Shaka ateta na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,862
930
SHAKA HAMDU SHAKA ATETA NA NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU.

Leo Ijumaa 23 Julai 2021 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga Ofisini kwake Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Pamoja na Mambo Mengine Shaka amemsisitiza Naibu Waziri kuzingatia kundi hili analolisimamia kuhakikisha linafatiliwa na kupata haki staki na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Samia Suluhu Hassan, pamoja na kukomesha vitendo vyote vya unyanyasaji ambayo vinawakumba walemavu.

Aidha, Mheshimiwa Ummy amewakikishia Ndugu Shaka kutoa ushirikiano kwa Chama Cha Mapinduzi Muda wowote inapoitajika.

#Kazi iendelee
#Chama Imara

IMG-20210723-WA0142.jpg

IMG-20210723-WA0143.jpg
 
Back
Top Bottom