Shaka aisifu Mahakama kesi ya Freeman Mbowe, asisitiza Serikali ya Rais Samia kuzingatia Demokrasia na Uhuru wa Mahakama

Mtoto wa Samia

JF-Expert Member
May 27, 2020
296
250

Shaka aisifu Mahakama kesi ya Freeman Mbowe, asisitiza Serikali ya Rais Samia kuzingatia Demokrasia na Uhuru wa Mahakama​

==================================
"Nimeona vibwagizo vya wenzetu huko mitandaoni kuwa wameruhusiwa kuingia mahakamani na simu pamoja na kufuatilia kesi ya kiongozi wao leo.

Niwaambie huo ndio Uhuru wa Mahakama na ndio Utawala wa Sheria kama msingi wa Demokrasia ya kweli chini ya utawala wa CCM na serikali makini inayoongozwa na Rais hodari, jasiri na mwenye uthubutu Mhe Samia Suluhu Hassan.

Katika nchi za kidekta tunayo yaona leo Tanzania huko hayapo " alisisitiza Shaka

IMG-20210916-WA0046.jpg


Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Ziara Katibu Mkuu CCM
16 Septemba, 2021 Lindi.
 

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
1,529
2,000
Ndani ya Uongozi wa Rais Samia,
Mahakama huru,
Bunge huru,
NGOs huru
Media huru

#TanzaniakwaniSisitunatakaje?
 

Ss Jr

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
528
500
Kwani Askari waliozuia watu wasiingie kwenye ukumbi wa mahakama walikuwa chini ya utawala wa Chama gani, na chini ya Rais gani?

Na kama CCM ni chama kinachofuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, Shaka atuambie Askari waliozuia watu kuingia ukumbini walitumia sheria gani kufanya hivyo, na kama walitumia sheria kwa nini maamzi yao yalitenguliwa na mahakama?

Na kama jeshi la Polisi halikufuata sheria je Shaka haoni aibu kuzungumzia demokrasia ambayo haipo ndani ya jeshi, na mahakama ilitoa uamzi baada ya watu kulalamika?

Shaka atuambie ikiwa mahakama ilitenda haki kuwaruhusu watu kuingia kwenye ukumbi wa mahakama, ni hatua gani ya Chama na serikali yake inawachukulia hao polisi waliovunja sheria?

Vinginevyo shaka tutamtilia shaka kwa uwezo wake wa kufikiri.
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,152
2,000
Siku hizi hata haki ya msingi ya raia bado kuna wajinga wengine wanaona kuwa ni hisani, kuna siku hawa wajinga watakuja kuisifia serikali kwa "kuruhusu uhuru wa watu kusafiri". Bure kabisa.
 

MASHANJARA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
244
500
"Nimeona vibwagizo vya wenzetu huko mitandaoni kuwa wameruhusiwa kuingia mahakamani na simu pamoja na kufuatilia kesi ya kiongozi wao leo.

Niwaambie huo ndio Uhuru wa Mahakama na ndio Utawala wa Sheria kama msingi wa Demokrasia ya kweli chini
Sifa kuu ya kuwa mwana ccm hasa kiongozi ni kukosa haya na kujitoa fahamu. Pole shaka. Yana mwisho. Hata jiwe na rais wa chuma kweri kweri yalipita. Hamjifunzi tu?
 

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,380
2,000
"Nimeona vibwagizo vya wenzetu huko mitandaoni kuwa wameruhusiwa kuingia mahakamani na simu pamoja na kufuatilia kesi ya kiongozi wao leo.

16 Septemba, 2021 Lindi.
Hawa watoto sometimes akili yao huwa siwaelewi .... sasa na hao police waliokuwa wanzuia wao wako chini ya nani??

Actually, hao police waliokuwa wanazuia watu wao ndiyo wao directly chini ya Maza kuliko Muhimili uliochomekwa!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom