doullar
Member
- Dec 29, 2016
- 31
- 13
Sauti yangu napaza,kuwaita mlo mbali
Natawaka kuuliza,munipe jibu la kweli
Moyoni lanitatiza,lanisumbua akili
Tumekuja duniani,tutumize lengo gani
Swali msije lipuza,kaniona punguani
Au msije nibeza ,kuniona limbukeni
Mpate la kueleza,likanikifu moyoni
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Mjibu watu wa dini,hata mlo wapangani
Wenye imani za chini,hili swali jaribuni
Msiyafiche moyoni,hayo majibu nipeni
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Wasomi mlo chuoni,swali hili ni la kwenu
Au mnasoma nini,msojua lengo lenu
Mtanipa walakini,nikikosa jibu kwenu
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Wenye elimu za chini,nanyi nimekusudia
Chonde jawabu nipeni,nami nipate ridhia
Najua hili si geni,mengi mmeyapitia
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Mujibu kwa kiswahili,lugha iliyonikuza
Majibu yenye dalili,msije kunichagiza
Mseme yaliyo kweli,uongo nimekataza
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Hapa naweka kituo,sigeuke msemaji
Nangoja michanganuo,kutoka kwa wajuaji
Sijalenga kusudio,wadau mnipe mji
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Sent from my iPhone using JamiiForums
Natawaka kuuliza,munipe jibu la kweli
Moyoni lanitatiza,lanisumbua akili
Tumekuja duniani,tutumize lengo gani
Swali msije lipuza,kaniona punguani
Au msije nibeza ,kuniona limbukeni
Mpate la kueleza,likanikifu moyoni
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Mjibu watu wa dini,hata mlo wapangani
Wenye imani za chini,hili swali jaribuni
Msiyafiche moyoni,hayo majibu nipeni
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Wasomi mlo chuoni,swali hili ni la kwenu
Au mnasoma nini,msojua lengo lenu
Mtanipa walakini,nikikosa jibu kwenu
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Wenye elimu za chini,nanyi nimekusudia
Chonde jawabu nipeni,nami nipate ridhia
Najua hili si geni,mengi mmeyapitia
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Mujibu kwa kiswahili,lugha iliyonikuza
Majibu yenye dalili,msije kunichagiza
Mseme yaliyo kweli,uongo nimekataza
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Hapa naweka kituo,sigeuke msemaji
Nangoja michanganuo,kutoka kwa wajuaji
Sijalenga kusudio,wadau mnipe mji
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani
Sent from my iPhone using JamiiForums