Shaka Hamdu Shaka aisifu mahakama ya Tanzania kesi ya Freeman Mbowe

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,450
799
Katibu wa NEC Itikadi & Uenezi CCM-Taifa Mhe Shaka Hamdu Shaka aisifu Mahakama kesi ya Freeman Mbowe, asisitiza Serikali ya Rais Samia ni ya kidemokrasia na inajali Uhuru wa Mahakama

"Hakuna kama Samia"


"Nimeona vibwagizo vya wenzetu huko mitandaoni kuwa wameruhusiwa kuingia mahakamani na simu pamoja na kufuatilia kesi ya kiongozi wao leo.

Niwaambie huo ndio Uhuru wa Mahakama na ndio Utawala wa Sheria kama msingi wa Demokrasia ya kweli chini ya utawala wa CCM na serikali makini inayoongozwa na Rais hodari, jasiri na mwenye uthubutu Mhe Samia Suluhu Hassan.

Katika nchi za kidekta haya tunayoyaona leo Mahakama za Tanzania huko hayapo " alisisitiza Shaka

IMG-20210916-WA0046.jpg

Shaka Hamdu Shaka

Katibu wa NEC Itikadi & Uenezi
Ziara Katibu Mkuu CCM

16 Septemba, 2021 Lindi.
 
Ndani ya Uongozi wa Rais Samia,
Mahakama huru,
Bunge huru,
NGOs huru
Media huru

#TanzaniakwaniSisitunatakaje?
 
Kwani Askari waliozuia watu wasiingie kwenye ukumbi wa mahakama walikuwa chini ya utawala wa Chama gani, na chini ya Rais gani?

Na kama CCM ni chama kinachofuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, Shaka atuambie Askari waliozuia watu kuingia ukumbini walitumia sheria gani kufanya hivyo, na kama walitumia sheria kwa nini maamzi yao yalitenguliwa na mahakama?

Na kama jeshi la Polisi halikufuata sheria je Shaka haoni aibu kuzungumzia demokrasia ambayo haipo ndani ya jeshi, na mahakama ilitoa uamzi baada ya watu kulalamika?

Shaka atuambie ikiwa mahakama ilitenda haki kuwaruhusu watu kuingia kwenye ukumbi wa mahakama, ni hatua gani ya Chama na serikali yake inawachukulia hao polisi waliovunja sheria?

Vinginevyo shaka tutamtilia shaka kwa uwezo wake wa kufikiri.
 
Siku hizi hata haki ya msingi ya raia bado kuna wajinga wengine wanaona kuwa ni hisani, kuna siku hawa wajinga watakuja kuisifia serikali kwa "kuruhusu uhuru wa watu kusafiri". Bure kabisa.
 
"Nimeona vibwagizo vya wenzetu huko mitandaoni kuwa wameruhusiwa kuingia mahakamani na simu pamoja na kufuatilia kesi ya kiongozi wao leo.

Niwaambie huo ndio Uhuru wa Mahakama na ndio Utawala wa Sheria kama msingi wa Demokrasia ya kweli chini
Sifa kuu ya kuwa mwana ccm hasa kiongozi ni kukosa haya na kujitoa fahamu. Pole shaka. Yana mwisho. Hata jiwe na rais wa chuma kweri kweri yalipita. Hamjifunzi tu?
 
"Nimeona vibwagizo vya wenzetu huko mitandaoni kuwa wameruhusiwa kuingia mahakamani na simu pamoja na kufuatilia kesi ya kiongozi wao leo.

16 Septemba, 2021 Lindi.
Hawa watoto sometimes akili yao huwa siwaelewi .... sasa na hao police waliokuwa wanzuia wao wako chini ya nani??

Actually, hao police waliokuwa wanazuia watu wao ndiyo wao directly chini ya Maza kuliko Muhimili uliochomekwa!!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom