Shahidi awatambua Sabaya na wenzake ndio waliwavamia dukani

..does he have an alibi?

..utetezi wa Sabaya utakuwa ni nini?

..Je, utetezi utakuwa kwamba hakutumia silaha?

..Au utetezi utakuwa kwamba hakuwepo kabisa eneo la tukio?

..Je, atakubali kusimama mahakamani na kujitetea, au ataamua kukaa kimya kwa kuogopa kujichanganya / kujichongea?
Key word, alibi.
 
Sabaya alimuiga bashite jinsi ya kupora pesa za watu, Utawala wa sheria ungekuwepo bashite angekuwa ndani
Bashite kesi za extortion anazo nyingi sana, inaonekana hakuna wa kumvalisha paka kengele.
 
Siku zote majungu na fitina kamwe hayawezi kushinda, kwa uwezo wa Mungu atamsaidia atashida mtihani huu alio upata.
Dunia ina watu wabaya sana kuliko hata wanyama!

yaani ni bora Mungu ametuwekea kifo, maaana ingekuwa hatufi nadhani tungetaabishana sana.

lkn leo utamtaabisha binaadamu mwezio lkn iko siku utafukiwa chini ya ardhi.

Binaadamu tusitendeane mabaya, tuishi kwa upendo.
Sabaya alifanya ukatili wa kutisha mno!!! Watu walitamani kufa mbele yake ila hawakufa,na waliokufa walikufa kwa mateso ya kusikitisha mno, Sabaya hana hukumu inayomstahili dun8a hii,labda tu Mungu amchulue akamhukumu mwenyewe!!!
 
Kwa akili yako, unaona kabisa Sabaya yupo na polisi, yeye ni MKuu wa wilaya, polisi wa wilaya wote wapo chini yake, na unategemea amwambie mama yake aite polisi?

wakati ujio wake tu ulikuwa wa kipolisipolisi-yeye ni mtu mwenye mamlaka, na unategemea amwambie mamake amwite mtu mwingine wa mamlaka aliyeop chini yake? na zaidi ya yote, kutokumwambia mamake aite polisi kuja kumwokoa mikononi mwa mkuu wa wilaya, unafikiri ina negate hoja kwamba aliwavamia na kuwafanyia kilichofanyika?

inapunguza uzito wa hoja kwamba yeye alikuwa anatisha sana kiasi kwamba mtu wa kawaida asingefikiria kutoa taarifa polisi?

Amekwisha huyu sabaya, na hata asipokwisha, ile kuvuliwa ukuu wa wilaya na Rais, kuwekwa lockup kwenye choo ya wazi anatita wakati wenzake wote wananusa nnya yake inatosha kuonyesha kiburi chake kimeshushwa hadi kuzimu kama kile cha mfalme Nebukadreza. bado bashite. shubatini kabisa.
Mkuu wa wilaya mporaji wewe unakuta mtendaji??
Hujui hata kazi za mkuu wa wilaya linabwabwaja tu kama mwehu
 
Shahidi wa pili katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, Numan Jasin (17) amewatambua kwa kuwashika mabegani Sabaya na wenzake.

Shahidi huyo ametoa ushahidi huo leo Alhamisi Julai 22, 2021 Mbele ya Hakimu Mkazi, Odira Amworo amesema Sabaya ndiye alikuwa anatoa amri zote, huku mshitakiwa wa pili alimpa simu kutaka apige nyumbani kufungua milango na wa tatu walikaa naye kwenye gari.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka shahidi huyo amesema awali wakiwa dukani hakuweza kuwatambua kwani kulikuwa na vurugu dukani.

Shahidi huyo amesema watuhumiwa hao waliwaweka chini ya ulinzi kwa takriban saa tatu kuanzia saa 11 jioni, walipigwa, kusachiwa na kuhojiwa na watuhumiwa hao.

Amesema katika duka hilo walikuwa chini ya ulinzi watu nane, ambao ni yeye, mjomba wake Hajirin Saad, Ally ,Mzee Salimu, Annas, Abuu Mansoor, Bakari Msangi na msichana mmoja.

Jasin amesema baada ya kuwa chini na ulinzi baadaye, waliachiwa wenzao na alibaki yeye na mjomba wake ambao walitakiwa kupanda katika gari lililokuwa nje ya duka.

Hata hivyo amesema mjomba wake ambaye alikuwa amefunga aliomba kununuliwa ndizi ili afungue ndipo Sabaya aliwanunulia ndizi moja moja.

Amesema baada ya kuondoka dukani magari yaliwapeleka nyumbani ambapo wakakuta milango imefungwa ndipo alipewa simu kumpigia mama yake na aliongea na kiarabu kumtaka asifungue.

Amesema baadaye walipelekwa kituo cha polisi Arusha na waliandika maelekezo na kupewa dhamana hadi Februari 10 saa 10 jioni.

Amesema kwa kuwa walimaliza mahojiano usiku polisi aliyekuwa anawahoji aliwapa msaada wa gari lake kuwarudisha nyumbani.
Shahidi huyo wa pili anaendelea kutoa ushahidi wake.

Miongoni mwa Maswali mimi sio mwanasheria Ok kama aliweza kuongea na mama yake kiarabu asifungue mlango kwanini hakumwambia aite polisi?

Anyway ngoja tuone wanavyoendelea kumsafisha Sabaya na tuhuma WALIOKUWA wanampaka miaka yote.

KWA KUWA ALIKUWA MTENDAJI
Yaani polisi aje amuamuru mkuu wa wilaya kuwaachia aliowashikilia..!?? AKILI HIZI..!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom