Shaka: CCM tutalinda Dola tuliyonayo kwa kuchapa kazi

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanya vizuri sana katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais mwaka 2020. Kati ya maeneo hayo ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro.

Hali hiyo imemfanya katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka kuwapongeza viongozi na wanachama na viongozi wa CCM mkoani humo. Hata hivyo Shaka amesema ushindi huo wa CCM ni deni kubwa kwa watanzania ili ijiwekee mazingira mazuri huko mbeleni ili kulinda dola waliyopewa.

"Tunayo kazi kubwa ya kulinda ushindi wetu na dola tuliyonayo. Hatutailinda dola waliyotupa wananchi kwa bunduki wala mapanga bali kwa kuitekeleza ilani yetu ya uchaguzi kwa ukamilifu, kuendelea kuwa karibu na wananchi kwa kuwasikiliza na kuwaondolea kero ili kuimarisha huduma na kuharakisha maendeleo yao." Amesema Shaka

Katika hatua nyingine Shaka amesema kumekuwa na upotoshaji kuwa usafiri wa treni kutoka Dar - Tanga - Moshi - Arusha umesitishwa sio kweli kwani CCM kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ibara ya 59(d) iliahidi kuendelea kuimarisha na kuboresha usafiri wa reli kote nchini.

"Ameitaka serikali kuharakisha ukarabati wa reli kipande cha Ruvu junction-Korogwe ili huduma ya usafiri wa reli kutoka Dar - Tanga - Moshi - Arusha irejee kwa uhakika, usalama na ufanisi ili kwa ustawi wa wananchi kiuchumi kama Rais Samia Suluhu Hassan anavyotaka." Alisisitiza Shaka

Shaka alihitimisha kwa kuwataka wana-CCM kote nchini kuwa mstari wa mbele kuyasemea mafanikio na yote mazuri yanayofanywa na serikali zetu zote mbili ambapo itasaidia kukabiliana na upotoshaji.


#CCMImara
#KaziIendelee
IMG-20220426-WA0063.jpg
IMG-20220426-WA0055.jpg
IMG-20220426-WA0058.jpg
IMG-20220426-WA0057.jpg
IMG-20220426-WA0038.jpg
IMG-20220426-WA0054.jpg
 
Back
Top Bottom