Shaka Hamdu Shaka: Chama cha Mapinduzi ni sikivu, kipo tayari kupokea ushauri wakati wote

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1643980213052.png

Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 45 ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema kwa kipindi chote hicho CCM kimeendelea kuwa chama sikivu na makini kinachojali majadiliano kuliko vitisho, kebehi, ubabe au kushurutishwa.

Amesisitiza CCM kipo tayari wakati wote kupokea maoni/ushauri na kutoa rai kwa Vyama vya Siasa Nchini kuendelea Umoja wa Kitaifa, kuthamini na kukuza ustawi wa demokrasia iliyopo akisema yapo Mataifa yanayoitamani Tanzania.

Amesema ndani ya Utawala wa CCM, maendeleo makubwa ya nchi yamepatikana, na yamekuwa msukumo mkubwa wa ujenzi wa amani kwa wananchi.
 
CCM muache sifa na unafiki. Kemeeni na kumshauri Rais wetu hali ya mfumuko wa bei , kukatika kwa umeme na maji.

Kwakuwa mko karibu na Rais punguzeni kusifia mkiangalia matumbo yenu, WANANCHI wanahali mbaya huku.

Pia tunawashauri "Waziri wa Nishati hafai kabisa hata kidogo, inatia kinyaa CCM ina timiza miaka 45 lakini umeme ni wa mgao inaumiza sana!!

Sukuma gang wanauliza pia vipi ile miradi ya Bwawa la umeme cranes bado tu hazijaletwa? Vipi makao makuu ya nchi kwa sasa kama hatuelewi?

Pia machinga wanamkumbusha mkuu wa mkoa wa DSM ajiuzulu kama alivyoahidi maana wanarudi kwa kasi kwenye maeneo yao baada ya kupelekwa dampo bila mafanikio!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mwambie wakurugenzi wengi sana wameiba hela za madarasa za uviko wameweka marumaru, kwenye madarasa ya zamani pamoja na madirisha ya aluminum kudanganyia .
 
Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 45 ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema kwa kipindi chote hicho CCM kimeendelea kuwa chama sikivu na makini kinachojali majadiliano kuliko vitisho, kebehi, ubabe au kushurutishwa.

Amesisitiza CCM kipo tayari wakati wote kupokea maoni/ushauri na kutoa rai kwa Vyama vya Siasa Nchini kuendelea Umoja wa Kitaifa, kuthamini na kukuza ustawi wa demokrasia iliyopo akisema yapo Mataifa yanayoitamani Tanzania.

Amesema ndani ya Utawala wa CCM, maendeleo makubwa ya nchi yamepatikana, na yamekuwa msukumo mkubwa wa ujenzi wa amani kwa wananchi.
Huyu jamaa ni mtu Mzalendo sana, Shaka tuko na wewe wakati wote
 
Back
Top Bottom