Shahidi awatambua Sabaya na wenzake ndio waliwavamia dukani

Shahidi wa pili katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, Numan Jasin (17) amewatambua kwa kuwashika mabegani Sabaya na wenzake.

Shahidi huyo ametoa ushahidi huo leo Alhamisi Julai 22, 2021 Mbele ya Hakimu Mkazi, Odira Amworo amesema Sabaya ndiye alikuwa anatoa amri zote, huku mshitakiwa wa pili alimpa simu kutaka apige nyumbani kufungua milango na wa tatu walikaa naye kwenye gari.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka shahidi huyo amesema awali wakiwa dukani hakuweza kuwatambua kwani kulikuwa na vurugu dukani.

Shahidi huyo amesema watuhumiwa hao waliwaweka chini ya ulinzi kwa takriban saa tatu kuanzia saa 11 jioni, walipigwa, kusachiwa na kuhojiwa na watuhumiwa hao.

Amesema katika duka hilo walikuwa chini ya ulinzi watu nane, ambao ni yeye, mjomba wake Hajirin Saad, Ally ,Mzee Salimu, Annas, Abuu Mansoor, Bakari Msangi na msichana mmoja.

Jasin amesema baada ya kuwa chini na ulinzi baadaye, waliachiwa wenzao na alibaki yeye na mjomba wake ambao walitakiwa kupanda katika gari lililokuwa nje ya duka.

Hata hivyo amesema mjomba wake ambaye alikuwa amefunga aliomba kununuliwa ndizi ili afungue ndipo Sabaya aliwanunulia ndizi moja moja.

Amesema baada ya kuondoka dukani magari yaliwapeleka nyumbani ambapo wakakuta milango imefungwa ndipo alipewa simu kumpigia mama yake na aliongea na kiarabu kumtaka asifungue.

Amesema baadaye walipelekwa kituo cha polisi Arusha na waliandika maelekezo na kupewa dhamana hadi Februari 10 saa 10 jioni.

Amesema kwa kuwa walimaliza mahojiano usiku polisi aliyekuwa anawahoji aliwapa msaada wa gari lake kuwarudisha nyumbani.
Shahidi huyo wa pili anaendelea kutoa ushahidi wake.

Miongoni mwa Maswali mimi sio mwanasheria Ok kama aliweza kuongea na mama yake kiarabu asifungue mlango kwanini hakumwambia aite polisi?

Anyway ngoja tuone wanavyoendelea kumsafisha Sabaya na tuhuma WALIOKUWA wanampaka miaka yote.

KWA KUWA ALIKUWA MTENDAJI
Mjomba wake aliekuwa amefunga aliomba apewe kitu afungue kwanza ndipo sabaya akawa nunulia ndizi moja moja wakafungulia.
Huyu jamaa alikuwa na roho mbaya sana
 
..tatizo ni mashahidi kudai walipelekwa POLISI.

..Je, Polisi wana rekodi ya Sabaya kuwapeleka watu hao kituoni?

..zaidi, ilikuwaje Sabaya akatoka kituo chake cha kazi wilaya ya HAI, na kwenda Arusha mjini na kufanya hayo anayotuhumiwa nayo?

..tatizo siyo tecno au laki 3, tatizo ni matumizi ya SILAHA ktk tukio analotuhumiwa Sabaya.

..ukiiba simu ya tecno na laki 3 bila kutumia silaha unahesabika kuwa ni mwizi / kibaki / mdokozi.

..ukiiba simu ya tecno na laki 3 kwa kutumia au kutishia kwa SILAHA utashtakiwa kwa UNYAN'GANYI / UJAMBAZI.

..Sabaya itabidi approve mahakamani kwamba alikuwa mahali pengine siku na saa ambayo tukio lilitokea. Kinyume na hayo nadhani kesi hii ni mbaya kwake.
Vipi kama alikuwa kikazi ? Ni wazi hao watu walikuwa wana makosa, Sabaya will be free soon…
 
Huyu Dogo kwa hizi purukushani anazopitia, naamini hata kama ikatokea akachomoka! Basi ujanja wake wote utakuwa umekwisha.

Itamlazimu kujipanga upya na kusafisha jina lake. Alifanya mambo mengi sana ya kitoto.
huyo hasafishiki kama alivyo bashite
 
Amesema baadaye walipelekwa kituo cha polisi Arusha na waliandika maelekezo na kupewa dhamana hadi Februari 10 saa 10 jioni.

Miongoni mwa Maswali mimi sio mwanasheria Ok kama aliweza kuongea na mama yake kiarabu asifungue mlango kwanini hakumwambia aite polisi?

Anyway ngoja tuone wanavyoendelea kumsafisha Sabaya na tuhuma WALIOKUWA wanampaka miaka yote.

KWA KUWA ALIKUWA MTENDAJI

Aite polisi vipi wakati umeshaambiwa walipelekwa polisi?hao polisi wangesaidia nini wakati aliyewakamata ndo boss wao au ulitaka hao polisi wakalinde nyumba yao?
 
Sabaya alimuiga bashite jinsi ya kupora pesa za watu, Utawala wa sheria ungekuwepo bashite angekuwa ndani
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kwa sisi wenye kufanya kazi ya kutoa haki, ukiona Shahidi amekutambua kwamba wewe ndio uliyefanya tukio unalotuhumiwa, aisee anza kukaa mguu sawa.

Siongezi maneno wengine endeleeni kuongea mnayotaka kuongea.
Key ya kesi za robbery huwa ni identification parade, witness akifanikiwa kumtambua mtuhumiwa ujue kesi inambana kwani huwa wanapanga line ya watu wanaoshabihiana na witness inamlazimu awatambue suspects.
 
kama aliwapa ndizi ili wafuturu basi inaonekana alikuwa mtu mwema kabisa hadi akakumbuka na kujali imani zao, ingekuwa jambazi kweli wala asinge hangaika na mambo hayo.
Inaonekana hauwajui majambazi, mbali na aina yao ya utafutaji pesa(ujambazi) nao ni binadamu wa kawaida na wanaishi maisha ya kawaida. A good number of them are very respectable in the society, ukionyeshwa na ukaambiwa ni jambazi hauwezi kuamini.
 
..tatizo ni mashahidi kudai walipelekwa POLISI.

..Je, Polisi wana rekodi ya Sabaya kuwapeleka watu hao kituoni?

..zaidi, ilikuwaje Sabaya akatoka kituo chake cha kazi wilaya ya HAI, na kwenda Arusha mjini na kufanya hayo anayotuhumiwa nayo?

..tatizo siyo tecno au laki 3, tatizo ni matumizi ya SILAHA ktk tukio analotuhumiwa Sabaya.

..ukiiba simu ya tecno na laki 3 bila kutumia silaha unahesabika kuwa ni mwizi / kibaki / mdokozi.

..ukiiba simu ya tecno na laki 3 kwa kutumia au kutishia kwa SILAHA utashtakiwa kwa UNYAN'GANYI / UJAMBAZI.

..Sabaya itabidi approve mahakamani kwamba alikuwa mahali pengine siku na saa ambayo tukio lilitokea. Kinyume na hayo nadhani kesi hii ni mbaya kwake.
Exactly.
 
Back
Top Bottom