Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Shahidi wa sita katika kesi ya Unyang'anyi wa Kutumia Silaha na uporaji inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkaoni Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya(34) na wenzake wawili,Bakari Rahibu Msangi ameieleza Mahakama kuwa kipigo alichokipata ni sawa na nusu kifo kwani alipoteza fahamu kwa muda huku akiwa amefungwa pingu mguuni na mikononi na walinzi wa Sabaya walimwambia kosa ni kuingilia dili ya Mkuu wao na sijui kama anaweza kubaki salama.

Sabaya na wenzake Silyvester Nyengu(26) na Daniel Mbura(38) wanatuhumiwa Kutumia Silaha kupora kiasi hicho cha pesa na Mali katika tukio lililotokea Februari 9 mwaka huu katika duka la Shahiid Store lililopo mtaa wa Bondeni Jijini Arusha duka linalomilikiwa na Mfanyabiashara Mohamed Saad Hajirini (45).

Msangi Alisema mungu ndio anajua kipigo alichokipata kutoka kwa walinzi wa Sabaya walivyompigia kwa amri ya Mkuu huyo na kusema tu hadi Sasa hawezi kusikia vizuri kufuatia masikio yake kutosikika vizuri kufuatia makofi mawili ya nguvu ya mfululizo aliyokuwa akipigwa kichwani,masikioni na mwili mzima na hajui kilichomfanya kuzinduka na kuwa hai hadi Sasa.

Alisema mlinzi wa Sabaya alimwambia Msangi kuwa tatizo lake ni kuingilia dili la Mkuu General Lengai Ole Sabaya na kuwa kiherehere kufuatilia mambo yake na salama yake ni yeye kumwonyesha Mohamed Saad Hajirini au Ally Saad Hajirini alipo vinginevyo hatabaki salama kwani anaweza kuuawa.

Shahidi Alisema hayo wakati akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali,Tumaini Kweka Mbele ya Hakimu Mwandamizi,Odira Amworo na kusema kuwa wafanyabiashara hao wa kiaarabu walitafutwa na Sabaya usiku kucha hadi majumbani mwao lakini hawakuweza kufanikiwa kuwapata usiku huu hadi walipoamua kukataa tamaa.

Alisema wakati anazungushwa mjini maeneo mbalimbali kuwasaka akina Hajirini,Sabaya aliendelea kumtisha kwa Bastola akiwa ndani ya gari na aliomba kutouawawa kwa kuwa ana Mke na watoto ambao wote ni wagonjwa na hana shida yoyote na Sabaya lakini alisisitizwa kuhakikisha anawaonyesha Waarabu ili aweze kusalimika.

Msangi ambaye alikuwa akitoa ushahidi huku akilia kwa uchungu aliendelea kusema kuwa alimsikia Sabaya akisema kuwa shughuli zote anazifanya Arusha za kuwasaka Waarabu ni maelekezo kutoka ngazi ya juu hivyo hakuna kiongozi wa Arusha wala Polisi anayeweza kumuuliza chochote pindi anavyofanya shughuli Arusha.

Alisema na kumsikia Sabaya akitaka Derava amweleza Msangi kuwa mie napata maelekezo kutoka kwa mtu mmoja tu wa nchi hii ya Tanzania( alimtaja Marehemu Dk John Magufuli) na sio mtu mwingine yoyote hivyo usiwe na kiherehere cha kufuata katika mambo yake na akimwona akae mbali kabisa.

Shahidi Alisema Sabaya akimtafuta Mohamed Saad Hajirini hadi nyumbani na kwenye gari alibaki yeye na dereva na baada ya muda alisikia ukunga ukitoka katika nyumba ya Hajirini iliyopo katika majengo ya NHC yaliyopo eneo la Makao Mapya Jiiini Arusha.

Alisema ghafla aliona Sabaya na walinzi wake wakirudi katika magari lakini hawakuweza kumpata Hajirini na waliendelea kulalamika kukosekana kwa Mfanyabiashara huyo ila waliapa kumtia nguvuni na wakimpata cha moto atakiona màana anafanya biashara haramu na kuihujumu Nchi.

Msangi aliendelea kuieleza Mahakama kuwa mmoja wa walinzi wake anaitwa Andwer na dereva walioneiana kumsaidia na kumpa mbinu za kuwasiliana na Ndugu au rafiki na alifanya hivyo kwa kupewa simu na alimpigia Mke wake na alikwenda eneo walipo ndani ya muda wa nusu saa na alipofika alimwomba Sabaya kumsamehe mume wake lakini aliishia kutaka kupigwa Risasi ya kichwa.

Alisema bàadhi ya walinzi wa Sabaya walionyesha nia ya kumsaidia lakini walikuwa wakifanya kwa usiri mkubwa kwani miongoni mwao alikuwa anawajua na walimwaahidi kumsaidia Ila awe mtulivu kwa kuwa Mkuu wao alikuwa amelewa hivyo asiwe na papara.

Mwisho


IMG-20210728-WA0007.jpg
 
Team Magufuli kwa sasa wanaishi kama digidigi! Ubabe wote kwisha!! Makonda amejificha! Hana nyodo tena!

Mnyeti kwa sasa amenywea, mpaka Gwambina imeshuka ligi kuu akiwa hana cha kufanya! Polepole na Bashiru chalii!

Aliyebakia na pumzi kidogo walau ya kukohoa, ni Msukuma pekee!! Gwajima ndiyo huyu anashambuliwa kuanzia ardhini, angani na majini! Muda si mrefu na yeye chalii.

Kweli kutesa kwa zamu!
 
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
 
Usicheke Mkuu Asprin 😂😂😂 anaweza akanyongwa mara moja jamaa akajua kishamaliza kazi kumbe bado mzima 😂😂😂😂. Hivyo hukumu ni lazima iwe utanyongwa hadi UFE. Katesa watu wengi sana huyo pimbi.
 
Shahidi wa sita wa jamhuri katika kesi ya unyan'ganyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Bakari Msangi ameangua kilio mahakamani wakati akielezea mahakama alipokuwa akitishiwa bastola na Sabaya huku akiwa amefungwa pingu miguuni na mikononi.

Msangi ambaye ni Diwani wa Sombetini kwa tiketi ya CCM, aliangua kilio hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiendelea na ushahidi wake huku akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 105, 2021 inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura wanakabiliwa na mashitaka matatu ya unyan'ganyi wa kutumia silaha.

Msangi ambaye alianza kutoa ushahidi wake jana alianza kulia mahakamani hapo wakati akiieleza mahakama namna alivyotekwa na kiongozi huyo na kundi lake ambapo alidai kufungwa pingu miguuni na mikononi akiwa ndani ya gari la Sabaya.

Ameeleza akiwa ndani ya gari hilo wakitoka katika duka la Mohamed Saad, Sabaya alitoa bastola yake na kumtishia nayo huku akimwambia anapenda kumwingilia katika mambo yake.

Shahidi huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa Sabaya aliendelea kumtukana na kumwambia dereva kuwa yeye (Sabaya) anayeweza kuongea nae katika nchi hii ni Rais Dk John Magufuli na siyo takataka nyingine huku akijipiga piga kifuani.

Aliieleza mahakama kuwa Sabaya alimtaka akamuonyeshe nyumba za Saad na ndugu yake na alipofika kwa Mohamed eneo la Dar Express, Sabaya aliwaeleza walinzi aliowakuta katika eneo hilo kuwa yeye ni DC wa Hai na ameelekezwa na Rais kufanya kazi fulani hivyo walinzi hao wakamuonyeshe anapoishi mtu huyo.

Shahidi huyo alidai mahakamani hapo kuwa baada ya dereva wa Sabaya na mmoja wa mabaunsa wake kumpa simu yake alimpigia mke wake na kumweleza kuwa ametekwa na Sabaya katika eneo la Tulia Lodge hivyo atafute jirani mmoja amsindikize katika eneo hilo.

Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kumpigia simu mke wake aliambiwa afiche simu zake maungoni kwake na mke wake alipofika eneo hilo alipiga magoti mbele ya gari la Sabaya na kumuomba kiongozi huyo amwachie mume wake.

Alidai Sabaya alitoa bastola yake na kumwita mkewe na kumwelekezea bastola kichwani na kisha mdomoni huku akimwambia atamuua ambapo mmoja wa mabaunsa wa Sabaya walimwambia Msangi asiongee kitu kwani Sabaya alikuwa amelewa na risasi ilikuwa kwenye chamber hivyo anaweza kumuua mkewe.

Shahidi huyo alidai kuwa kabla ya kuelekea katika Lodge ya Tulia wakiwa ndani ya gari la Sabaya aliona simu ikiita(Whatsapp) iliyoandikwa DC Arusha Kenan ambapo ilipopokelewa alisikia Sabaya akisema location Mt. Meru.

Shahidi huyo alidai wakiwa katika eneo la hospitali ya Mt. Meru Sabaya alichukua fedha walizokuwa wametoka nazo dukani kwa Shaahid na kuweka bundle la kama Sh milioni moja kwenye soksi mguu wa kushoto na nyingine mguu wa kulia kisha akashuka kwenye gari.

Alidai baada ya kurejea kwenye gari alimsikia mshitakiwa huyo wa kwanza akisema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi ni maskini huku akisema angalia gari analoendesha (Altezza).

Alidai Sabaya alipokea simu nyingine na baada ya kuikata aliwaambia walinzi wake kuwa huyo aliyekuwa anazungumza naye ni OC CID wa Hai aliyemweleza kuwa watu aliokuwa amewakata mchana wametoa hela hivyo aifuate na ndipo walielekea Tulia Lodge, Sakina.
 
Team Magufuli kwa sasa wanaishi kama digidigi! Ubabe wote kwisha!! Makonda amejificha! Hana nyodo tena!

Mnyeti kwa sasa amenywea, mpaka Gwambina imeshuka ligi kuu akiwa hana cha kufanya! Polepole na Bashiru chalii!

Aliyebakia na pumzi kidogo walau ya kukohoa, ni Msukuma pekee!! Gwajima ndiyo huyu anashambuliwa kuanzia ardhini, angani na majini! Muda si mrefu na yeye chalii.
Usisahau na team upinzani inazidi kukiona cha moto. Wameanza na kaka lao Mbowe kapigwa kesi ya ugaidi, halafu atafungwa miaka ambayo idadi yake haijulikani. Akija kutoka huko ashakuwa zezeta tayari.

Hii nchi hii!!!!
 
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Ndio maana hukuwa mwanasheria maana unhekuwa mwanasheria kesi zite ungekuwa unashindwa kama maswali yenyewe ndio haya!!! 😱😱😱
 
Mkuu,

Mbona hujatuletea Cross Examination baina ya Mawakili upande wa Mtuhumiwa pamoja na Shahidi?

Ukikutana na Mawakili wanaouliza maswali ya kiakili, mashahidi wengine wangekataa kutoa Ushahidi.

Umesema umepigwa karibu na kifo, unaweza kuelezea mahakama hii kifo ni nini? Nusu yake je? Umewahi kufa ukajua kukoje?

Umesema umefungwa miguu na pingu, kweli au si kweli? Miguu yako ina mzunguko kiasi gani? Iweje pingu ya kufungia mikono ikaweza kukufunga Miguu?
Unajua ukubwa na mechanism ya lock ya pingu mkuu?? Hujawahi kujiuliza kwanini inafunga watu wote wenye mikono minene na myembamba na haichomoki hata ukiwa na mikono myembamba??

Hata hivyo tusubiri tu kama kuna X examination ya Wakili msomi mshkaj wangu Mahuna tutaziona tu
 
Kenani Kihongosi naye inabidi aitwe mahakani sio? Kwamba aliondolewa umaskini kidogo na Sabaya
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom