Shaka: Falsafa ya Uchumi kuongoza Uchumi yathibitishwa TANZANIA ndani ya siku 558 za Rais Samia

World light

JF-Expert Member
Aug 4, 2022
275
258
IMG-20221010-WA0059.jpg

SIKU 558 ZA SAMIA MADARAKANI MISINGI YA FALSAFA ZA UCHUMI KUONGOZA UCHUMI ZAFANIKIWA- MWENEZI SHAKA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema ndani ya siku 558 tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa Tanzania, amefanikiwa kutekeleza falsafa ya uchumi kuongozwa kwa misingi ya kiuchumi..
IMG-20221010-WA0056.jpg

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani alipotembelea Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani amesema misingi hiyo ni pamoja na kuvutia wawekezaji, ushirikishaji sekta binafsi na kutumia diplomasia badala ya mabavu katika kufungua uchumi.
IMG-20221010-WA0057.jpg

"Leo ni takribani siku 558 tangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa nchi yetu, ambapo baada ya kiapo alitoa mwelekeo wa serikali atakayoiunda na kuiongoza kuwa, nia yake ni kuifungua nchi kiuchumi.

"Sote ni mashuhuda tumeanza kushuhudia akiruhusu misingi ya falsafa za uchumi kuongoza uchumi badala ya nguvu za kiutawala. Tumeshuhudia Rais Samia akitumia taaluma yake ya uchumi na uzoefu wake wa kiuongozi na masuala ya kidiplomasia akibadili kabisa mazingira na kasi ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo," amesema.

Shaka amesema ndani ya kipindi hicho kupitia diplomasia ya uchumi Rais Samia amefanikiwa kutafuta na kuvutia wawekezaji, kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza shughuli za uzalishaji zitakazoongeza ajira na mapato ya serikali.

Aidha, amesema ameimarisha mazingira ya bishara na uwekezaji kwa kuondoa urasimu, ukusanyaji kodi wa mabavu, kufanya maboresho ya sheria na mifumo mbalimbali kwa lengo la kuondoa kero kwa wafanyabiashara na wawekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ibara 22, 46 na 49.

Akiwa katika maonyesho hayo, Shaka ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki maonesho hayo yakiwamo ya taasisi za umma, binafsi na wajasiriamali.
 
Nasema kama kuna mtu hata pata pesa wakati huu wa Rais Samia nasema kamwe hatokuja kupata mpaka anakufa
 
Mandonga nakuunga mkono,
Kwa sasa TANZANIA watu wanakula bia Ni balaa, baa zote zimejaa, watu wanatumia pesa, Samia ameirudisha enzi ya Kikwete Kiana
 
Wengine wanalalamika bei za vyakula kupanda, huku wengine wanashinda baaa!!! Hiii kweli bongoland
 
View attachment 2382709
SIKU 558 ZA SAMIA MADARAKANI MISINGI YA FALSAFA ZA UCHUMI KUONGOZA UCHUMI ZAFANIKIWA- MWENEZI SHAKA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema ndani ya siku 558 tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa Tanzania, amefanikiwa kutekeleza falsafa ya uchumi kuongozwa kwa misingi ya kiuchumi..
View attachment 2382796
Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 9, 2022, Kibaha mkoani Pwani alipotembelea Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani amesema misingi hiyo ni pamoja na kuvutia wawekezaji, ushirikishaji sekta binafsi na kutumia diplomasia badala ya mabavu katika kufungua uchumi.
View attachment 2382798
"Leo ni takribani siku 558 tangu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa nchi yetu, ambapo baada ya kiapo alitoa mwelekeo wa serikali atakayoiunda na kuiongoza kuwa, nia yake ni kuifungua nchi kiuchumi.

"Sote ni mashuhuda tumeanza kushuhudia akiruhusu misingi ya falsafa za uchumi kuongoza uchumi badala ya nguvu za kiutawala. Tumeshuhudia Rais Samia akitumia taaluma yake ya uchumi na uzoefu wake wa kiuongozi na masuala ya kidiplomasia akibadili kabisa mazingira na kasi ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo," amesema.

Shaka amesema ndani ya kipindi hicho kupitia diplomasia ya uchumi Rais Samia amefanikiwa kutafuta na kuvutia wawekezaji, kuimarisha mazingira ya biashara na kuongeza shughuli za uzalishaji zitakazoongeza ajira na mapato ya serikali.

Aidha, amesema ameimarisha mazingira ya bishara na uwekezaji kwa kuondoa urasimu, ukusanyaji kodi wa mabavu, kufanya maboresho ya sheria na mifumo mbalimbali kwa lengo la kuondoa kero kwa wafanyabiashara na wawekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ibara 22, 46 na 49.

Akiwa katika maonyesho hayo, Shaka ambaye aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki maonesho hayo yakiwamo ya taasisi za umma, binafsi na wajasiriamali.
Kitaa pesa ipo tufanye kazi kwa bidii
Bei ikiwa juu na pesa ikawepo kuna shida?
 
Back
Top Bottom