Shaka asema kazi ya kuleta maendeleo hapewi kila mtu

AFRIKAMOJA

Member
Aug 11, 2022
30
37
~Kishindo cha Shaka uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Amani

~Asema ni CCM ndiyo yenye uwezo wa kuleta maendeleo ya nchi

~Asisitiza kazi nzuri inayofanywa na Rais Mwinyi inaonekana

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wananchi katika Jimbo laAmani kumchagua mgombea wa wake kwa kuwa ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Imesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husein Ali Mwinyi anafanya kazi kubwa na nzuri, hivyo anastahili kupewa viongozi watokanao na CCM ili kuiendeleza kasi hiyo.

Aidha, amesema kazi ya kuleta maendeleo hususani katika jimbo hilo haiwezi kuletwa na kila mtu, hivyo kuna kuna umuhimu mkubwa wa kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM ambaye anao uwezo wa kuifanya kwa ufanisi.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Amani, Zanzibar wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Abdul Yussuf Maalim.

"Kazi ya kuleta maendeleo ya nchi hii hapewi kila mtu, kazi ya kuleta maendeleo Jimbo la Amani sio kila mmoja anaiweza, wapo wenye uwezo wa kuleta propaganda kwenye jimo la Amani, lakini wapo wenye uwezo wa kuleta maendeleo na Wana amani mkasema kweli haya ni maendeleo ambayo tunayahitajia, ndiyo maana tukasema Abdul songa mbele nenda ukapeperushe bendera ya Chama Cha Mapinduzi sababu tulijua anaimudu kazi hiyo.

Ushindi wa CCM katika Jimbo la Amani ni kama kufa na kupona, tutashinda kwa haki, tutashinda kwa amani, lakini tutashinda tukiwa wamoja na tumeshikamana," alisema.

Alisema kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili ni kubwa hivyo anastahili kupongezwa na kuungwa mkono ikiwamo kumchagulia wagonbea watokanao na CCM ili kushirikiana naye.

"Ndani ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Dk. Mwinyi mtu apende asipende, afurahi asifurahi Dk. Mwinyi amefanya vizuri kuleta maendeleo. Mabadiliko tunayoyashuhudia Zanzibar...lazima tukubali matarajio ya wazanzibari kwa Dk. Mwinyi ni makubwa zaidi," alisema.

Kwa upande wake mgombea huyo, alisema iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo amejipanga kuendeleza kasi ya maendeleo kwa kushirikiana na Rais Dk. Husein Ali Mwinyi na viongozi wengine wa Chama, serikali na wananchi kwa ujumla.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Disemba 17, mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Maalim Mussa.


IMG-20221201-WA0073.jpg
IMG-20221201-WA0071.jpg
IMG-20221201-WA0070.jpg
IMG-20221201-WA0060.jpg
IMG-20221201-WA0067.jpg
IMG-20221201-WA0062.jpg
IMG-20221201-WA0061.jpg
IMG-20221201-WA0059.jpg
IMG-20221201-WA0065.jpg
IMG-20221201-WA0091.jpg
IMG-20221201-WA0094.jpg
IMG-20221201-WA0090.jpg
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
37,641
55,022
Aidha, amesema kazi ya kuleta maendeleo hususani katika jimbo hilo haiwezi kuletwa na kila mtu, hivyo kuna kuna umuhimu mkubwa wa kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM ambaye anao uwezo wa kuifanya kwa ufanisi.
Shaka kaa ukijua hizo fedha ni za Walipakodi wa Nchii hii, huzitoi CCM wala mfukoni kwako, kwa hiyo hata sisi Wapinzani tukipata ridhaa ya Wananchi kihalali tunaweza kuleta Maendeleo kuliko ninyi.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom