Shairi: Sisi Nyuki tunasema, tupo na Malkia wetu

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,971
2,000
SISI NYUKI TUNASEMA, TUPO NA MALKIA WETU

1. Sisi ni nyuki wakali,
Imara tumesimama
Kwa dhati pia ukweli,
Tutamsaidia mama
Tuko ngangari kamili,
Kuipa nchi heshima
Sisi nyuki tunasema,
Tupo na Malkia wetu


2. Malkia keshasema,
tayari yuko kamili
Mpole mtenda mema,
Ni mtu anayejali
Imara amesimama,
Nchi kuipa asali
Sisi nyuki tunasema,
Tupo na Malkia wetu


3. Nyuki tunafanya hima,
kutengeneza asali
Sasa zama za neema,
na siyo za ukatili
Uonevu na nakama,
Hivyo vipishie mbali
Sisi nyuki tunasema,
Tupo na Malkia wetu


4. Hima tena fahima,
hii haina kufeli
Wote mnaolalama,
Mioyo tulizeni tuli
Za ukweli hizi zama,
Siyo propaganda kali
Sisi nyuki tunasema,
Tupo na malkia wetu


5. Hizi ni zama za nyuki,
Na siyo zama za chawa
Nyuki hatutaki kiki,
Na misifa kuimbiwa
Namba moja kwetu haki,
kunyoosha sawasawa
Sisi Nyuki tunasema,
Tupo na malkia wetu
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,967
2,000
SISI SI NYUKI, KIONGOZI WETU KIONGOZI WA MALAIKA

1. Sisi si nyuki wala wali,
Imara, madhubuti twang'aa hali,
Msingi wetu ni kazi ya ukweli,
Bi Mkubwa na timu hawana hali,
Amepungua uongozi bora si kamili,
Ulaghai na kukwepua nchi zake mali,
Sisi si nyuki bali watu,
Anaongoza Malaika kiongozi wetu.

2. Malaika wote kiasili,
Wamethibitisha yuko kamili,
Mpole mwema, mwenye akili,
Ni kiongozi imara na ajilali,
Imara amesimamia mali,
Nchi aliipa asali na nzuri hali,
Sisi si nyuki bali watu,
Anaongoza Malaika kiongozi wetu.

3. Hata nyuki wafanyao hima,
Hukiri wazi hii ni nyingine neema,
Fadhila kuu na tele rehema,
Si uzembe, ubadhirifu hizi zama,
Rushwa, wizi, na hujuma kwa umma,
Hivyo viliepushwa na Chuma,
Sisi si nyuki bali watu,
Anaongoza Malaika kiongozi wetu.

4. Hila na nuksi tena ni historia,
Aliweka Bulldozer makini doria,
Wote raia kwa nyuso wanaashiria,
Treni ya umeme inangoja abiria,
Bwawa la Nyerere uzinduzi husubiria,
Si propaganda wala hadithi za kufikiria,
Sisi si nyuki bali watu,
Anaongoza Malaika kiongozi wetu.

5. Nasema katu hizi si zama za nyuki,
Na wala siyo zama za mingi mikiki,
Ni rai ya maendeleo na miradi lukuki,
Uzalendo wa kweli ndio mpingo kisiki,
Namba moja ni JPM hata vipi uhamaki,
Kaonesha njia ya yakuti na akiki,
Sisi si nyuki bali watu,
Anaongoza Malaika kiongozi wetu.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,800
2,000
Tunataka Katiba mpya kama asali kutoka kwa malkia nyuki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom