Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,834
Tulikupeleka shule, Elimu ukaipata
Tulijinyima tusile, Huduma ukaipata
Ulifanya tusilale, Matunzo kuyatafuta
Toto letu hili tundu, Limekuwa ni sipika
Hutaki maendeleo, Unapiga makelele
Huna hata mwelekeo, Nchi wataka ilale
Twataka maendeleo, Si maneno hayo tele

Uzalendo wako nini, Hebu nieleze sasa
Vipi huko kijijini? Wanacheza kwasakwasa?
Huvipendi vya nyumbani, Ni nini ulichokosa?

Kila kitu unabeza, Umegeuka uchungu
Wajifanya mangimeza, Kuwatetea wazungu
Vijana wawapoteza, Badilika ndugu yangu

Wewe kipaza sauti, cha wanyonyaji wa kale
Zawadi yako ni suti, na wezi ni wale wale
Unapewa matikiti, Ili upige kelele

Wale sio ndugu zako, Ka jojo wakutumia
Sisi ndio ndugu zako, Ukitemwa kufikia
Wale huko ni koboko, kung’ata wamezoea

Elimu uliyopata, Tumia kujenga nchi
Acha kuwa ni robota, la kubebea kabichi
Huo ni ujinga futa, Simama tujenge nchi

Chungu ni wadogo sana, Lakini wako pamoja
Kwanini wapenda sana, Kuvunja wetu umoja?
Sifa umepata sana, Sasa wafanya vioja

Tamati nimefikia, Maelezo nimeyatoa
Ujumbe kuwafikia, Sina haja kokotoa
Ndugu yetu kasikia, Aachane kukodoa