#COVID19 Shaka Hamdu Shaka: Rais Samia kaonesha njia, wananchi wafanye uamuzi sahihi wa kupata chanjo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
223
500
Nukuu za Katibu wa itikadi na Uenezi CCM wakati akizungumza leo katika Uzinduzi wa Chanjo ya Uviko 19 Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hii muhimu ndani ya Taifa letu. CCM inampongeza Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ibara za 83(o) na 84."

"Tuliahidi CCM itaimarisha huduma za Afya kwa watanzania sambamba na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kuwakinga dhidi magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19. Alilofanya Rais Samia leo ni utayari wake na nia yake thabiti katika kuwatumikia watanzania na kuliongoza Taifa. "

"Uongozi ni kuonesha njia ndivyo alivyofanya Rais Samia na ndio maana viongozi na wasaidizi wake tumemuunga mkono kupata chanjo hii ya UVIKO 19 hapa ikulu. Tuwaombe wananchi waendelee kupata taarifa sahihi na wafanye uamuzi sahihi wa kupata chanjo hii. Kinga ni bora kuliko Tiba."

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
Ikulu Dar es Salaam
28 Julai 2021.

IMG-20210728-WA0038.jpg


IMG-20210728-WA0040.jpg


IMG-20210728-WA0041.jpg


IMG-20210728-WA0042.jpg
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,974
2,000
Tuliahidi CCM itaimarisha huduma za Afya kwa watanzania sambamba na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kuwakinga dhidi magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19. Alilofanya Rais Samia leo ni utayari wake na nia yake thabiti katika kuwatumikia watanzania na kuliongoza Taifa. "
Asisahau kuwa hiyo chanjo ni msaada baada ya kutokuwa na mbele wala nyuma.
 

Lucas philipo

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
1,646
2,000
Mimi nadhani kuna shida katika uelewa!!


Nianacho mimi ni wataalamu wetu waliotuaminisha katika matumizi ya "nyungu" na kuikandia Chanjo na leo wanatuambia tena inafaa kwa matumizi na haina madhara!

Kungewekwa wazi tangu mwanzo na wakaonyesha utaalamu wao kusingekuwa na haja ya kutumia nguvu katika hamasa ya chanjo!!

Ndio maana wengine wanahoji ubora wa chanjo hii.
 

mbalizi1

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
16,192
2,000
Mimi nadhani kuna shida katika uelewa!!


Nianacho mimi ni wataalamu wetu waliotuaminisha katika matumizi ya "nyungu" na kuikandia Chanjo na leo wanatuambia tena inafaa kwa matumizi na haina madhara!...
Nadhani haikuwa rahisi kukinzana na mawazo ya Magufuli ndio sababu watu baadhi waliungana naye waziwazi, wengine walilazimika na wengine walikaa kimya.

Hii yote ilitokana na hofu na uoga dhidi ya Magufuli, ndio sababu Leo hii wanatuaminisha tofauti na vile walivyotuaminisha mwanzo wakati wa utawala wa Magufuli.

Hii ndio athari ya kutawala kwa kutumia nguvu, badala ya watu kushauri vile inavyofaa wanashauri kwa kufuata mawazo ya mtawala kwa kuogopa kuonekana wanakinzana naye.
 

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
366
1,000
Na Mwandishi Wetu,
Ikulu, Dar es Salaam.
28 Julai, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameongoza viongozi mbalimbali wa serikali na kidini, wasanii na wanahabari kupata chanjo ya UVIKO-19 katika Ikulu ya Dar es Salaam ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kuendelea kufanyika kwa zoezi hilo nchini.

Wengine waliochanjwa ni waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, katibu mkuu kiongozi, viongozi wa kisiasa akiwemo katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka, viongozi wa dini, waziri wa afya Mheshimiwa Dkt Doroth Gwajima, makatibu wakuu wa wizara, waandishi wa habari, baadhi ya wasanii na viongozi wengine mbalimbali waliokuwepo.

Rais Samia amewahakikishia watanzania chanjo ni salama na lengo la kila chanjo ni kuwakinga watu dhidi ya maambukizi na hivyo basi kuokoa maisha kwa mantiki hiyo amewaomba wachanjwe dhidi ya virusi hivyo japo ni hiari kufanya hivyo.

"Mimi ni Mama wa Watoto 4, Bibi wa wajukuu, mke lakini pia Rais na Amir Jeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo nikijua nina majukumu yote haya, hii chanjo ni salama na wataalamu wetu wamejiridhisha, NIKO TAYARI Kuchanjwa, naomba mniunge mkono" Rais Samia

Akizungumza baada ya kuchoma chanjo hiyo mara baada ya uzinduzi uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hii muhimu ndani ya Taifa la Tanzania.

"CCM inampongeza Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ibara za 83(o) na 84." Alisema Shaka

Alisisitiza tuliahidi CCM itaimarisha huduma za afya kwa watanzania sambamba na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kuwakinga dhidi magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19.

"Alilofanya Rais Samia leo ni utayari wake na nia yake thabiti katika kuwatumikia watanzania na kuliongoza Taifa likiwa salama zaidi ameonesha uaminifu wake katika kutimiza ahadi. Uongozi ni kuonesha njia ndivyo alivyofanya Rais Samia na ndio maana viongozi na wasaidizi wake tumemuunga mkono kupata chanjo hii ya UVIKO 19 hapa ikulu. Tuwaombe wananchi waendelee kupata taarifa sahihi na wafanye uamuzi sahihi wa kupata chanjo hii. Kinga ni bora kuliko Tiba." Alisema Shaka

Shaka amepongeza utaratbu wa serikali wa kutoa kipaumbele kwa watu walio katika hatari ya maambukizi wakiwemo wazee na wote walio mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi katika awamu hii ya kwanza ya dozi takribani milioni moja zilizowasili.

#ChanjoNiSalama
#ChanjoNiKinga
#KuchanjaNiHiyari
#KuchanjaNiKujali

IMG_20210728_150955.jpg
IMG_20210728_152823_843.jpg
IMG_20210728_153258_031.jpg
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,385
2,000
Tumebarikiwa Tena kwa kuwa na Rais Msikivu anayetaka kuiongoza Serikali sikivu..........

Katika kipindi hiki cha mawimbi MAKALI bado mh.Rais SSH ameonesha njia ya kutaka MASILIZANO NA KUSIKILIZA SAUTI ZOTE HATA ZILE ZA NYIKANI.....

Kama mama wa watoto 4.....
Kama mke......
Kama bibi wa wajukuu kadhaa.....
Kama Amiri Jeshi Wa Majeshi ya ulinzi na usalama.......

Ameanza kuonesha USALAMA WA CHANJO HII......

TUMUUNGE MKONO KATIKA DHIMA YAKE HII KUBWA

#NaliandaaBegaLanguNikachomweJ&J
#TujitokezeKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#SiempreJMT
 

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
263
500

CCM: LAZIMA TUWAKINGE WATANZANIA DHIDI YA MARADHI YA MLIPUKO IKIWEMO UVIKO-19

Nukuu za Katibu wa Utikadi na Uenezi CCM wakati akizungumza leo katika Uzinduzi wa Chanjo ya Uviko 19 ikulu Jijini Dar Es Salaam.


Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hii muhimu ndani ya Taifa letu. CCM inampongeza Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ibara za 83(o) na 84.


Tuliahidi CCM itaimarisha huduma za Afya kwa watanzania sambamba na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kuwakinga dhidi magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19. Alilofanya Rais Samia leo ni utayari wake na nia yake thabiti katika kuwatumikia watanzania na kuliongoza Taifa.

Uongozi ni kuonesha njia ndivyo alivyofanya Rais Samia na ndio maana viongozi na wasaidizi wake tumemuunga mkono kupata chanjo hii ya UVIKO 19 hapa ikulu. Tuwaombe wananchi waendelee kupata taarifa sahihi na wafanye uamuzi sahihi wa kupata chanjo hii. Kinga ni bora kuliko Tiba.

Alichokifanya Rais Samia ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo katika kipindi cha miaka mitano tuliahidi tutaimarisha huduma za Afya kwa watanzania sambamba na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kuwakinga dhidi magonjwa nyemelezi na mlipuko ikiwemo UVIKO-19.

Alilofanya Rais Samia leo ni utayari wake na nia yake thabiti katika kuwatumikia watanzania na kuliongoza Taifa likiwa salama. Uongozi ni kuonesha njia ndivyo alivyofanya Rais Samia na ndio maana viongozi na wasaidizi wake tumemuunga mkono kupata chanjo hii ya UVIKO 19 hapa ikulu.

Kupata chanjo ni hiyari lakini Kinga ni bora kuliko tiba.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
Ikulu Dar es Salaam
28 Julai 2021.

IMG-20210728-WA0017.jpg


IMG-20210728-WA0020.jpg


IMG-20210728-WA0018.jpg


IMG-20210728-WA0019.jpg


IMG-20210728-WA0028.jpg


IMG-20210728-WA0030.jpg


IMG-20210728-WA0031.jpg


IMG-20210728-WA0032.jpg
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,385
2,000
CCM imeendelea kulifinyanga
taifa hili KIUTULIVU....(wenye fikra wanatambua).

CCM imeendelea kuwatumikia watanzania katika nyanja mbalimbali kwa kuhakikisha wanasimika SERIKALI SIKIVU kwa wote......

Kama lilivyo jina lake,mh.Rais SSH anaendeleza kazi hiyo kwa KUONESHA NJIA.....


Huku katika vijiwe vya kahawa mada inayoongelewa ni CHANJO ..na wako wengi WANAOLEWA baada ya kutaka KUELEWA....

Tuendelee KUWAELEWESHA.......

#TujitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#SiempreCCM
#NchiKwanza
 

Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,211
2,000
Majinga haya hayawazi kuhusu mtego wa kuhitaji vaccine for the rest of our life. Tumeacha herd immunity ya asili tumekimbilia herd immunity ya chanjo UJINGA UJINGA UJINGA UJINGA
chanjo inatengeneza life long depency Rais anajua ila amekalia kujipaka wanja na kurembea rembua hovyo.

#kauli mbiu yao inajulikana ni lazima wote wachanja ili ifanye kazi na iitakuwa hivyo matoleo yote ya Corona

Hatuna bajeti ya barabara hadi tumeanzisha tozo
Swali ni je? Zitatoka wapi ela za chanjo nyingine million 29 zinazotakiwa??

Pumbavu kabisa hicho kibibi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom