Shairi (la kubuni) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shairi (la kubuni)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by funzadume, Jun 18, 2010.

 1. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Hapo nilipo nalia sina pa kukimbilia
  Mke kanikimbia na watoto kachukua
  Sina pa kusemea dunia imeniinamia
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  Nilipokuwa mzima, watu hawakunisema
  si Rehema si Fatuma, ambao wanisakama
  wanasema si mzima, utadhani wamenipima
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  vipele vinanitoka, kujikuna nimechoka
  najiona takataka, mwili unaninuka
  kutembea ninataka, ila nguvu zimekata
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  Hospitali nikienda, manesi wananiponda
  basi nikitaka panda, nazuiliwa na konda
  wajiona kama ganda, lililo njiapanda
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  naomba wasamalia, mje kunisaidia
  kifo chaninyemelea, kaburi lanililia
  nuru yanipotea, fahamu zanikimbia
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  nikienda maskani, wananiteta wahuni
  wote hawanitamani, nimepoteza thamani
  sitakiwi duniani, kwangu ni kaburini
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  by Funzadume (mwana wa Washawasha)
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pole sana funzadume, kwa hayo yaliyokupata,
  Huo ndio uanaume, kuvumilia matata,
  Umekanyaga umeme, mchana wa saa sita,
  Japokuwa umenaswa, JF hatutakutenga.
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Duh... Mwanakijiji yuko wapi aunganishe
   
 4. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  kila nikikohoa watu wanaziba pua
  nikitaka kunyoa, vinyozi wanikimbia
  sina pa kukimbilia, naijutia dunia
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  nilipopata sijajua, maana ni nyingi njia
  sindano za kuchangia , au nyembe kunyolea
  ngono sikuzembea, mpira nilivalia
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI

  jaribu nawe kupima, huenda si mzima
  Kaburunye nimekusoma, asante kwa huruma
  achana na kina Halima, watakuambukiza ngoma
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  bado hajaamka si unajua dunia tunatofautiana masaa
   
 6. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hahahahaaa, umenikumbusha enzi zileeee:

  Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
  kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
  watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
  wakataka na kauli, iwafae maishani

  akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli
  hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
  roho naona yachinjwa, kifo kinanikabili
  kama mnataka mali semeni niseme nini
   
 7. masharubu

  masharubu Senior Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kilio unacholia,funza tumekisikia
  Sina cha kukuambia,wewe sasa tangulia
  Dua tutakuombea,peponi kwendatulia

  Watoto tutawalea,na mama yao pia
  skuli wataingia,shaka hiyo ondoa
  Ada tutawalipia,pasi na kwabagua

  Masharubu ninalia,funzadume waondoka
  Wapitutakimbilia,machozi yanatutoka
  Jamvini Utapotea,yako yatasahaulika
   
 8. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  shuka mistari tuendelee na shairi letu
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  nashukuru masharubu, umegonga sukurubu
  kwa Muumba natubu, nawafuata mababu
  jinsi navyopata tabu, kutokufa sina sababu
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hongera Funzaadume naona sasa mtaanza kwenda sambamba na mwanakijiji na MJ1
   
 11. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  thanks mpendwa
   
 12. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Funzadume sikiliza, nikupe zangu nasaha
  Ngono uliendekeza, ukadhania ni raha
  kwa kweli umeteleza, imegeuka karaha
  Pole sana mwanakwetu, kwa hayo yaliyokupata

  Nakushauri mwenzangu, sasa hebu ugeuke
  Atakusamehe Mungu, Kama ukitubu kwake
  Ataondoa uchungu, hatakupiga mateke
  Mungu husamehe dhambi, ukitubu kwa ukweli

  Watafute walokole, wakufanyie maombi
  Mwasema wana kelele, lakini hawana dhambi
  Yamekutoka mapele, utapona kwa maombi
  Mungu aponya ukimwi, hata wafu afufua

  wamkumbuka jeska, yule dada wa haruna,
  alikuwa mwathirika, kwa maombi amepona
  jambo hili ni hakika, hata wewe utapona
  hebu ufanye haraka, usiwe na moyo mgumu

  hapa tamati nafika, nina majonzi moyoni
  uchungu umenishika, hili ni balaa gani
  funzadume wangu kaka, umenitia huzuni
  Mungu akusaidie, upone ugonjwa wako
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  shauri nimelipata, tatizo vipi tafika
  kufika kwa katekista, nauli zahitajika
  hela zimeshakata nakabiliwa ukata
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI
   
 14. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Eneo la tanganyika, pekazi pale ya kawe
  watu waliookoka, watakutoa kiwewe
  usije kudanganyika, ukaelekea msewe
  kama nauli ni shida, piga simu wakufate.

  namba za simu nataja, ziandike kwa makini
  sifuri saba sita moja, ile voda ya zamani,
  ukipiga watakuja, wewe uwe na imani
  dawa ya ukimwi moja, nayo ni jina la Yesu
   
 15. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  imani inaponya, lakini kwangu hapana
  gonjwa lanisakanya, siwezi hata kuona
  nimekuwa kama nyanya, ningali bado kijana
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI
   
 16. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mungu wetu anaponya, funzadume sikiliza,
  hata uwe kama nyanya, hili halitatiza,
  amemponya matonya, juma na hata Aziza,
  wewe nenda pale kawe, au wapigie waje
   
 17. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  simu nilishauza, nipate kujiuguza
  kutembea kwanikwaza, nguvu nimepoteza
  tumaini nimepoteza, nakufa mie funza
  Ndugu tusiwatenge, wagonjwa wa UKIMWI
   
 18. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Waelekeze nyumbani, kama simu umeuza
  wamo humu jamvini, waje shetani kumchakaza

  sema unaishi wapi, niliwalete maskani
  wakaa mtaa upi, nieleze kwa umakini
  watakuja na mshipi, wakutoe mautini
  Jina la Yesu kiboko, funzadume uamini
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Funzadume nimekuja, sio kukutia tabu
  majibu ninayo ngoja, sio kukupa sulubu,
  uliopata ugonjwa, haki unanipa tabu,
  Gonjwa hilo la ukimwi, wapi ulilipatia?

  Vyanzo vyake vingi kweli, kutwa hatwishwi ambiwa
  wewe msema ukweli, chanzo wakijuulia
  uliupata kwa mwali, au nao wezaliwa?
  Gonjwa hilo la ukimwi, wapi ulilipatia?
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,489
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  siwezi kukupa jibu, wapi nilipopatia
  labda kwenye ulabu, akili zilipotea
  ushauri wa tabibu, kinga nilitumia
  Ndugu tusiwatenge wagonjwa wa UKIMWI
   
Loading...