Shajara inarejesha kumbukumbu na mengi uliyosahau

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
SHAJARA INAREJESHA KUMBUKUMBU NA MENGI ULIYOSAHAU

Natamani nikuwekeeni yale mazito niyoandika katika shajara zangu lakini natia natoa maana sheria ya mtandaoni imekuwa kali kidogo.

Mengi katika niliyohifadhi katika shajara zangu zinahusu Zanzibar.

Unapoandika katika shajara uko faragha unajitanua upendavyo maana unazungumza na nafsi yako...niliwaonesha wachapaji vitabu shajara zangu wananitia hima niwaandikie kitabu kuhusu Zanzibar na matatizo ya uchaguzi.

Nawaambia haya siwezi kuyasema hadharani maana ithibati yake ni mie nipate upande wa pili na kwao huu ni muhali mkubwa.

Wachapaji wao wanaangalia mauzo ya kitabu...si rahisi leo viongozi wetu kukubali baadhi ya nema zilizopotea na ukweli uliofichwa.

Ukisoma huo ukurasa wa shajara yangu utaona nimeandika:

''Election results are not coming out as they should... CUF is leading by 11 seats...rang up Mzee Rashad in Dar es Salaam...make copies of Ali Nabwa's 1973 prison letters from DRUM.''

Hapo juu kuna majina matatu - Ahmed Rashad Ali na Ali Nabwa.
Nkisema niwaeleze hawa wote hapa makala itakuwa ndefu sana.

Hawa wanahitaji makala yao maalum na nina hakika msomaji wangu utajifunza mengi.

Ukipenda unaweza kutembelea hapo chini:


(Nimeshindwa kuweka link ya Ali Nabwa ambayo ni taazia yangu niliyomwandika baada ya kifo chake iliyochapwa na The East African kwa kuwa ''wajanja'' wameingia na kuweka picha za matusi).

Nimeanza kuwa na diary toka mwaka wa 1968.

Huwa siwezi kumaliza hata kurasa mbili nikifungua kuzisoma naifunga.

Nawaona rafiki zangu wote ''vividly,'' tuko darasani au katika ''jam session,'' na nasikia ala na sauti zetu tukiimba hizi zilikuwa enzi za Motown au tuko Mnazi Mmoja tunacheza mpira tukiachiana pasi mbele na nyuma with ''precision,'' sote tumevaa Gola, Puma au Addidas.

Chaguo lako.

Gola ndiyo kiiikuwa kiatu kisichokuwa na thamani bei rahisi sana.

Na tulikuwa na coach.

Katika hawa na viwanja hivi walitoka baadhi yetu wakawa wachezaji mpira maarufu na wakavaa rangi za Tanzania katika miaka ya mwanzoni 1970s

Moyo wangu huvuja damu leo nikiona watoto wanacheza mpira barabarani katika mitaa pekupeku na mpira ni wa makaratasi.

Wenzangu wengi wametangulia mbele ya haki wengine niliokuwanao katika mpira na wengi katika ''afternoon jam sessions.''

Katika utoto wetu katika miaka ya 1960 tuliileta Motown, Apollo Theatre na Broadway Dar es Salaam.

Kulikuwa anakuja bint nyumbani kwangu anamfuta mwanangu wa kiume mara kwa mara jioni.

Wote wakisoma pamoja shule ya msingi.

Siku hiyo nikamuuliza mtoto wangu mbona huyu anakuja kukufata hapa kika siku?

''Baba huyu tunacheza mpira timu moja.''
Timu yenu mnacheza na wasichana?"

''Tena huyu ni hodari tunampanga hadi mechi.''

Kinywa changu kimekauka mate.

''Yaani timu yenu ina wasichana na mnachezanao mpira?''

Mwanangu kashangaa kuona mimi nashangaa yeye kuwa timu moja ya mpira na wasichana.

Kila mtu kamshangaa mwenzake.

PICHA: Picha ya kwanza ni ukurasa mmoja kutoka shajara yangu ya mwaka wa 1995 wakati wa uchaguzi Zanzibar na picha ya pili mkono wa kushoto katika shubaka la vitabu ni baadhi ya shajara zangu.

Picha ya tatu hapo ni Apollo Theatre, Harlem New York chimbuko la wanamuziki mashuhuri wa Motown.

Screenshot_20220301-074455_Facebook.jpg
 
Nitangulize samahani mzee wangu.
Jamiiforums ni zaidi ya tuijuavyo. FaizaFoxy ni mtani wangu, rafiki na mtu wangu wa karibu. Kwa mantiki hiyo, hapo juu nilikua namtania.
Natumai uliipata ile yangu ya Qariah Kuu (Kariakoo).

Halafu pole sana kwetu sote kwa kuondokewa na Wendo. Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.
Faiza...
Tushapoa Maalim wangu.
 
Kolola,
Ikiwa umekusudia mimi nimsaidie Maalim Faiza nataka nikufahaishe kuwa Faiza haitaji msaada wa yoyote katika ukumbi huu.

''Intellect'' ya Faiza ni wachache sana hapa wanaweza hata kuikaribia.
Sitanii.

Above average.

Pitia post zake hapa zisome hili utaliona.
Pia ana uwezo mkubwa sana wa lugha ya Kiingereza na Kiarabu.

Na kasoma vizuri Qur'an.
Nadhani mtu wa kusaidiwa ni wewe.
 
Kolola,
Ikiwa umekusudia mimi nimsaidie Maalim Faiza nataka nikufahaishe kuwa Faiza haitaji msaada wa yoyote katika ukumbi huu.

''Intellect'' ya Faiza ni wachache sana hapa wanaweza hata kuikaribia.
Sitanii.

Pitia post zake hapa zisome hili utaliona.
Pia ana uwezo mkubwa sana wa lugha ya Kiingereza na Kiarabu.

Na kasoma vizuri Qur'an.
Nakubaliana nawe ila anakosa hekima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom