Shaka: Tumeahidi ajira milioni 8 kwenye Ilani ya CCM, tumetoa Tshs 157.8 Bilioni kwa ajili ya ukarabati wa bandari ya Mtwara

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,984
4,083
Nawasalimu kwa jina la JMT,

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kuhamasisha uhai wa Chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kupokea taarifa za mashina na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika Mkoa wa Mtwara.

Shaka ameonekana kutoridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025,Pamoja na serikali kutoa 157.8BL kwaajili ya Ukarabati wa bandari ya Mtwara kwaajili ya kutoa ajira mpya kwa Watanzani mradi bado unasuasua hali iliyopelekea Shaka kutoa Kalipio kali kwa Uongozi wa Mkoa wa Mtwara.

Shaka amewaonya vikali watendaji wa Serikali wanaotaka kukwamisha maendeleo ya Watanzania na kwakufanya hivyo Wanamkwamisha Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuharakisha na kurahisisha maendeleo ya Wanamtwara na Watanzania kwa ujumla wake.

 
#SHAKAMASHINANI

IMG-20210917-WA0066.jpg
 
Back
Top Bottom