Shaka: Kabla ya Mapinduzi Matukufu lipo tabaka lililokandamiza, kubagua na kupuuza wengine huku likishindwa kujali "UTU" na kuwapuuza walio wengi

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,448
1,003
CamScanner 01-12-2023 20.40_1.jpg

Na Mwandishi wetu Z'bar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinajivunia mabadiliko makubwa yaliyofikiwa Zanzibar katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ambayo yamewafanya wananchi kujiamini na kujiitegemea kimaendeleo alisema Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa

Aliendelea kwa kusema Zanzibar imepiga hatua kubwa sana na Chama Cha Mapinduzi inatoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa iliyokwishafanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, ikiendelea kuunga mkono juhudi za kukomesha ukandamizaji wa haki , ubaguzi, Dhulma na manyanyaso

Katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu licha ya kuleta ukombozi kamili lakini pia yamewafanya wananachi kuwa na fikra huru na kujitawala alisisitiza kwa unyenyekevu Ndg
Shaka Hamdu Shaka katibu wa NEC Itikadi & Uenezi CCM Taifa

Kabla ya mapinduzi lipo tabaka lilokandamiza, kubagua na kuwapuuza wengine huku wananachi wakikosa haki za msingi na kutotumia fursa za kiuchumi sawa na utu wao kutothaminiwa, na kupuuzwa alisisitiza Ndg Shaka Hamdu Shaka ambie pia ni Msemaji wa CCM Taifa

Aliendelea kusema, Mapinduzi ya mwaka 1964 ni ushahidi kuwa Zanzibar ilikuwa na watu waliokoseshwa elimu bora, kutomiliki uchumi, ardhi, kukosa makaazi bora na kunyimwa huduma za jamii

Hata hivyo Serikali zote SMZ (Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) na SMT (Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) zimetimiza wajibu wa kusimamia maendeleo. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais Dk. Mwinyi baada ya miaka 59 wametafsiri mapinduzi ya ukombozi kuwa Mapinduzi ya kiuchumi. Maendeleo yanayoonekana sasa hayakuwepo miaka 200 ya utawala wa kikoloni

Anasema, Kazi kubwa iliyofanywa na Chama cha ASP ilikuwa kuhakikisha utawala wa ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa huduma za jamii unakomeshwa katika visiwa vya Unguja na Pemba kwa sera ya mapinduzi ya ukombozi na kazi iliyobaki ni kujenga uchumi na maendeleo.

Anatoa angalizo, "Ni vyema kwa watendaji waliopewa dhamana katika Serikali na taasisi za umma kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kumsaidia Rais Dk. Mwinyi ili akamilikshe kazi ya kutekeleza mapinduzi ya kiuchumi na kuongeza Kasi ya kuleta maendeleo."

"Kazi ya kumwondoa mkoloni aliyetawala kwa ubaguzi na ukandamizaji imemalizika. Kazi iliyobaki ni kuongoza kwa haki, umoja na maendeleo. Kukumbuka madhila yaliyokuwepo kabla ya mapinduzi kunatupa ari ya kufikia mabadiliko tuanayoyataka,

Baada ya kufanikisha mapinduzi ya mwaka 1964 na utawala kushikwa na ASP, Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume alianza utekelezaji wa sera za maendeleo ikiwemo kutolewa bure kwa huduma za msingi"

Shaka anajivunia kazi kubwa ya CCM "Elimu imetolewa bure, maji safi na matibabu, serikali ikaweka viwango vya mishahara minono kwa mujibu wa ajira ya kila mfanyakazi, yamejengwa makaazi ya kisasa na sasa kazi hiyo inaendelezwa na serikali ya Rais Dk. Mwinyi,"

"Ni waombe watanzania wenzangu hasa vijana kutobabaishwa na porojo za baadhi ya wapinga maendeleo na mapinduzi matukufu ya 1964 ambao wamekuwa wapotoshaji wa ukweli kwa kudai serikali za CCM hazijafanya lolote tangu mwaka 1964 wakati asiliamia 98 ya maendeleo yaliyofanyika nchini yamepatikana katika utawala wa Chama Cha Mapinduzi" alihitimisha Ndg Shaka Hamdu Shaka, katibu wa NEC itikadi & Uenezi CCM Taifa.
 
Shaka ni kiongozi,

Huyu kijana anahekima sana,Kauli zake zinavutia na kuhamasisha Uzalendo kwa Taifa,
Mungu bariki Mapinduzi matukufu,
 
Na baada ya uhuru lipo tabaka linalokandamiza wengine kwa kuwabagua na kupuuzwa na watawala wa ccm huku wakishindwa kujali utu na kuwapuuza walio wengi.
Uchaga unakusumbua, Nyie Kilimanjaro hamuoni CCM mambo iliyowafanyia?
 
Nakumis sana Wewe dada, Ulipotelea wapi!? Naona Sasa Cheo Cha Machawa Sasa ni Rasmi,

🤣🤣🤣
Miss you too bro. Mmoja wa makaka bora kabisa jukwaani
Heri ya mwaka mpya na ukawe mwaka wenye baraka tele kwako
 
Back
Top Bottom