Shaidi muhimu kesi ya Zombe mahututi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shaidi muhimu kesi ya Zombe mahututi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Mar 3, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Rashid Lema, mmoja wa watuhumiwa wawili muhimu ambao bado hawayasimama kizimbani kutoa maelezo yao yu mahututi. Hali yake ilibadilika jana katika gereza la keko na akapelekwa hospitali ya Temeke. Leo asubuhi, alipewa rufaa kwenda muhimbili ambako amepokelewa muda mfupi uliopita na amelazwa.
  Maelezo ya lema yanadhaniwa kuwa ni muhimu kwa sababu ni mmoja wa watu wanaoelezwa kuwa walishuhudia tukio la mauaji. lakini ilipofika zame yake ya kusimama kizimbani kujitetea, alishindwa kufanya hivyo kwa sababu za kiafya
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Hivi, hii sinema ya huyu shahidi..kwa nini wasipate ushahidi wake kabla hayajatokea ya kutokea ambayo naona ni almost imminent?
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mpita Njia shukrani kwa habari, manake kulikuwa kuna tetesi kuwa amefariki. Mungu amsaidie apate nafuu haraka, ili aweze kuja kutoa ushahidi katika kesi inayowakabili.
   
 4. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwanini mpaka azidiwe ndio wampeleke Hospitali? Hapo lazima Zombe na Mkuu wa gereza waelezee umma ni vipi kapatiwa huduma za matibabu hapo nyuma otherwise imepangwa kuwa azidiwe au amezidishwa kuwa mgonjwa na sio mungu wetu anavyopangaga tuugue, kwanini nasema hivyo? kuna jamaa aliwamwagia tindikali watu kule Mwanza akiwamo na mbunge mmoja baadaye akakamatwa akapelekwa mahabusu na kabla hajaeleeza chochote cha muhimu akapelekwa hospitali kama favour fulani vile kumbe bwana jamaa wamesuka!!! na baadaye alifia Hospitalini Tanzania chochote kinawezekana wazee!
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa nini mahakama isihamia huko alipo,mbona mahakama ilienda msitu wa pande,wanasheria mtufafanulie kuhusu hili kwani sasa yamezidi mara balali,mara shahidi wa EPA mara shahidi kesi ya Zombe,ni kesi au ka mchezo?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  KUna taarifa kuwa alifikishwa Muhimbili tangu saa 5 leo asubuhi lakini manesi walikataa kumpokea hadi wakazozana na maofisa wa magereza waliomleta. Amepokelewa rasmi majira ya saa 10 alasiri
   
 7. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mungu anaweza kupanga lolote na likatokea na binadamu hana uwezo kama huo. refer the doctrine of pre-destination
   
 8. S

  SkillsForever Member

  #8
  Mar 3, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kuna nini??hakuna zengwe kweli hapo?namuombea apone haraka.....pole sana lema..kwenye ukweli na haki ipo pia!!!
   
 9. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  story za mafia tulikuwa tunazisoma kwenye vitabu sasa tunazishuudia live kutoka kwa viongozi wetu. hapo lazima kuna kitu kikubwa kinaendelea lazima mtu afe ili wengine waokoke na kufungwa maisha au kunyongwa.

  Tanzania inatisha siku hizi.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Taarifa kutoka Muhimbili leo zinaeleza kwua hali ya lema imeimarika. daktari anayemhudumia anasema kuwa sasa anaweza kula, kuzingumza na kutembea mwenyewe bila msaada. Kutokana na kuimarika kwa afya take, anaweza kuruhusiwa wakati wowowte
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na akipona basi,,,maana nna wasiwasi sana na yanayomkuta. katika dunia yetu hii mengi yanaweza kufanyiziwa na mtu yeyote. Ikumbukwe kuwa wanaomtibu huko gerezani ni askari magereza ambao kumfanyia ufisadi ni rahisi kwa rubuni kidogo tu. Huyu alikuwepo na amekiri yote yaliyotokea siku ile kule msituni, hivyo sitoshangaa kama kuna kitu ambacho atakuwa amefanyiwa na wenzake. Na kwa nini mahakama isimwamuru huyu mshitakiwa mwingine aliyebaki atoe ushahidi wake? Kwa nini aseme mpaka Lema atakaposema ndo atasema? Kwani lema ndo msemaji wake? Anaficha nini? Na Lema akirehemika leo hatatoa utetezi wake?
  Mchezo wa kuigiza huu!!!!
   
Loading...