Shairi: Braza Punguza Mwendo

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,292
Braza punguza mwendo.

1)achapo nikuusie,japowe mtu mzima.
Sikiza na usikie,jahazi lenda kuzama.
Fanya le ujiundie,hawatoacha kusema.
Braza punguzaga mwendo,na mbele jitazamie.

2)jinsi le uwazuie,uwape nguvu mapema.
Bora kaka wachunie,we waone makima.
Kule usikimbilie,ukue mkata pema.
Braza punguza mwendo,na mbele jitazamie.

3)midomo wafungulie,kuwa na moyo wa chuma.
Bure cha wajinunie,wewe fata taaluma.
Kijiji kitung'arie,utapata taadhima.
Braza punguza mwendo,na mbele jitazamie.

4)acha te nikuambie,matunda ya usichuma
Makofi wakupigie,na salamu wakituma.
Ila le na usikie,usiharibu mapema.
Braza punguza mwendo,na mbele jitazamie.

5)na wale uwaambie,kile che ni cha karima.
Acha wa wakitambie,tambiko litaja tima.
Mjute mjililie,mate watapowatema.
Braza punguza mwendo,na mbele jitazamie.

Shairi:BRAZA PUNGUZA MWENDO.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyllyninga@gmail.com
 
barabara yaruhusu,wacha nipite mie
mwendo si ajali,
kwako ondoa hofu
povu lakutoka,braza wacha hofu
weka wako mkanda,kitambi shikilie.

braza fumba macho,kasi usiione
dereva weka mwendo,abiria wakome

kumbe na mm najua ushairi...:(:(:(
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom