Shahidi kesi ya mauaji bilionea Msuya, Asema waliwakamata washtakiwa kwa mganga

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,778
Kwa ufupi
Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, shahidi huyo aliyekuwa kwenye timu ya operesheni, alisema katika mahojiano ya awali washtakiwa walikiri kumuua Msuya.

Shahidi wa 10 Sajini Atway wa upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya, jana aliieleza Mahakama namna walivyowakamata washtakiwa wawili kwa mganga wa jadi.

Akitoa ushahidi wake kwa kuongozwa na wakili wa Serikali Kassim Nassir, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni mshtakiwa wa tano, Karim Kihundwa na wa sita, Sadick Mohamed.

Mahojiano kati ya wakili Nassir anayesaidiana na mawakili waandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula, Omary Kibwana, Lucy Kyusa na shahidi huyo wa Jamhuri yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili Nassir: Shahidi ieleze Mahakama ulifikaje kwa mganga?

Shahidi:Tulichuka pikipiki mbili wakati huo mimi nilijifanya mgonjwa kwa maana ya kutaka kutibiwa, ndipo nikaenda kwa mganga huyo.

Wakili Nassir: Uliwatambuaje watuhumiwa hao?

Shahidi: Niliwatambua kwa kutumia picha. Hata mgambo na askari tuliokuwa nao niliwaonyesha picha.

Wakili Nassir: Shahidi ieleze Mahakama, lengo la kujifanya mgonjwa ni nini?

Shahidi: Ili niweze kuwatambua kwa urahisi nitakapoingia kwa mganga.

Wakili Nassir: Nini kilifuata baada ya kufika kwa mganga?

Shahidi: Tulipofika niliingia ndani na askari mwenzangu, mgambo walizunguka ile nyumba na mimi nikaingia kwa mganga peke yangu.

Wakili Nassir: Ieleze Mahakama, baada ya kuingia nini kilichofuata?

Shahidi: Nilipoingia nilimkuta mganga Khalidi Adam Sakamula.

Wakili Nassir: Baada ya hapo ikawaje?

Shahidi: Aliniangalia kwa kutumia vifaa vyake na kuniuliza kama ninaweza kuendelea na matibabu au niende nirudi kesho yake

Wakili Nassir: Ulijibu nini?

Shahidi: Nilimwambia nitarudi baadaye, ngoja nifuatilie vitu ulivyoniagiza

Wakili Nassir: Je uliondoka?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nassir: Baada ya kuondoka nini kilichotokea?

Shahidi: Nilipotoka nje nilikutana na mgambo pamoja na askari na wakanieleza kuwa wameona watu wawili umbali wa mita 20 kutoka nyumba ya mganga.

Wakili Nassir: Je, walijuaje kama ndiyo watuhumiwa?

Shahidi: Kwa sababu walikuwa na picha ya watuhumiwa hao ambayo na mimi nilikuwa nayo.

Wakili Nassir: Ukafanyaje?

Shahidi: Niliwaambia tuondoke ili tumfuate Afande Samuel (shahidi wa tisa) ndipo turudi pamoja na gari.

Wakili Nassir: Nini kilichoendelea?

Shahidi: Tuliondoka kumfuata Afande Samuel, tukampa taarifa juu ya kuwaona watuhumiwa hao.

Wakili Nassir: Nini kiliendelea?

Shahidi: Tulirudi pale kwa mganga tukiwa na gari ya polisi.

Wakili Nassir: Mlipofika nini kiliendelea?

Shahidi: Tulipofika kwa mganga, Afande Samuel alimwambia mganga anawatibu watu wawili wanaohusika na mauaji ya Erasto Msuya na kumtaka atuonyeshe waliko.

Wakili Nassir: Mganga alifanyaje?

Shahidi: Mganga alionyesha ushirikiano wa haraka na kutupeleka kwenye nyumba waliokuwamo watuhumiwa hao.

Wakili Nassir: Mlipofika ilikuaje?

Shahidi: Tulipokaribia kufika watuhumiwa walituona na kuanza kukimbia

Wakili Nassir: Mlifanyaje?

Shahidi: Nassir: Nilibaki kwenye gari, Afande Samuel alichukua pikipiki na kuanza kuwafukuza. Wakili Nassir: Nini kilichoendelea?

Shahidi: Baada ya muda kidogo Afande Samuel alimleta mtuhumiwa Sadick.

Wakili Nassir: Nini kiliendelea?

Shahidi: Nilibaki na Sadick kwenye gari, Afande Samuel alirudi kule alipotokea.

Wakili Nassir: Baada ya hapo ilikuaje?

Shahidi: Afande Samuel alirudi akiwa na mtuhumiwa Karimu.

Wakili Nassir: Huyo Karimu alikuaje?

Shahidi: Karimu alikuwa kaungua miguuni.

Wakili Nassir: Katika mahojiano ya awali mliyomhoji Sadick, alijibu ni nini?

