Shaka Hamdu Shaka: Sukuma ndani! "Mkibaini mchwa yeyote popote wa fedha za miradi ya Umma"

2957590_Screenshot_20211008-160457_1.jpg
 
NATAKA KUHAMIA CCM WAKUU,

mimi ni chadema kitambo ila kwa sasa kwa yanayoendelea nimeamua nihamie tu CCM,
Chama na Serikali wote wananifurahisha sana na nimeridhika naweza kuishi CCM, Naombeni kadi wakuu
Hongera Chama cha Mapinduzi
Huja wahi kuwa chadema. Wewe ni kada wa ccm
 
NATAKA KUHAMIA CCM WAKUU,

mimi ni chadema kitambo ila kwa sasa kwa yanayoendelea nimeamua nihamie tu CCM,
Chama na Serikali wote wananifurahisha sana na nimeridhika naweza kuishi CCM, Naombeni kadi wakuu
Hongera Chama cha Mapinduzi
14|10|2021

Kesho Rais Samia atakuwa Chato kwenye kuzima Mwenge karibu sana
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akisoma Azimio la kumpongeza Mwenyekiti wa CCM ambaye ni amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri zilizotukuka tena zilizofanyika kwa kipindi kifupi Shaka amewataka Viongozi wote wa Kamati za Siasa kuanzia Kata, Wilaya hadi mkoa kuhakikisha hakuna senti moja ya mradi wowote wa umma|Serikali inatafunwa na aliyewaita " Mchwa " yaani majizi,

Mhe Shaka amewakumbusha Viongozi wa kamati za Siasa kuwa Chama Cha Mapinduzi ndio Chama kilichopewa ridhaa na Watanzania na ndio chenye Jukumu la kuhakikisha Wananchi wanafikiwa na huduma zote muhimu kwa wakati kwani Ilani inayotekelezwa ni Ilani ya CCM ya 2020|25,Mhe Shaka amesisitiza miradi yote ya mkopo wa IMF kwa mujibu wa Serikali itamalizika baada ya miezi tisa ( 9 ) hivyo kamati zote za Siasa zifuatilie kwa Ukaribu sana miradi hii,

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi Taifa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi hakitamvumilia yeyote atakayehusishwa na rushwa au Ufisidi wa fedha za miradi ya wananchi huku akiwataka kamati zote za Siasa kuzielekeza dola kuwafikisha michwa hao kwenye vyombo vya kisheria ikiwa ni baada ya kujiridhisha kuwako na ubadhilifu wa pesa za miradi yote zikiwemo pesa za mkopo wa TZS 1.3Trilioni toka IMF ambao Rais wetu ameupata kwa sababu tu ya imani ya Wahisani kwake na kila mtanzania atahusika kuulipa mkopo huo hivyo pesa hizo sio Sadaka zilindwe kwa wivu mkubwa,

Safi sana
 
JPM mwenyewe alikua na ubavu wa kusukuma ndani majizi, kwa serikali hii sijui, ngoja tuone...

Kwanza mama hapendi ukali wala ugomvi...
 
JPM mwenyewe alikua na ubavu wa kusukuma ndani majizi, kwa serikali hii sijui, ngoja tuone...

Kwanza mama hapendi ukali wala ugomvi...
Unacho shangaa ni nini?

Agizo la chama tayari subiri matokeo au kama na wewe muhusika jaribu uone mwoto,
 
Back
Top Bottom