Shairi la chupi:- wadau wa lugha mwaombwa kulihakiki


Wangooto

Wangooto

Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
18
Likes
0
Points
3
Wangooto

Wangooto

Member
Joined Feb 1, 2013
18 0 3
Watoto leo twalia, siri za baba kuvuja, Vya ndani kuchungulia, tumegeuka vioja, Wewe demokrasia, mbona sharia wavunja, Chupi ina umuhimu, kwa abu na mwana pia. Ili uwe muungwana, umeivua chutama, Bado unagangamana, kwa jeuri wasimama, Ushauri umekana, wajiona akrama, Chupi ina umuhumu, kwa abu na mwana pia. Baba huivai chupi, asili umeitweza, Wanatwaona mshipi, sasa umetuumiza, Nidhamu leo ni kapi, heshima tumepoteza, Chupi ina umuhimu, kwa abu na mwana pia. Adhifari lamsiki, Pua I yataka kheri, Najua utahamaki, kwa shari pasi fakuri, Tulia na uhakiki, neno kila kistari, Chupi ina umuhimu, kwa abu na mwana pia.
 

Forum statistics

Threads 1,273,853
Members 490,528
Posts 30,493,527