SHAIRI: Kitambi kimeniponza

getemsales

Member
Feb 8, 2017
6
9
Kitambi kimeniponza


Kitambi kimeniponza, sina hamu asilani.
Kimenifanya nawaza, maisha si ya thamani.

Mahari mara ya kwanza, natakiwa milioni.

Wakashindwa kunioza kwa laki tano jamani.

Nikampenda shariza, asili ya arabuni.
Ile tu kumposa, dhahabu za milioni.
Ni kitambi sina pesa, mi kabwela kama nini.
Kitambi kinaniponza, nakosa mke jamani.
fat-man.jpeg
 
Kitambi kimeniponza


Kitambi kimeniponza, sina hamu asilani.
Kimenifanya nawaza, maisha si ya thamani.

Mahari mara ya kwanza, natakiwa milioni.

Wakashindwa kunioza kwa laki tano jamani.

Nikampenda shariza, asili ya arabuni.
Ile tu kumposa, dhahabu za milioni.
Ni kitambi sina pesa, mi kabwela kama nini.
Kitambi kinaniponza, nakosa mke jamani.
View attachment 1158156
Kitambi umekifuga,na huku huna shilingi
Huna pesa za kuhonga,na kulipa mashangingi
Nazi yako longalonga,ajira sina misingi
Punguza hicho kitambi,kisije kuponza tena

Hebu Fanya mazoezi,uzingatie na Nazi
Nakuchana waziwazi,sutaki uvunje Nazi
Usiyawaze mapenzi,uasherati uzinzi
Kama pepo zibarizi,kusi na uvute pumzi
 
Kitambi kitambike, hadharani kifunike
Usije kosa mke,kwa utambi utambike

Utambi umekutoka,tazani wataka chomoka!
Rudisha ulivyokopa,urudi Kama rofa!
Mke hautakosa,kitambi kikinyonyoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom