Shaka Hamdu Shaka ndani ya Ngorongoro kuzindua kampeniza uchaguzi mdogo wa Mbunge

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,530
2,141
Chama Cha Mapinduzi kuzindua rasmi kampeni zake za Uchaguzi mdogo jimbo la Ngorongoro trh 26|11|2021 katika Viwanja vya Malambo kata Sale.

Kampeni hizo zitazinduliwa na Katibu wa NEC Itikadi & Uenezi "Simba wa Vita " Shaka Hamdu Shaka akiambatana na Viongozi mbalimbali pamoja Wale wa Wilaya na Mkoa.

Kampeni hizi za Uchaguzi mdogo zinafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Marehemu William Tate Ole Nasha aliyefariki kwa shinikizo la damu.

Upinzani mkali ni kati ya Chama Cha Mapinduzi CCM na Chama cha Alliance for Change & Transparency ACT-Wazalendo hii ni baada ya CHADEMA kutia mpira kwapani ikiwa ni katika kukwepa aibu ya kushindwa Uchaguzi baada ya Chama hicho kukumbwa na mdororo wa kisiasa hasa baada ya kujihusisha na Ugaidi.

 
CHADEMA kuweni wawazi shida yenu ni Ufuasi hafifu na sio Tume ya Uchaguzi kama mnavyouhadaa umma wa Watanzania,


HONGERA ACT -WAZALENDO
 
1637869036633.png
 
Hahahahaha hamjisikii raha kupigana wenyewe kwa wenyewe? (CCM v/s ACT)
Hehehe jameni chadema

Kwani Zito si mwenzenu? Au mmesahau wakati uchaguzi ulopita mliungana kuanzia bara hadi kule Zanzibar
 
Kusema ukweli ACT bado hawajatoa upinzani katika majimbo yote matatu ya bara walioshindana ikiwemo majimbo mawili ya kigoma ambako ni ngome yao. ACT Wasipoonesha positive opposition kipindi hiki ambacho CHADEMA wamejitoa, basi CHADEMA kitabakia chama kikuu Cha upinzani mpaka pale serikali itakapoingia na kuisaidia ACT ili kuiua CHADEMA. Ndio maana chaguzi ndogo zimekosa mvuto maana baba yao CHADEMA hayupo.
 
chaguzi kama hizi ni bora wao CCM wajitangaze tu wameshinda, there's no point kushiriki uchanguzi ambao,
  • Mwenyekiti wa uchaguzi anateuliwa na mwenyekiti wa chama shiriki ktk huo uchaguzi
  • Makamishina wa uchaguzi wanateuliwa na mwenyekiti wa chama shiriki ktk huo uchaguzi
  • Wasimamizi wa uchaguzi wanateuliwa na mwenyekiti wa chama shiriki ktk huo uchaguzi
  • State machinery ie polisi, mahakama etc wapo kulinda maslahi wa chama tawala na sio kuweka mazingira huru,haki na ya usawa kushiriki uchaguzi

Hakuna usawa kwenye kufanya shughuli za kisiasa kama sheria inavyotaka ie hakuna makongamano na mikutano ya kujenga, kuimarisha na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi hapa tunaona wanaoruhusiwa ni chama tawala tu maana take hivi vyama vingine havipati nafasi ya kujijenga na kutoa mawazo mbadala ili kumpa mwananchi nyezo na uwezo wa kufanya uamuzi sahihi kwenye uchaguzi.kujumla chaguzi za Tanzania ni kiini macho tu kwa muktadha wa demokrasia ya vyama vingi
 
Anzishenigogoro CCM ili na wao waone joto ya jiwe kama ilivyokuwa CUF na NCCR Mageuzi enzi zile
 
Back
Top Bottom