Shairi: Kipenzi Changu Afrika

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Juu ya mataaluma chombo kimeshika mwendo kasi
Kama Nyoka kwenye majani chateleza kwa kasi
Ndanimwe kimeshiba watu walioketi kwa nafasi

Nipo ndani naangaza katika madirisha ya tumbo lake
Miti na milima yapita ikienda zake
Nakumbuka nyumbani kwetu nilipotoka
Natabasamu kwa raha nikikumbuka Afrika

Mbeleko yako imembeba mwanadamu
Kwa karne nyingi sana yafaa akuheshimu

Umepambwa kwa rubi dhahabu na almasi
Na mito itiririkayo polepole na iendayo kasi
Ukarimu wa watoto wako ni mfano halisi
Wa uzuri wako ewe kipenzi Afrika

Umevumilia ngurumo na misukosuko mingi
Maumivu, na machungu mengi
Kwa upendo na huruma tele
Huku chozi likikutoka ukasema yalopita si ndwele
Ukatoa tabasamu la uchungu ukasema tuangalie ya mbele

Afrika usilie watoto wako watarudi
Watarudi nyumbani wakuletee zawadi
Wamwagilie maua na miti yenye kunyauka
Wakupambe uzidi
kupendeza Afrika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom