Shahidi wa kumi katika kesi ya kughushi mukhtasari wa serikali aibua mzozo

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Shahidi wa kumi katika kesi ya kughushi mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi iliyofunguliwa na mkuu wa wilaya ya zamani,Dahn Makanga ameibua mabishano ya kisheria katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha mara baada ya wakili wa upande wa utetezi,Ephraim Koisenge kuomba kumtambua shahidi huyo.

Hatua hiyo ilitokana na kauli iliyotolewa na mwendesha mashtaka wa serikali,Mary Lucas kuiomba mahakama hiyo kuhairisha shauri hilo kutokana na shahidi huyo wa kumi kuwa safarini.

Akizungumza mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,Gantwa Mwankuga wakili wa utetezi,Koisenge alimuomba wakili wa serikali kumtaja shahidi huyo hadharani kwa kuwa katika orodha ya mashahidi waliowasilishwa majina yao mahakamani hapo jina lake halionekani.

Mara baada ya kauli hiyo ndipo mwendesha mashtaka wa serikali,Lucas alijibu kwamba shahidi huyo wa kumi anatoka katika halmashauri ya jiji la Arusha na ni mtumishi katika ofisi za jiji hilo.

Mara baada ya mvutano huo ndipo hakimu Mwankuga alimuuliza wakili wa utetezi,Koisenge endapo ana pingamizi lolote na kujibu hapana na kuamua kuhairisha shauri hilo hadi Julai 11 mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanamleta shahidi huyo mahakamani hapo bila kukosa .

Hadi sasa ni jumla ya mashahidi tisa upande wa mashtaka tayari wameshawasilisha ushahidi wao mbele ya mahakama hiyo ambapo juni 11 mwaka huu shahidi wa mwisho anatarajia kuwasilisha ushahidi wake katika kesi hiyo inayovuta hisia za watu mbalimbali mkoani Arusha.


Katika kesi hiyo nambari 430 ya mwaka 2016 Makanga ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Bariadi Mashariki alifika mbele ya kituo kikuu cha polisi cha kati na kumtuhumu mme mwenzake Mollel kughushi mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kujipatia hatimiliki ya kiwanja namba 231 kitalu DD kilichopo Mianzini jijini hapa.

Mwisho.
 
Back
Top Bottom