Shairi: Mlaaniwe

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
629
1,013
Mulaaniwe.
Sio kwa matungulile, wala ndulele mekoni
Si kama kinjekitile, unga na maji ya mtoni
Ni kwa hilo jasho tele, Damu tabu za maskini
Nasema Mulaaniwe huu wimbo mpya mjini

Mkata mkato umemkata, kwenye simuni maskini
Wamdumishia ukata , yala! ni hospitalini
Haitoshi kutibika, akatutoka jamani
Nasema Mulaaniwe, mulaaniwe milele

Mtwana pamoja watwana , wakike tumwite nani
Kabisa tunalandana , jasho letu vietini
Bado twa beba mabwana, da! tupo utumwani
Mulaaniwe kwa jasho, mulaaniwe milele

Mapasipoti shidani, garama nao mlolongo
Fursa za ugaibuni, mnatufelisha wabongo
Tumewakosea nini, mwatupiga na magongo
Nasema mulaaniwe, na vizazi vyenu vyote

JamiiForums-458733577_474x492.jpg
 
View attachment 2014019
Mapasipoti shidani, garama nao mlolongo
Fursa za ugaibuni, mnatufelisha wabongo
Tumewakosea nini, mwatupiga na magongo
Nasema mulaaniwe, na vizazi vyenu vyote
 
Back
Top Bottom