Shairi "tumeumbiwa nini"

doullar

Member
Dec 29, 2016
31
13
Sauti yangu napaza,kuwaita mlo mbali
Natawaka kuuliza,munipe jibu la kweli
Moyoni lanitatiza,lanisumbua akili
Tumekuja duniani,tutumize lengo gani

Swali msije lipuza,kaniona punguani
Au msije nibeza ,kuniona limbukeni
Mpate la kueleza,likanikifu moyoni
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani

Mjibu watu wa dini,hata mlo wapangani
Wenye imani za chini,hili swali jaribuni
Msiyafiche moyoni,hayo majibu nipeni
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani

Wasomi mlo chuoni,swali hili ni la kwenu
Au mnasoma nini,msojua lengo lenu
Mtanipa walakini,nikikosa jibu kwenu
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani

Wenye elimu za chini,nanyi nimekusudia
Chonde jawabu nipeni,nami nipate ridhia
Najua hili si geni,mengi mmeyapitia
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani

Mujibu kwa kiswahili,lugha iliyonikuza
Majibu yenye dalili,msije kunichagiza
Mseme yaliyo kweli,uongo nimekataza
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani

Hapa naweka kituo,sigeuke msemaji
Nangoja michanganuo,kutoka kwa wajuaji
Sijalenga kusudio,wadau mnipe mji
Tumekuja duniani,tutimize lengo gani



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Sote waja tumeumbwa, mola kumsujudia
Pekeye ndo wakuombwa, dini kumtakasia
tuyawache tulogombwa, mema kuyakimbila
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaaa

Tumeumbwa kwa kusudi, si bahati ilo mbaya
Kujua hatuna budi, hiso faradhi kifaya
elimu na uweledi, ujinga mwisho mbayaa
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaa

Dunia chumba cha dhiki, mola amejaalia
tuishi kwa tekiniki, kifo chatukaribia
usije dhani hung'oki, mauti yatakujia
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaa.

Ndugu ulotoa mada, haya majibu nakupa
upate nyingi faida, usije kutoka kapa
elimu yako mazida, kwazote dhambi kukwepwa
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaaa




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sote waja tumeumbwa, mola kumsujudia
Pekeye ndo wakuombwa, dini kumtakasi
tuyawache tulogombwa, mema kuyakimbila
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaaa

Tumeumbwa kwa kusudi, si bahati ilo mbaya
Kujua hatuna budi, hiso faradhi kifaya
elimu na uweledi, ujinga mwisho mbayaa
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaa

Dunia chumba cha dhiki, mola amejaalia
tuishi kwa tekiniki, kifo chatukaribia
usije dhani hung'oki, mauti yatakujia
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaa.

Ndugu ulotoa mada, haya majibu nakupa
upate nyingi faida, usije kutoka kapa
elimu yako mazida, kwazote dhambi kukwepwa
JF itambue,lengo la sisi kuumbwaaa




Sent using Jamii Forums mobile app

Shukurani safuheri,kwayo majibu sawia
Atakulipa kahari,nduguyo nakuombea
Nami naweka nadhiri,kazi nitayafanyia
Niieneze habari,kuikumbusha dunia


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Bora umejua hilo, ndungu dulla shukurani
Tuliloumbiwa ndilo, latuweka duniani
Ziada ya hii milo, kutupa nguvu mwilini
ila sio lengo hilo, hilo weka akilini
Shukurani safuheri,kwayo majibu sawia
Atakulipa kahari,nduguyo nakuombea
Nami naweka nadhiri,kazi nitayafanyia
Niieneze habari,kuikumbusha dunia


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hima mja tajikima,kufanya yalo mazuri
Swala iwe ya lazima,kumtukuza dahari
Kufunga ntajituma,niisubiri futari
Aniongoze karimu,pepo nikaisubiri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom