Shaka: CCM haitadumaza Mahusiano ya Kimataifa

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu,
Dar Es Salaam.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuhudhuria kwa maafisa wa kibalozi ,mashirika ya haki za binadamu na Umoja wa Ulaya (EU) zinaweza kuifuatilia kesi yeyote mahakamani ili kujua iwapo mahakama zinatenda haki kwa mujibu wa sheria huku wakiwa hawana haki ya kuingilia uhuru wa mahakama.

Kimesema Tanzania ni Taifa lenye sifa kemkem kutokana na kufuata kwake misingi ya utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na kuenzi utii wa matakwa ya katiba na sheria.

Hayo yameelezwa jana na Katibu wa itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipoulizwa iwapo anajua lolote huhusu maafisa wa ubalozi wa marekani na Uhamiaji wa ulaya walivyoanza kufuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe mahakamani.

Shaka alisema kwa upande wake hana taarifa za shitaka hilo kufikishwa mahakamani na asingependa kulizumgumzia kwani halijui na hajui chochote hivyo akasema yuko tayari kuzungumzia hatua ya maafisa wa kibalozi kuhudhuria mahakamani.

Alisema maafisa hao wana wajibu wa kufuatilia suala lolote mahakamani baada ya kupewa kibali toka wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa aidha wanapotaka kutazama maendeleo ya miradi ya ushirikiano na ya kisekta kama mkakati wa kudumisha mahusiano ya kimataifa.

"Maafisa wa kibalozi wa jumuiya nyingine yakiwemo mashirika ya haki za binadamu na utawala bora toka popote yanaweza kufika mahakamani hakuna cha ajabu. Tanzania nchi mashuhuri kwa sifa ya kuenzi haki za binadamu.

Hivyo uamuzi wao kwenda mahakamani pengine ni kutaka kupata kipimo cha uhuru katika uendeshaji wa kesi mbalimbali katika mahakama zetu"Alisema Shaka.

Aidha alisema Mataifa rafiki kwao yanayoheshimu haki za binadamu, utawala wa sheria, yanayothamini uhuru wa kujieleza, wa maoni na yanayotoa nafasi ya uhuru wa habari hayatapata kitete hadi kuwazuia maafisa wa kibalozi au wa jumuiya za kimataifa zisihudhurie mahakamani.

'Nadhani wana nia ya kusikiliza uendeshaji kesi, utoaji haki na pale mahakama zinapowatia hatiani watuhumiwa na washitakiwa. Nijuavyo mahakama hazifungi watuhumiwa bila kupatikana ushahidi yakinifu. Mahakama ziko huru kwa mujibu wa matakwa ya sheria. Kwa Tanzania hii inaeleweka"Alisisitiza.

Shaka alisema kuwepo kwa maafisa hao au kutokuwepo kwao bado wana uwezo wa kupata taarifa sahihi kupitia vyombo mbalimbali na huo huwa ni mpango wa utakaoionesha dunia kama mahakama za Tanzania ziko na uwazi, zinajiamini kiutendaji na ukweli ikiwemo uhuru wa kisheria bila kuvuka mipaka au kuleta mgongano katika mgawanyo wa madaraka.

Amani, umoja na utulivu tunaojivunia leo na kupigiwa mfano kama kisiwa cha amani ulimwenguni ni pamoja na utoaji haki kwa usawa
unakofanywa na mahakama zetu.

Katibu huyo alisema Tanzania imekuwa ikiwakaribisha hata watazamaji toka mataifa ya nje ili kuja kufuatilia na kutazama uendeshwaji wa michakato ya chaguzi zake kuu toka hatua ya uandikishaji wapiga kura,hatua za uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo hivyo hili la wao kufuatilia kesi mahakamani sio jambo la ajabu.

"Maafisa wanaohudhuria mahakamani husikiliza iwapo mienendo ya kesi kama inafuata taratibu za kisheria. Hawaendi mahakamani. Mambo yote huendeshwa kwa mujibu wa sheria za taifa husika. Hutasikia wakisema hili ni shitaka halisi au ni maonevu. Wapo ili kudumisha mahusiano ya kidipomasia jambo ambalo kama Chama tunapenda kuona yakiimarika zaidi huku uhuru wetu kama Nchi ukiheshimika. "Aleleza Shaka.

Mwisho.

IMG-20210808-WA0057.jpg
 
Wakati mwingine ni ngumu sana kujua kama tuna viongozi sahihi wa kuongoza watu milioni 60. Wapo wazuri na wapo ambao hata hauwezi fahamu walifikaje hapo juu walipo.
 
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uwezo wa viongozi na makada wa chama hicho unatokana na utayari, uthubutu na kuujua umma unataka nini, kwa wakati upi na namna ya kutimiza mahitaji husika kulingana na changamoto zinazowakabili wananchi.

Pia kimesema chama cha siasa ambacho hakiwezi kuheshimu matakwa ya wanachama, wananchi na Taifa hutanguliza maslahi binafsi ya viongozi kuliko maslahi mapana ya umma kama wafanyavyo upinzani na hapo ndipo penye tofauti kati yao na chama tawala.

