Shahidi kesi ya Sabaya, wenzake aenda kushiriki swala la Eid El Hajj, kesi yaahirishwa

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,352
11,477
Kesi ya Sabaya? Ha ha ha! Anashinda mchana hivi anaondoka akionesha vidole viwili alama ya ushindi. Huku akiwa amewagaragaza waliomshtaki.

Mbona inaonekana tu ipo wazi wala hata haihitaji Darubini kuangalia kesi inavyoelekea.

----

Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili leo imeahirishwa kwa kuwa shahidi wa pili Numan Jasin (17) anashiriki ibada ya Eid El Hajj hivyo itaendelea Alhamisi Julai 22, 2021.

Shahidi huyo alikuwa msaidizi wa duka la mfanyabiashara Mohammed Saad linalodaiwa kuvamiwa na Sabaya na wasaidizi wake.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya na wasaidizi wake wawili, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura wanashtakiwa kwa makosa matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akiongozwa wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka jana Jumatatu jioni shahidi huyo alidai kuwa, Sabaya na wenzake baada ya kuvamia dukani waliwaweka chini ya ulinzi na kuwapiga huku wakiwarekodi kwa simu kuzungumza mambo waliyotaka.

Jasin amesema walilazimishwa kukiri kuwa waliiba dola 70,000 mjini Moshi na kuwa wanafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kinyume cha sheria la sivyo wangefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Shahidi huyo amesema wakiwa dukani walipigwa na kusachiwa na mabaunsa waliokuwa wakiongozwa na Sabaya.

Amesema waliokuwa chini ya ulinzi ndani ya duka hilo ni pamoja na Ally Saad, Fundi Salim, Annas, Tajirin na msichana mmoja aliyefika dukani kama mteja.

Amesema aliyemtambua Sabaya ni Diwani wa Kata ya Sombetini (CCM), Bakari Msangi ambaye alifika dukani na kumuita kwa jina Sabaya.

Jasin ambaye alieleza alikuwa hamjui Sabaya, amesema baada ya Msangi kumuita kwa jina Sabaya alimuuliza kama hajuwi jina lake ndipo alimuita General Lengai ole Sabaya.

Amesema Sabaya alimuhoji Msangi amefuata nini dukani ndipo, alijibu ameitwa na rafiki yake Saad baada ya kumwambia kuna tatizo dukani.

Amesema Sabaya alimweleza Msangi kuwa sisi tunafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kinyume cha sheria.

Awali Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula alieleza Mahakama kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Chanzo: Mwananchi
 
Yule mtu wa system unaanzaje kumfunga , na akitoka tu lazima awanyonye kinyesi watu fulan 😀
 
Asingeingia kabisa huko selo au kupanda lile basi au kuvaa pingu. Tayari kazalilishwa vibaya.

Labda badala ya kupanda karandinga angepewa usafiri wake binafsi wenye AC kila siku kesi.

Na kule lupango kuna choo cha vip ? Atakula kuku chips sidhani kama anaenda kuoga kwa maafande kule na kunya.

Ha ha huyu jamaa ana hali mbaya jamani.

Na kupata vip treatment nadhani inabidi ajiongeze.
 
Akiweza aoneshe vidole 10 vyote, achukue na vya kwako, kama kunyosha vidole kunasaidia, ili atoke mahabusu leo, na kesi ife.
 
Naona wewe jamaa wa Sabaya unateseka Sana. Hivi unadhani Sabaya atachomoka kwenye kesi hii??
Unawajua vizuri CCM, hawana aibu, hawana woga, hawajali kitu chochote zaidi ya chama, waongo, chama kwanza na wanafanya vile itakavyo wapendeza wao na hakuna wa kuwafanya kitu.
 
Kesi ya Sabaya? Ha ha ha! Anashinda mchana hivi anaondoka akionesha vidole viwili alama ya ushindi. Huku akiwa amewagaragaza waliomshtaki.

Mbona inaonekana tu ipo wazi wala hata haihitaji Darubini kuangalia kesi inavyoelekea.

----

Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake wawili leo imeahirishwa kwa kuwa shahidi wa pili Numan Jasin (17) anashiriki ibada ya Eid El Hajj hivyo itaendelea Alhamisi Julai 22, 2021.

Shahidi huyo alikuwa msaidizi wa duka la mfanyabiashara Mohammed Saad linalodaiwa kuvamiwa na Sabaya na wasaidizi wake.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya na wasaidizi wake wawili, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura wanashtakiwa kwa makosa matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akiongozwa wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka jana Jumatatu jioni shahidi huyo alidai kuwa, Sabaya na wenzake baada ya kuvamia dukani waliwaweka chini ya ulinzi na kuwapiga huku wakiwarekodi kwa simu kuzungumza mambo waliyotaka.

Jasin amesema walilazimishwa kukiri kuwa waliiba dola 70,000 mjini Moshi na kuwa wanafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kinyume cha sheria la sivyo wangefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Shahidi huyo amesema wakiwa dukani walipigwa na kusachiwa na mabaunsa waliokuwa wakiongozwa na Sabaya.

Amesema waliokuwa chini ya ulinzi ndani ya duka hilo ni pamoja na Ally Saad, Fundi Salim, Annas, Tajirin na msichana mmoja aliyefika dukani kama mteja.

Amesema aliyemtambua Sabaya ni Diwani wa Kata ya Sombetini (CCM), Bakari Msangi ambaye alifika dukani na kumuita kwa jina Sabaya.

Jasin ambaye alieleza alikuwa hamjui Sabaya, amesema baada ya Msangi kumuita kwa jina Sabaya alimuuliza kama hajuwi jina lake ndipo alimuita General Lengai ole Sabaya.

Amesema Sabaya alimuhoji Msangi amefuata nini dukani ndipo, alijibu ameitwa na rafiki yake Saad baada ya kumwambia kuna tatizo dukani.

Amesema Sabaya alimweleza Msangi kuwa sisi tunafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kinyume cha sheria.

Awali Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula alieleza Mahakama kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Chanzo: Mwananchi
wnamtaabisha jamaa wa watu bureee lkn Mungu yupo atamsimamia
 
Unawajua vizuri CCM, hawana aibu, hawana woga, hawajali kitu chochote zaidi ya chama, waongo, chama kwanza na wanafanya vile itakavyo wapendeza wao na hakuna wa kuwafanya kitu.
Yani mtu wa ccm anaweza kuunga mkono kitu chochote kile hata kwenye ndoto ili mradi ni ccm. Hata kondoo wana afadhali ukiwaambia leo chama kimeamua jambo fulani wala hafikiri mara mbili ni jema ama la ananyoosha njia kesho ukisema chama kimefuta maamuzi ya jana anakwambia kidumu chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom