Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam...
Hongera sana Shaka, tunakuamini sana
 
Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam.

=====

CCM yapiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia mjini

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeagiza marufuku ya waendesha bodaboda na bajaji kutofika au kufanya shughuli zao katikati jiji la Dar isitishwe mara moja kwa kuwa si muafaka lakini pia imetolewa kwa kukurupuka.

Kauli hiyo ya CCM imekuja siku moja baada ya Kamishana Msaidizi wa Polisi, Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Abdi Issango kunukuliwa akipiga marufuku bodaboda na bajaji wote kuingia mjini na wale walioko mjini watoke isipokuwa bajaji za walemavu. Marufuku hiyo ilikuwa ianze kutekelezwa rasmi tarehe 1 Novemba mwaka huu.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 31 Oktoba, 2021, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema marufuku hiyo ilitolewa bila kuzingatia taratibu za msingi zinazopaswa kufanya uamuzi unaogusa masilahi ya wananchi.

Amesema jambo hilo limeleta taharuki na CCM imepokea kwa mshangao mkubwa kwani ni jambo ambalo halikuwa na matayarisho mithili ya watu kukurupuka katika kutoa maamuzi hayo.

“CCM kimepokea na kufuatilia malalamiko ya wananchi mbalimbali ikiwamo, machinga, waendesha bodaboda, sanjari na malalamiko hayo, CCM kinaungana na Rais Samia katika dhamira yake ya kuona nchi yetu inapangwa vizuri na kuwa kivutio kwa kuwapanga vema machinga na wafanyabiashara wengine.

“Tuliona sasa Rais amewajali na kuwathamini kwa kutoa maelekezo kwamba watoa huduma hizo wapangwe katika maeneo rafiki,” amesema.

Amesema Chama kimeagiza Mamlaka za kiserikali mkoa wa Dar es Salaam zinazohusisha viongozi na watendaji, vyombo vya dola na mamlaka zingine zenye majukumu ya kusimamia usafiri na usafirishaji maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam chini ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta hiyo, zikutane kwa haraka iwezekanavyo.

“Lengo ni kuangalia iwapo kuna changamoto zozote zilizojitokeza ili zijadiliwe na kupata ufumbuzi wa muda mfupi, wa kati na mrefu ama ufumbuzi wa kudumu ili kutoathiri na kubughudhi ustawi wa shughuli za makundi ya watu wanaohusika.

“Chama kinasisitiza kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, kitafuatilia na kuhakikisha

utekelezaji huu unafanyika kwa mafanikio makubwa,” amesema.

Pia soma:

Thread 'Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini' Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini

View attachment 1994026
Huyu bwana anawapa shida sana CHADEMA TZ,
 
Mojawapo ya makosa makubwa sana katika muundo wa CCM na katiba yetu ni kule kuruhusu Chama cha siasa kufanya mambo ya kiserikali. Hata madai ya kuwa "tunatekeleza ilani ya CCM ni makosa" sana.

Kinachotakiwa ni kuwa baada ya Uchaguzi, ilani hiyo ipelekwe Bungeni ipitishwe kama blue print ya serikali, siyo document ya kampeini ya chama cha siasa iwe inatumika katika maamuzi ya serikali.
 
Back
Top Bottom