Shaka: TFS mkimaliza kuwavunja miguu vijana wote nguvu kazi ya Taifa itatoka wapi?

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
2,154
2,000
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu yanayowahusu wakala wa misitu Tanzania (TFS) kupiga wananchi wetu hadi kuwavunja miguu kwa kisingizo cha kuwakamata na mkaa au kuwabambikizia kesi zisizo na msingi wowote wa kisheria,Kuanzia leo iwe mwanzo na mwisho, Serikali ya Mama Samia imejipambanua tusimamie sheria bila kuleta mateso|manyanyaso na hata udhalilishaji uliopitiliza|

|Chama Cha Mapinduzi kitamuelekeza Waziri Wa Maliasili na Utali Dk Ndumbaro juu ya kadhia hii, Vijana wake wakishawamaliza kuwavunja miguu vijana wote nguvu kazi ya Taifa hili itatoka wapi?

Nyakati zote Rais Samia amekuwa akisimama na Wananchi wake kamwe hatuwezi kufumbia macho uchonganishi huu kwa kisingizio eti kuvunja sheria|

|CCM haitakubali kuona wananchi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu wakiishi kama wakimbizi katika kwenye nchi yao. TFS acheni uonevu na unyanyasaji wa wananchi wanaopakana na misitu hususan hapa Jimbo la Ushetu| alisema Shaka

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Kahama Kampeni CCM.

IMG-20211008-WA0018.jpg


IMG-20211008-WA0020.jpg


IMG-20210927-WA0050.jpg


IMG-20210927-WA0014.jpg


IMG-20210918-WA0078.jpg


IMG-20210916-WA0054.jpg
 

ABC ZA 2020

JF-Expert Member
May 2, 2018
635
500
Watu hawashtuki tu Serikali ya Rais Samia niya "UTU" sana, Lazima waache mambo ya kuwabambika watanzania kesi na kuwavunja miguu halikubaliki kabisa,

Shaka amekuwa kiongozi mwenye utu sana nafsini mwake kwenye hili tunamuunga mkono 100%,Tusikubali watu wamchonganishe Rais na wananchi wake,
 

AGGGOT TZ

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
735
500
Shaka fukuza hao pumbafu kabisa,

Wanavunja watu miguu wamewazaa?

Nyie Magemu nawachukia sana kabisa,

CCM safi sana kusimama na wananchi,

Mama Samia hawa wanakuharibia sana kama hujui
 

Almighty

JF-Expert Member
May 27, 2020
602
500
Shaka usionee huruma mtu fukuza kabisa,

Kwanini watese watu wetu?

Fukuza na anza na waziri wao,

Tunataka serikali inayoheshimu watu wake zama za uonevu zilikufa,

Chapa kazi Shaka fukuza hao wote huko Kahama
 

Mansander

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
649
1,000
Watu hawashtuki tu Serikali ya Rais Samia niya "UTU" sana, Lazima waache mambo ya kuwabambika watanzania kesi na kuwavunja miguu halikubaliki kabisa,

Shaka amekuwa kiongozi mwenye utu sana nafsini mwake kwenye hili tunamuunga mkono 100%,Tusikubali watu wamchonganishe Rais na wananchi wake,
Kwani CCM si ndiyo inatawala? sasa anajilalamikiaje mwenyewe? au CCM haina control kwamba kila chombo cha serikale yake kinajifanyia kinavyotaka? Hawa watu waache cheap politics za danganya toto
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,332
2,000
TFS tunawakumbusha.....

Moja ya MAJUKUMU ya AFISA WANYAMAPORI ni:-

Kufuatilia utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya uhifadhi wa wanyamapori.

Hapo juu haliko KUVUNJA RAIA MIGUU.
Hapo juu haliko KUUA RAIA WALIPA KODI NA MISHAHARA YENU.


Kongole kwake komredi El Comandante Shaka Hamdu Shaka👏👊😍

#SiempreJMT
#NchiKwanza
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,602
2,000
Ngoja wale pinga pinga wakitoka msalani na kuikuta habari hii... lazima watakuja na mawazo tofauti ya kupingana na Shaka. Na la kushangaza zaidi watawatetea wakala wa misitu ilimradi tu waende njia tofauti na ile ya CCM na Serikali yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom