Shaka: CCM na Serikali yake inathamini mchango wa wanawake

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu

Taifa lolote lisilothamini mchango wa wanawake ni butu, dhana ya usawa wa kijinsia ni kichocheo cha ushiriki na ushirikishwaji katika maendeleo endelevu ya kila Taifa linalothimini na kujali mchango wa kina mama.

Baba wa Familia ya watanzania Rais John Pombe Joseph Magufuli alisema asubuhi ya leo 8 Machi 2019 kuwa serikali anayoiyongoza inathamini kazi nzuri inayofanywa na akina mama, amewataka muendelee kutembea kifua mbele.

Nasi wasaidizi wake katika Chama cha Mapinduzi tunamuunga mkono kwenye hilo ninawahakikishia tutawapa kila aina ushirikiano, msaada na tutawashika mkono wanawake wa Morogoro na watanzania kwa ujumla ili muweze kufikia ndoto zenu maana hata ilani ya CCM 2015-2020 imetuelekeza kusimamia na kuendeleza harakati za maendeleo ya wanawake kiuchumi, kijamii na kiasiaza nchini.

#WanawakeJeshiKubwa
IMG-20190308-WA0047.jpeg
IMG-20190308-WA0046.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom