Shaka, tukusikilize wewe na CCM au Serikali?

Wananchi hawakumchagua mkuu wa mkoa au Wilaya

Watu waliichagua CCM na CCM ndio ikaweka hao watu
Ni Mara nyingi ccm imeingilia utendaji wa viongozi iliyowaweka madarakani.

Ukimteua mtu akufanyie jambo fukani,maana yake umemwamini,huna shaka nae.
Kumsimamia siyo na wewe kutoa matakamko kinyumbe na ukiyemteua.

Utasikia kiongozi wa ccm anazungukia miradi ya maendeleo,( hili siyo baya)
Zungukia ukiona kasoro,mwite muhusika muhojiane mkosoane na kama kuna tamko mpe akalitoe. Kutoa matamko ni sawa na kujikosoa kwamba hukuwa makini kwenye uteuzi. Kama kuna mtendaji amekosea na unataka aondolewe ipo ngazi ya juu yake iagize hiyo itekeleze ulichoamua.

Utaona kabla ya serikali kutoa tamko,ccm imeshatoa tamko,sasa hao uliowaweka madarakani wanakazi gani?

Ccm ndiyo iliyotuchafulia Mimi yetu toka enzi za magufuli.
Wameona vijana ni wengi hivyo ili kupata kura zao imewaruhusu wafanyebiashara popote bila kujali sheria.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mtindo huu tutegemee vurugu tu kuhusu utendaji wa serikali ya CCM

Hivi chama tawala kinaisimamia vipi serikali yake? Mkuu wa mkoa kwa mfano wa Dar anatoa maagizo bodaboda na bajaji wasiingie mjini halafu katibu mwenezi wa CCM shaka anatoa agizo wakati huohuo uamuzi wa mkuu wa mkoa ni makosa usifuatwe huo ni mwelekeo gani kwenye utawala.

Ni CCM inaongoza nchi mambo ya siku hadi siku au wao wanaotoa sera na dira ya kufuatwa na serikali yao.

Shaka sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu na kuleta fujo tu kwenye uongozi wa nchi. Ni mtu hata haelewi mipaka ya majukumu yake.

Kwa macho ya wajuzi wa utawala amejipa majukumu ya katibu mkuu wa CCM na sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu. Kiutaratibu chama kupitia Katibu Mkuu wake wangeongee japo na waziri mkuu kuhusu uamuzi wa mkuu wa mkoa kama wangeona kuna kasoro sio kufuta uamuzi wa mkuu wa mkoa.

Shaka anaonekana hana weledi na ana papara na wasiwasi kulinda maslahi binafsi ya kisiasa ya aliyemteua badala ya kuacha watendaji wa serikali wafanye kazi yao

6263B9C9-E6C9-48ED-91A2-E1F0AD0F26FA.jpeg
 
Ni mtu mbovu sn
 
Jambo moja tu, BODABODA na MACHINGA watu hawalali. Jeshi la polisi lilitoa tamko kufuatia taarifa za ki-intelijensia kwamba bodaboda wasiingie mjini, mkuu wa mkoa akaona kichwa bado kinauma sababu ya machinga akapindua tamko la polisi, Shaka akaona Katibu mkuu wa CCM akimtangulia kusema atakosa cha kuongea akadandia kauli ya mkuu wa mkoa, msemaji wa serikali akaona mama akisikia hajaongelea akirudi itakuwa noma, na yeye akasimama juu ya kichwa cha Shaka.

Ukitokea ujambazi wa aina yoyote Posta jeshi la polisi lisilaumiwe. Wao wametumia weledi, wanasiasa wanaomba urafiki na vikundi visivyokuwa kwenye mfumo.
Shida imegeuzwa kuwa ni mtaji wa kisiasa
 
Sera vyama vingi mfo chama kimoja hapo ndio tatizo linapoanza. Msimamizi wa serikali ni Bunge sababu wao ndio wanaopitisha bajeti na serikali inaendeshwa kwa bajeti, na upande mwengine Mahakama inaingia kwenye usimamizi wa serikali vile vile serikali inawasimamia Bunge na Mahakama.

Shughuli za Kimhimili hazisimamiwi na chama kufanya hivyo ni kuingilia shughuli za mihimili mingine. Tatizo tulitoka kwenye mfumo wa chama kimoja na bado kizazi cha mfumo huo kipo na kinaongoza, hadi hicho kizazi kiondoke ndio labda tutajipanga upya

Haijawa wazi sana ila ndio hivyo.
 
Kwa mtindo huu tutegemee vurugu tu kuhusu utendaji wa serikali ya CCM

Hivi chama tawala kinaisimamia vipi serikali yake? Mkuu wa mkoa kwa mfano wa Dar anatoa maagizo bodaboda na bajaji wasiingie mjini halafu katibu mwenezi wa CCM shaka anatoa agizo wakati huohuo uamuzi wa mkuu wa mkoa ni makosa usifuatwe huo ni mwelekeo gani kwenye utawala.

Ni CCM inaongoza nchi mambo ya siku hadi siku au wao wanaotoa sera na dira ya kufuatwa na serikali yao.

Shaka sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu na kuleta fujo tu kwenye uongozi wa nchi. Ni mtu hata haelewi mipaka ya majukumu yake.

Kwa macho ya wajuzi wa utawala amejipa majukumu ya katibu mkuu wa CCM na sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu. Kiutaratibu chama kupitia Katibu Mkuu wake wangeongee japo na waziri mkuu kuhusu uamuzi wa mkuu wa mkoa kama wangeona kuna kasoro sio kufuta uamuzi wa mkuu wa mkoa.

Shaka anaonekana hana weledi na ana papara na wasiwasi kulinda maslahi binafsi ya kisiasa ya aliyemteua badala ya kuacha watendaji wa serikali wafanye kazi yao
Weredi ndio Tatizo.Hata Kama viongozi wametokana CCM kiongozi wa CCM Hana haki wala uwezo wa kutoa amri kwa watumishi wa umma au viongozi wa kisiasa nje na mikutano ya Chama.Alichopaswa ni kutoa mapendekezo ya CCM Kama chama cha siasa.Watu huwa hawajifunzi kwa akina Mangula namna ya kusisitiza utelelezaji wa ilani.
 
Shaka ana kiherehere mpaka kimepitiliza, anataka kuiga ile style ya Kinana kufuatilia watendaji wa serikali lakini kiherehere chake kinasababisha anavuka mpaka.
 
Kuna mijitu sijui shule ilikimbia ama kujaza mi post humu kwani ni chama gani ndo kimeshikilia serikali ama mmetumwa kuja kumchafu kijana.CCM ndo kiko madarakani huyo mkuu wa mkoa akiharibu halalamikiwi yy ni chama kilichomuamini na kumuweka hapo.Muwe pia mnasikiliza vizuri kijana kasema wakae washilikiane na kamati mbali mbali walijadili swala hili kwa mapana sio mtu anakaa anatoa maagizo bila kujua madhara yatakayo patikana kwenye maslahi ya taifa na chama.
Siyo kila kiongozi ni mtawala. Mtawala hutambuliwa kwa himaya yake (territory), hivyo basi

1. Mkuu wa mkoa ni mtawala na pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika himaya yake. Wanausalama wana jukumu la kumshauri kuhusu mambo ya usalama na cha kufanya kwa wakati husika.

2. Katibu wa chama (NEC, itikadi na uenezi) ni kiongozi na si mtawala. Mwenye himaya/nchi ni mwenyekiti wake. Hivyo hakupaswa kutweza maamzi ya mtawala kwa namna ile. Ikumbukwe kuwa yeye hawezi kufanya mkutano ama shughuli yoyote ndani ya himaya ya mkuu wa mkoa pasipo kumfahamisha.

3. Viongozi wote kwa pamoja wanauhudumia umma ule ule kwa malengo sawa. Ni busara sana kuwasiliana kwa sitaha na kwa uhakika bila kudharauriana.
 
Sawa mkuu ila pia maamuzi mengi hua lazima yapate baraka za chama sasa km chama hakikuhusishwa na hili ni sawa chama kuingilia kati maana tangazo limetolewa kwenye vyombo vya habari sasa na chama kingekaa kimya kingeonekana hakisimami na wananchi.Pia mkuu bado machinga wanalia uongeze tena kundi jingine kuliondoa lawama zote zitaenda chamani.
 