Shahidi: Alijibu kuwa amehusika na mauaji.

Wakili Nassir: Alikuambia ni mauaji gani na kwanini?

Shahidi: Walihusika na mauaji ya Erasto Msuya na kila mmoja alikuwa na madhumuni yake.

Wakili Nassir: Nini kilitokea baada ya kuwaeleza?

Shahidi: Alimweleza Afande Samuel mahali ambako silaha ilifichwa.

Wakili Nassir: Nini kilifanyika tena?

Shahidi: Mtuhumiwa Sadick alimweleza Afande Samuel silaha iliyotumika.

Wakili Nassir: Nini kilichoendelea?

Shahidi: Afande Samuel alimpigia simu RCO Kilimanjaro na kumweleza kuwa wamewakamata watuhumiwa na wamesema sehemu walikoficha silaha.

Wakili Nassir: Ieleze Mahakama hii nini kilichoendelea baada ya Afande Samwel kupiga simu?

Shahidi:Tuliwachukua watuhumiwa wote wawili na kurudi nao kituo cha polisi Kariua.

Wakili Nassir: Ieleze Mahakama hii, 15/09/2013 ilikuaje?

Shahidi: Tarehe 15/09/2013 majira ya saa tisa jioni tuliondoka na kurudi Kilimanjaro.

Wakili Nassir: Umesema ulimkamata mtuhumiwa Sadik ukimwona unaweza kumkumbuka?

Shahidi:Ndiyo

Wakili Nassir: Ana mwonekano gani hasa?

Shahidi: Ni mwembamba, mrefu mweusi wa wastani.

Wakili Nassir: Hebu ionyeshe Mahakama hii na umwonyeshe Jaji kwa kumwonyeshea kidole ili amwone. (Shahidi anatoka kizimbani kuelekea kwenye kizimba cha washtakiwa).

Shahidi: Mheshimiwa jaji ni huyu hapa (akimnyooshea kidole mtuhumiwa wa sita) ni huyu.

Wakili Nassir: Umewezaje kumkumbuka tangu 2013 hadi leo?

Shahidi: Ana mwonekano uleule (huku akirudi kwenye kizimba)

Wakili Nassir: Ieleze Mahakama hii ukimwona Karimu unaweza kumkumbuka?

Shahidi:Ndiyo

Wakili Nassir: Tuelezee ana mwonekano gani?

Shahidi:Ni mweupe, mrefu kidogo ana mwili

Wakili Nassir: Ionyeshe Mahakama, Karimu ni yupi? (Shahidi akitoka kizimbani kwake na kuelekea kwenye kizimba cha washtakiwa).

Shahidi: Ni huyu hapa wa tano.

Jaji Maghimbi: Hebu asimame,

Karimu akakasimama

Jaji Maghimbi: Na huyo Sadick naye asimame, ni yupi Karimu?

Shahidi: Ni huyu hapa mheshimiwa jaji(huku akimwonyeshea kidole Karimu)

Wakili Nassir: Shahidi umewezaje kuwakumbuka wote hao?

Shahidi: Kwa sababu hawajabadilika.

Wakili Nassir: Baada ya hapo ilikuaje?

Shahidi: Tarehe 26/09/2013 Afande Samuel alituita tena kwa ajili ya safari nyingine.

Wakili Nassir: Aliwaeleza nini?

Shahidi: Alituambia tunamfuata mtuhumiwa mwingine Ally Mussa (Mjeshi) na yupo Mwanza

Wakili Nassir: Mwanza sehemu gani?

Shahidi: Alisema yupo Mwanza Wilaya ya Kwimba mji mdogo wa Ngudu.

Wakili Nassir: Baada ya hapo mlikwenda wapi?

Shahidi: Tulijiandaa kwa safari. Tarehe 27/09/2013 tulikwenda Mwanza, tulifika kituo cha polisi Kwimba na baadaye kwenda kituo kidogo cha polisi Ngudu. Inspekta Samuel aliongea na uongozi wa pale.

Wakili Nassir: Ikawaje?

Shahidi: Nilikabidhiwa askari wawili wenyeji wa pale.

Wakili Nassir: Kwa ajili ya nini?

Shahidi: Kumfuatilia Mjeshi

Wakili Nassir: Je? Mlifanikiwa?

Shahidi: Hatukufanikiwa, tulirudi kupumzika tukisubiri maelekezo mengine.

Wakili Nassir: Maelekezo kutoka wapi?

Shahidi: Kwa Inspekta Samuel.

Wakili Nassir: Nini kilifuata siku iliyofuata?

Shahidi: Tulikwenda tena ila hatukufanikiwa.

Wakili Nassir: Baada ya hapo?

Shahidi: Tulirudi kituoni, ndipo Inspekta Samuel alipopata taarifa kuwa mtuhumiwa anaelekea kivuko cha Geita

Wakili Nassir: Mlifanya nini?

Shahidi: Tulielekea kivuko cha Geita.

