Shaka: Tumeahidi ajira milioni 8 kwenye Ilani ya CCM, tumetoa Tshs 157.8 Bilioni kwa ajili ya ukarabati wa bandari ya Mtwara

Hawa ndio aina ya viongozi CCm inapaswa kuwatunza. Wamekulia chamani na sio Mamluki kama wengine. Wamewekwa pembeni kidogo wameanza mipasho na kujifanya wakosoaji.

Kwa mwenendo wa Shaka naamini chama kinaandaa viongozi makini wa Sasa na baadae. Aendelee kuchapa kazi. Na hasa aweke msisitizo kwenye hiyo bandari ya kimkakati inayoweza kuhudumia Tz,Malawi,Zambia na Kaskazini ya Msumbiji.
 
Ooh yes! Alitakiwa Shaka afanye haya;

1. Amwite mkandarasi na msimamizi wa mradi

2. Aombe program of work, je hela zimekuja, kitu gani kinakwamisha, na hatua achukue hapohapo

..mkandarasi anapokea maagizo toka kwa mamlaka iliyosaini mkataba naye, na hapo inawezekana ni mamlaka ya bandari Tanzania.

..shaka hana utaalamu unaomuwezesha kukagua mradi wa ujenzi wa bandari. nashauri kazi na maamuzi ya kitaalamu tuwaachie wataalamu.
 
Shaka nilitegemea unakuta mradi unasua sua maamuzi yanachukuliwa. Lakini kufoka haitosaidia. Unaondoka hapo wanarudi kule kule.
Ahahahaa hapa ndipo unasema tumkumbuke Legendary late Pombe, tunajua nini kingefuata baada ya kusuasua...
 
Shaka Mashinani,

IMG-20210917-WA0076.jpg
 
|Nawasalimu kwa jina la JMT,

|Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kuhamasisha uhai wa Chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kupokea taarifa za mashina na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika Mkoa wa Mtwara|

|Shaka ameonekana kutoridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025,Pamoja na serikali kutoa 157.8BL kwaajili ya Ukarabati wa bandari ya Mtwara kwaajili ya kutoa ajira mpya kwa Watanzani mradi bado unasuasua hali iliyopelekea Shaka kutoa Kalipio kali kwa Uongozi wa Mkoa wa Mtwara|

|Shaka amewaonya vikali watendaji wa Serikali wanaotaka kukwamisha maendeleo ya Watanzania na kwakufanya hivyo Wanamkwamisha Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuharakisha na kurahisisha maendeleo ya Wanamtwara na Watanzania kwa ujumla wake |
Mlituambia kuwa wapinzani ndio wanawakwamisha kuleta maendeleo na mkafanya figisu kwenye uchaguzi mkawa wenyewe, sasa malalamiko ya nini tena?
 
Mwanamke wa kwanza kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa la 76 tangu tupate uhuru ni Mama Samia Suluhu Hassan,

We Proud on you Mama
_________________________

IMG-20210918-WA0036.jpg
 
Shaka fukuza hao wezi,

Acha kucheka na kima,

Fukuza majizi,

Kamata majizi,

____________________________________
Shaka yeye anawakilisha chama tawala CCM maamuzi ya kufukuza ni ya Kiserikali zaidi hapo Shaka ni kuwataka au kupendekeza hatua zaidi kwa wenye dhamana za uteuzi kutengua na kufukuza, au mimi ndio sielewi mambo ya kiutawala?

#Mama 2025
 
Hawa ndio aina ya viongozi CCm inapaswa kuwatunza. Wamekulia chamani na sio Mamluki kama wengine. Wamewekwa pembeni kidogo wameanza mipasho na kujifanya wakosoaji.

Kwa mwenendo wa Shaka naamini chama kinaandaa viongozi makini wa Sasa na baadae. Aendelee kuchapa kazi. Na hasa aweke msisitizo kwenye hiyo bandari ya kimkakati inayoweza kuhudumia Tz,Malawi,Zambia na Kaskazini ya Msumbiji.

nakubaliana na wewe 100%
Shaka ni hazina sana,
 
|Nawasalimu kwa jina la JMT,

|Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kuhamasisha uhai wa Chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kupokea taarifa za mashina na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika Mkoa wa Mtwara|

|Shaka ameonekana kutoridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025,Pamoja na serikali kutoa 157.8BL kwaajili ya Ukarabati wa bandari ya Mtwara kwaajili ya kutoa ajira mpya kwa Watanzani mradi bado unasuasua hali iliyopelekea Shaka kutoa Kalipio kali kwa Uongozi wa Mkoa wa Mtwara|

|Shaka amewaonya vikali watendaji wa Serikali wanaotaka kukwamisha maendeleo ya Watanzania na kwakufanya hivyo Wanamkwamisha Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuharakisha na kurahisisha maendeleo ya Wanamtwara na Watanzania kwa ujumla wake |
💪👊👋👍😍
 
Hawa ndio aina ya viongozi CCm inapaswa kuwatunza. Wamekulia chamani na sio Mamluki kama wengine. Wamewekwa pembeni kidogo wameanza mipasho na kujifanya wakosoaji.

Kwa mwenendo wa Shaka naamini chama kinaandaa viongozi makini wa Sasa na baadae. Aendelee kuchapa kazi. Na hasa aweke msisitizo kwenye hiyo bandari ya kimkakati inayoweza kuhudumia Tz,Malawi,Zambia na Kaskazini ya Msumbiji.
Huyu naye si alipataga kashfa ya ugasho ....
 
Back
Top Bottom