Shaka: Ikitokea kuna dalili za Uhuru wetu kutaka kuwekwa rehani na sisi tukakaa kimya tusishangae makaburi ya wasisi wetu yatakapotetemeka

Rais wa Matajiri

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
1,475
607
==
"Kazi ya kulinda tunu ya uhuru na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ni jukumu la kufa na kupona kwa kila mzalendo kwani fatiki ya kupigania uhuru imepoteza maisha na mali za watu, nguvu na jasho jingi" Shaka Mwenezi Taifa

"Urithi wa Uhuru unapaswa kuthaminiwa na watanzania wote ambao ni warithi halali bila kutazama rangi za watu wake, asili zao, makabila au imani za dini zao" Shaka Mwenezi Taifa

"Haikuwa kazi nyepesi na rahisi kwa viongozi walioasisi mapambano ya kupigania uhuru kinadharia na vitendo hivyo itakuwa kituko endapo matunda ya uhuru itashindikana kulindwa au kutetewa" Shaka Mwenezi Taifa

"Wakati Taifa likielekea kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa uliopatikana disemba 9 mwaka 1961 kwa iliokuwa tanganyika, kazi muhimu inayotakiwa kutekelezwa ni kuhakikisha uhuru huo unabaki kwa manufaa toka kizazi kimoja hadi kingine" Shaka Mwenezi Taifa

"Iwapo atatokea mtu yeyote atakayeridhia kuwa kibaraka toka miongoni au kuwapigia magoti maadui wa uhuru lazima asutwe na kumulikwa kwa macho yote mawili" Shaka Mwenezi Taifa

"Kutoweka kwa uhuru wetu ni kuhatarisha maisha na ustawi kwa kila mmoja wetu. Kupoteza uhuru ni kazi rahisi lakini ikumbukwe jukumu la kupigania uhuru limegharimu na kupoteza maisha ya babu na bibi zetu hadi kizazi hiki wakaikuta nchi ikijitawala" Shaka Mwenezi Taifa

"Uamuzi wa kuunda taifa jipya la Tanzania ambalo halikuachwa na wakoloni ieleweke haikuwa kwa njia ya mkato badala yake waasisi wa Muungano walipitisha maamuzi magumu kwa muktadha wa kupigania maslahi ya kizazi hiki na vijavyo" Shaka Mwenezi Taifa

"Ikitokea kuwa na dalili za uhuru wetu kutaka kuwekwa rehani na sisi tukikaa kimya tusishangae makaburi ya wasisi wetu yatakapotetemeka. Watanzania wasiwe tayari kuona uhuru wao ukiporwa" Shaka Mwenezi Taifa

"Kila mmoja wetu ajione ana kazi ya kulinda uhuru ili usinyakuliwe hivyo mnalo jukumu la kuhakikisha mnatunza na kueneza machapisho ya historia ya nchi yetu" Shaka Mwenezi Taifa

"Wapo watu hawafurahi na kupendezwa kutuona tukijiongoza kwa kufuata matakwa ya sera zetu. Watu hao hawataacha vituko badala yake wataendeleza maneno maneno hadi pale watakapotuona tukigawanyika na kupoteza nguvu ya mshikamano wetu" Shaka Mwenezi Taifa

Niwahakikishie wakati tukiadhimisha miaka 60 Serikali ya Rais Samia ataendelea, kuondosha vikwazo vyote ambavyo vinakwamisha utendaji wenu ikiwa ni utekelezaji wa ibara ya 80 (b)ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025" Shaka Mwenezi Taifa

HIZI NI NASAHA YAKINIFU ZA KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA ITIKADI NA UENEZI SHAKA HAMDU SHAKA WAKATI AKIONGEA NA WAANDISHI NA WACHAPISHAJI VITABU LEO 01|12|2021

photo_2021-12-01_07-45-57.jpg
 
Back
Top Bottom