Wakili Nassir: Mlifanyaje?

Shahidi: Tulivuka tukaelekea Nyaganazi

Wakili Nassir: Mlivyoelekea huko mkafanyaje?

Shahidi: Baada ya Afande Samuel kutupa taarifa kuwa anaelekea huko tulimfuata hadi Kibondo.

Wakili Nassir: Afande Samuel alikwenda kufanya nini Kituo cha Polisi Kibondo?

Shahidi: Kutoa taarifa kuwa sehemu zote za vivuko ziwekewe vizuizi (barrier)

Wakili Nassir: Baada ya kuomba hivyo mlifanyaje?

Shahidi: Kutokana na kwamba ilikuwa usiku majira ya saa nane, hatukutambua aliko mtuhumiwa.

Wakili Nassir: Ikawaje?

Shahidi: Tulikwenda kupumzika, usiku huohuo Afande Samuel alipigiwa simu kuwa mtuhumiwa huyo haendelei tena na safari.

Wakili Nassir: Mlipumzika mpaka saa ngapi?

Shahidi: Hadi saa 11 alfajiri, baada ya muda kidogo Afande Samuel alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mtuhumiwa ameonekana Kigoma Mjini

Wakili Nassir: Baada ya kupewa taarifa yupo Kigoma Mjini mlifanyaje?

Shahidi: Tulianza safari ya kuelekea Kigoma Mjini

Wakili Nassir: Mlipofika mlifanyaje?

Shahidi: Tuliripoti kituo cha polisi Kigoma Mjini.

Wakili Nassir: Mlifanikiwa kumpata mtuhumiwa?

Shahidi: Hapana

Wakili Nassir: Ikawaje?

Shahidi: Tarehe 05/10/2013 saa 11 alfajiri tulielekea stendi kuu ya mabasi Kigoma

Wakili Nassir: Nini kiliendelea

Shahidi: Tukiwa stendi kuu, saa 12:15 asubuhi Afande Samuel alimuona mtu kama Ally Mjeshi na mwenzake wakiwa wanaongea na simu.

Wakili Nassir: Afande Samuel alifanyaje?

Shahidi: Alichukua simu akampigia mtuhumiwa kujua kama ni yeye.

Wakili Nassir: Nini kiliendelea

Shahidi: Mtuhumiwa alipokea simu halafu akakata.

Wakili Nassir: Nini kilifuata?

Shahidi: Tulijipanga mimi na Afande Samuel kwenda kuwakamata.

Wakili Nassir: Ikawaje sasa?

Shahidi:Tulifika pale walipokuwa wamesimama na kuwakamata.

Wakili Nassir: Mlivyowakamata mkawaambiaje?

Shahidi: Afande Samuel alijitambulisha na kumhoji palepale kuhusiana na kuhusishwa na mauaji ya Erasto Msuya.

Wakili Nassir: Ally Mjeshi akasemaje?

Shahidi: Alijibu ni kweli alihusika.

Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema, Janeth Joseph na Charles Lyimo.
 
sasa watuhumiwa wamekubari tokea mwaka 2013... mbona imechukua muda sana...

inakaribia miaka 5 wapo mahabusu.... hapo bado hukumu yenyewe.
 
Kiukweli, Shahidi amejitahidi kueleza kwa ufasaha ushahidi wake. Pamoja na Wakili kuuliza mambo mengi, maswali yake hayakujitosheleza. Alipaswa kupata na nia/motive ya mauaji hayo. Kiujumla, wamefanya vyema. Jeshi la Polisi linapaswa kuwatrain Askari wachache kwa ajili ya ushahidi. Hii itasaidia.
 
Mkuu ushahidi anatoa askari yule aliyehusika kufuatilia sio yoyote
 
Hii ndio habari imekamilika ina kila muongozo bravo wadau wetu kwa habari hii
 
Mi sijaelewa huyo askari alikua anapewa taarifa na nan alipo mtuhumiwa.. Na safari zake za kila mahali.... Huyo mtoa taarifa ni nan ama ni yeye alikua anajiigiza kama wanajuana..??

Na mbona walikua wanakubari kiurahisi sanaa... Na inaonesha hawajutii ata kuuwa..

Bado sijajua lengo la wauwaji..

Wale wauwaji walio kuwepo kwa mganga waliungua na nn??

Na kama walikua wanatibiwa walikua wanaumwa nn wote kwa pamoja??

Mi naomba nieleweshe uenda habari siijui vizuri..
 
Kuwpo kw mganga ni kutaka kunusuru kw njia ya kishirikina,, wali lako jingine kuhusu cominication Hio ni mambo ya intelejensia ,, la kuungua mguu yawezekana nikatka hali ya kubanwa ili waseme ukweli, na maanisha adhabu za kiupelelezi ili kuweza kukamilisha ushadi,
 
Very interesting..na yule dada aliyechinjwa kigamboni si anahusika na huyu msuya!
 
Back
Top Bottom