Kwa mtindo huu tutegemee vurugu tu kuhusu utendaji wa serikali ya CCM

Hivi chama tawala kinaisimamia vipi serikali yake? Mkuu wa mkoa kwa mfano wa Dar anatoa maagizo bodaboda na bajaji wasiingie mjini halafu katibu mwenezi wa CCM shaka anatoa agizo wakati huohuo uamuzi wa mkuu wa mkoa ni makosa usifuatwe huo ni mwelekeo gani kwenye utawala.

Ni CCM inaongoza nchi mambo ya siku hadi siku au wao wanaotoa sera na dira ya kufuatwa na serikali yao.

Shaka sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu na kuleta fujo tu kwenye uongozi wa nchi. Ni mtu hata haelewi mipaka ya majukumu yake.

Kwa macho ya wajuzi wa utawala amejipa majukumu ya katibu mkuu wa CCM na sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu. Kiutaratibu chama kupitia Katibu Mkuu wake wangeongee japo na waziri mkuu kuhusu uamuzi wa mkuu wa mkoa kama wangeona kuna kasoro sio kufuta uamuzi wa mkuu wa mkoa.

Shaka anaonekana hana weledi na ana papara na wasiwasi kulinda maslahi binafsi ya kisiasa ya aliyemteua badala ya kuacha watendaji wa serikali wafanye kazi yao
kama rais aliweza kutumia mali za serikali kama magari nk na kwenye ziara hiyo hiyo akafanya mambo ya kichama kwa kuwa ni mwenyekiti, unasemaje hapo
 
Kwa mtindo huu tutegemee vurugu tu kuhusu utendaji wa serikali ya CCM

Hivi chama tawala kinaisimamia vipi serikali yake? Mkuu wa mkoa kwa mfano wa Dar anatoa maagizo bodaboda na bajaji wasiingie mjini halafu katibu mwenezi wa CCM shaka anatoa agizo wakati huohuo uamuzi wa mkuu wa mkoa ni makosa usifuatwe huo ni mwelekeo gani kwenye utawala.

Ni CCM inaongoza nchi mambo ya siku hadi siku au wao wanaotoa sera na dira ya kufuatwa na serikali yao.

Shaka sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu na kuleta fujo tu kwenye uongozi wa nchi. Ni mtu hata haelewi mipaka ya majukumu yake.

Kwa macho ya wajuzi wa utawala amejipa majukumu ya katibu mkuu wa CCM na sasa anajipa madaraka ya waziri mkuu. Kiutaratibu chama kupitia Katibu Mkuu wake wangeongee japo na waziri mkuu kuhusu uamuzi wa mkuu wa mkoa kama wangeona kuna kasoro sio kufuta uamuzi wa mkuu wa mkoa.

Shaka anaonekana hana weledi na ana papara na wasiwasi kulinda maslahi binafsi ya kisiasa ya aliyemteua badala ya kuacha watendaji wa serikali wafanye kazi yao
Huyo ana hasira na 'legacy' ya JPM kutuhumiwa ni mla rushwa kutoka kwa madiwani akiwa mwenyekiti wa CCM Morogoro kupitisha meya asiye na sifa sijui aliwezaje kuchaguliwa kuwa kiongozi kwenye mkoa wa wastaarabu kiasi hicho

Vitisho vingi badala ya kueneza falsafa za chama kwa lugha rafiki na kwa kuheshimu waliokuwa viongozi wake

Waliokuwa wanamchukia JPM ndani ya chama ndio waliopewa vyeo kuonesha hasira zao, je mteuzi wao anajisikiaje mtangulizi wake kusemwa vibaya na kudharirishwa bila kukemea wakati mambo mengine anakemea?
 
Sawa mkuu ila pia maamuzi mengi hua lazima yapate baraka za chama sasa km chama hakikuhusishwa na hili ni sawa chama kuingilia kati maana tangazo limetolewa kwenye vyombo vya habari sasa na chama kingekaa kimya kingeonekana hakisimami na wananchi.Pia mkuu bado machinga wanalia uongeze tena kundi jingine kuliondoa lawama zote zitaenda chamani.
La machinga lina baraka za chama 'wapangwe' hilo ni la taifa.
Kila mkoa una kamati ya siasa ya chama ambapo RC ni mjumbe. Mwenyekiti wa chama mkoa kazi yake ni nini basi kama atasubiri boss wake alione pasipo yeye kuwa wa kwanza? Si unaona vile katibu ngazi ya taifa kateleza!
Hata hivyo wacha waparuane wenyewe kwa wenyewe wamalizane.
 
CCM ndicho chama kilichounda serikali hivyo viongozi wa chama wanasimamia uwendshaji wa serikali. Hata hivyo Mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa chama. Angesema kwa niaba ya Mwenyekiti angeeleweka.

SI SAWA. Chama cha siasa hata chama tawala hakina mamlaka ya kuisimamia serikali moja kwa moja. Uhusiano wa chama na serikali uko kupitia Bunge.

Serikali huwa haitekelezi ilani wala maagizo ya chama tawala. Bali inatekeleza maazimio ya Bunge na sheria zilizopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais - sio mwenyekiti wa chama tawala. Akivaa kofia ya uenyekiti wa chama basi hana uwezo wa kuisimamia serikali moja kwa moja kwa maana ya kutoa maagizo na maonyo bali anaweza kujadiliana/kushauriana na mawaziri na wabunge wa chama chake.

Si kila kilicho kwenye ilani ya chama ni cha kutekelezwa. Lazima kiandaliwe muswada (bill), uwasilishwe Bungeni, kujadiliwa na wabunge wote na kupitishwa na wabunge wengi kisha kuwasilishwa kwa Rais na kusainiwa (executive formality). Kuna mengine yanaweza kukataliwa (kama tuna Bunge makini linalopigania maslahi ya wananchi). Na mengine ya upinzani yanaweza kuchukuliwa na kuongezewa katika miswada hiyo. Ni kazi ya serikali na wabunge wa chama tawala kupigania vipengele vya ilani yao katika miswada ya serikali vipitishwe Bungeni. Ndipo viende serikalini kutekelezwa.

Tatizo ni kwamba kinachoendelea Tanzania ni JEURI YA CHAMA (CCM) ndiyo inatawala nchi baada ya miaka mingi kiasi kwamba wengi wamesahau hata kupuuza kabisa mfumo sahihi wa nafasi ya vyama vya siasa katika uongozi wa nchi. Ni ujinga mkubwa (tragic ignorance) unaochangia kuangamiza taifa.

Unakuta kiongozi wa serikali au CCM anadai watumishi wote wa serikali lazima wawe na ilani ya CCM! Kwamba wajue wanatekeleza ilani ya CCM! Asiyetaka aache kazi! Watendaji wa CCM wanazunguka kila mahali na wanaamrisha na kufokea maafisa wa vyombo vya dola na watendaji wa taasisi za serikali kama vile wako kwenye chain of command ya taasisi/vyombo hivyo. Utafikiri hakuna mtu aliyeelimika kuhusu mambo hayo nchini atoe mwongozo sahihi. Mtu yeyote aliyeko kwenye senior position serikalini lazima ajue hili. Labda kama tunakubali kuwa serikalini kumejaa mazuzu.
 
Anayo haki ya kuwatetea wapiga kura wake,2025 ye ndie atakaeulizwa na sio Makala
 
Kauli ya Shaka kutengua amri ya mkuu wa mkoa inaonesha umuhimu wa ulazima wa katiba mpya, serikali za nchi zenye mfumo wa vyama vingi serikali ndiyo huongoza nchi na wananchi tunatakiwa tuisikilize serikali na si vinginevyo.

Bahati mbaya hivi sasa CCM imejipa jeuri ya kuidharau serikali na kutuaminisha sisi kuwa CCM ndiyo yenye amri zote nchini!

Kitendo cha CCM kinaondoa uhalali wa serikali kuwepo jambo ambalo halina afya kwa taifa.

Pia soma:

Thread 'Shaka apiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia katikati ya Mji wa Dar' Shaka apiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia katikati ya Mji wa Dar
Tusubiri kuona. Ukongwe ( > 60 yrs) unasumbua sana.
 
Isikilize CCM. CCM ndio walipita mitaani kuomba kura na mkawapa kura, ccm ikaunda serikali
Huelewi sio kosa lako. Tunaongozwa na serikali ya ccm sio ccm. Ccm yenyewe ina viongozi wake. Baada ya kushinda uchaguzi wanachagua baraza la mawaziri rais na mawaziri wanaongoza nchi. Sio tena kina shaka kutoa maagizo bila kupitia serikali. Hiyo sio sawa waache upuzi wao.
 
Back
Top Bottom