kitaasisi na kiufundi (technical).
Tuna kazi kubwa sana ya kufanya marekebisho ya kikatiba kuweka sawa mambo haya. Kazi hiyo isipofanyika, Tanzania itakamilisha safari yake ya kuwa BANANA REPUBLIC exactly kama ilivyo Equatorial Guinea.
OkAkili chafu ya kwako mkuu inaishia kulalamika kuanzia January mpaka December. Haina jipya hata moja.
Mngekuwa mnafikiria tofauti na CCM wenye akili wangeshaona kitambo sana. Mbowe alipewa pesa na Sabodo milioni 600 ajenge chama akazipeleka kujenga hoteli yake!. Hapo bado yupo upinzani anakuwa na akili za kifisadi namna hii akipewa nchi itakuwaje?.
Unalalama kama umekunywa pombe iliyokwisha ku-expire kitambo sana. Unasahau kuna ndege nyingi tu zinaruka eneo lote hili la afrika mashariki na kati mpaka India.
Unasahau kuwa viwanja ya ndege vinajengwa karibu kila mkoa, unasahau barabara zinajengwa kila mkoa na nchi inazidi kufunguka. Huo umeme unaotumia kunijibu mimi unasahau ni kazi ya CCM! Pole sana kijana.
Sina ugeni wowote na nchi hii. Bahati mbaya hatufahamiani hapa. Naelewa kila kitu unachosema na usichosema kuhusu nchi hii. It simply is a rotten system hurtling down to the dogs. Hakuna cha kuchangamkia hapa. Ndio message yangu hata kama utaona haina maana.Mkuu wewe ni mgeni wa Tanzania yetu hii?. Unaandika kama vile kipindi kile Mama Migiro na Mzee Kinana wanazunguka nchi nzima kuisema serikali wewe haukuwa unaelewa nini kinaendelea hapa TZ.
Mpaka utakapofanyika huo mgawanyo wa madaraka haya yote uliyoyaandika yatakuwa hayana maana yoyote.
Mkuu wewe ni mgeni wa Tanzania yetu hii?. Unaandika kama vile kipindi kile Mama Migiro na Mzee Kinana wanazunguka nchi nzima kuisema serikali wewe haukuwa unaelewa nini kinaendelea hapa TZ.
Mpaka utakapofanyika huo mgawanyo wa madaraka haya yote uliyoyaandika yatakuwa hayana maana yoyote.
Mitego ya Rais Samia ya Royal Tour yanasa TZS 158.4bl | Hoteli nne kubwa za kitali hadhi ya Kempinski kujengwa Serengeti, Ngorongoro,Manyara & Tarangire,Jibu Mswali haya kwa Ukamilifu,
1.Rais Mnyenyekevu Africa -SAMIA
2.Rais mpole Africa -SAMIA. √
3. Rais mchamungu Africa -SAMIA √
4. Rais rafiki wa wananchi wake Africa -SAMIA √
5. Rais Chaguo la Watanzani 2025-2030 -SAMIA √