Hayo yamesemwa jana na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alipoulizwa iwapo CCM ina utofauti na upinzani alisema kuna utofauti kati ya viongozi wake na upinzani vivyo hivyo katika ubora wa muundo na sera CCM huwezi kukifananisha na chama chochote nchini.

Shaka alisema kwanza vyama upinzani hivyo ukiacha kuwa ni vichanga, havijawa na uzoefu wa kutosha, viongozi wake wamepatikana nje ya mifumo yenye kuaminika kwa jamii ikiwemo kutokimbazana na mahitaji ya wakati.

Alisema mfano chadema iwapo kingelikuwa kinafanya tathmini au tafiti za kisiasa toka kwa wanachama wake na makundi mengine ndani ya umma kutaka kufahamu ajenda ipi ni kipaumbele kwa wakati huu kati ya uchuni na katiba mpya, basi takwimu zingewaonesha kipaumbele namba moja ni uchumi.

Katika hili tunawakumbusha wakafanye rejea kwenye utafiti wa TWAWEZA sauti za wananchi ambao ulionesha vipaumbele vya wananchi na katika hivyo katiba haikuwepo, wananchi walitaja maji, afya, elimu, rushwa, miundombinu na uchumi.

Alisema kutokana na chama hicho (Chadema) kushindwa kufanya tafiti za msingi zenye kwenda sanjari na mahitaji ya wakati, ndiyo maana kila wakati kimekuwa kikijikuta kikishindana na nguvu za upepo kwa mujibu wa wakati ndio maana hakijui kama uchumi wa watu ni kipaumbele cha kwanza na vingine hufuata baadaye.

"Chama bora na makini hujikita katika tafiti za kitaalamu kila mara ili kuweza kufahamu mahitaji ya wananchi na Taifa pamoja na namna nzuri ya kuyakamilisha. Matakwa na mahitaji ya wakati yanapopishana na kuanza kuchomoza ukaidi wa viongozi ni dosari na kiashiria kuwa chama husika kimepoteza ushawishi wake na kipo hatarini kuingia makumbusho ya kisiasa. Nguvu ya ushawishi sio uwezo wa kupaza sauti bali ni uwezo wa kuyaishi mahitaji ya wakati kwa njia sahihi." Alisema shaka.

Alisema kila madhumuni, shabaha, sera na malengo yenu kadri mnapoitazama jamii hapo ndipo mnapotakiwa kusimama pamoja kama viongozi huku mkiwa mmejitayarisha, mnajiamini na kujitegemea kifikra katika msimamo mmoja wenye manufaa ya wengi.

Aidha katibu mwenezi huyo alisema viongozi wasiojiamini kamwe hawawezi kuendeleza malengo yao ya msingi. Maana hawana moyo wa uvumilivu na subira hivyo ni vigumu sana kumudu migogoro ndani ya vyama wanavyoviongoza. Vyama vya upinzani vina viongozi wa aina hii wasiojiamini ndio sababu migogoro haikomi na vinadumaa.

"Sifa ya CCM ni bidii, utayari, umoja wake madhubuti, subira na ustahimilivu. Hayupo anayeweza kutenda na kutekeleza mawazo au fikra zake bila kupatikana uamuzi na msimamo wa pamoja. Hivyo vikao ni muhimu sana kuliko uwezo binafsi wa mtu. Siku zote CCM huamua mambo yake kwa kutazama mahitaji ya wengi kupitia vikao" Alisema

Shaka alisema aina ya viongozi wenye kuelewa hayo na kuyasimamia huwezi kuwakuta kwenye vyama vingine badala yake huko jamii itakutana na wapigania madaraka, wapenda vyeo na utawala na wala hutawaona viongozi au wanasiasa makini.

"Yapo mataifa yenye katiba zinazoitwa katiba bora. Cha ajabu mataifa hayo yapo kwenye ukabila, milio ya risasi, mapigano na umwagaji damu wao kwa wao. Yote ni kwa sababu wanasiasa wanapambana kusaka vyeo na kutafuta urahisi wa kupata madaraka ya kiutawala. Tanzania imepata gharama kubwa kujenga misingi ya amani, umoja, mshikamano iliyonayo leo ikiwa imewekewa misingi thabiti kwenye katiba. Kwa sasa tushirikiane na tushikamane vizuri kujenga uchumi kwanza." Alisisitiza shaka

Mwisho
IMG-20210808-WA0056.jpg
IMG-20210808-WA0052.jpg
IMG_20210808_162227_913.jpg
 
2020 Mliwanyima kibali waangalizi wa nje katika uchaguzi
 
Shaka alisema kwa upande wake hana taarifa za shitaka hilo kufikishwa mahakamani na asingependa kulizumgumzia kwani halijui na hajui chochote hivyo akasema yuko tayari kuzungumzia hatua ya maafisa wa kibalozi kuhudhuria mahakamani.

Sisi tunajua kwa maneno haya, tayari uwoga umetamalaki ndani ya CCM na serikali yake ya awamu ya sita.

Kuna mtanzania gani asiyefahamu kesi hii ya ugaidi iliyopo mahakamani na pia mwenendo wake wa kutajwa na kuhairishwa!?
 
Back
Top Bottom