Shairi: Haya siyo maisha

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,134
4,293
HAYA SIYO MAISHA.

Watu wanatengana, eti kisa ni pesa
Fukara wanapigana, sababu ni siasa
Hovyo wanagombana, damu wakiinusa
Roho kuchukiana, pendo tukalikosa
Sidhani Kama hivi, haya siyo maisha.

Wanga ni kulogana, yote wanayo chuki
Jini kutupiana, yule kapata hiki
Wivu kuonekana, utu hatuutaki
Sana twakuwaruzana, wengi ni mamluki
Sidhani Kama hivi, haya siyo maisha.

Hawa wanasemana,mengi yenye uongo
Wale wasengenyana,kule watema nyongo
Huku tunalishana, la pori lile tango
Mwisho tunalumbana, Kisha twajenga pengo
Sidhani Kama hivi,haya siyo maisha.

Bado twanuniana, kisa huku moyoni
Fundo limeshikana, twalificha usoni
Twadai twapendana, neno la mdomoni
Rohoni tungeona, amekaa shetani
Sidhani kama hivi, haya siyo maisha.

SHAIRI - HAYA SIYO MAISHA.
MTUNZI - Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Ninga hapo umejenga,mjengo wa moyo huru
Na beti umezipanga,kuhusu chuki ,Uhuru
Jamie nipe kipenga,wenye chuki niwadhuru
Dunia anga kaanga,iwe kakara kukuru

Wenye chuki wanaboa,sitaki kuwachukia
Maneno wanachokoa,domo lao lanukia
Kwa domo wanadonoa,maudhi kupayukia
Dunia anga kaanga ,iwe kakara kukuru
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom