Shairi: Zawadi kwa wapenzi wote wanaotunziana siri

Aug 4, 2017
49
34
Hamjambo wadau.

Unajua kuna baadhi ya mahusiano hufa au kuvunjika kwasababu tu mmoja au wote wawili ni wabwatukaji au ni watu wasio na vifua vya kutunziana siri.

kuna baadhi ya mambo katika mahusiano yanawahusu wawili tu,

Nimewatungia shairi hili wale wote wenye nidhamu za kutunza siri ktk mahusiano.

1. wapenzi wengi wamekosa umahiri, umahiri wa kutunza siri,

lakini wewe u mzuri, umenitunzia siri,

nimekukosea mengi lakini umeyafanya mazuri,

u mzuri wewe uliye msiri.


2. tulipokula mbatata kwa ugali, haya yote ulisitiri,

haujawahi kuropoka, nakiri, yanayotuhusu wawili,

unayatunza yanayojiri, ndani ya chumba chetu cha siri,

u mzuri wewe uliye msiri.


3. wapenzi wengi ni machachali, wanaropoka bila siri,

ukiwakanya ni wakali, kama wamelamba shubiri,

jinsi unavyonisitiri, sijawahi choka kukujali,

u mzuri wewe uliye msiri.


4. wapenzi wengi ni wazuri, lakini hawana siri,

wakinunua binzari, hutangaza hadi mtaa wa pili,

hongera kwa kunisitiri, na kunifanya niwe rijali,

u mzuri wewe uliye msiri.


5. wapenzi wengi ni wakali, zaidi ya ladha ya pilipili,

lakini wewe unajali, mpole kama kivuli,

maneno yao kama shubiri, maneno yako matamu kama kidali,

u mzuri wewe uliye msiri.


2017, shairi hili limeandikwa na Mniko The Poet.
 
safi sana mkuu watunzi wa mashairi wanapotea sana hivi karibuni
kweli mkuu unajua mashairi yana raha yake, kwenye nchi zilizoendelea wana kitu kinaitwa MIC POETRY(POETRY READ LOUD) na fans hulipia kwenda kuenjoy event kama hizi.
 
safi sana mkuu watunzi wa mashairi wanapotea sana hivi karibuni
kweli mkuu unajua mashairi yana raha yake, kwenye nchi zilizoendelea wana kitu kinaitwa MIC POETRY(POETRY READ LOUD) na fans hulipia kwenda kuenjoy event kama hizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom