Shahidi aliyehongwa milioni 5 awakaanga ccm singida-chadema hawanunuliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shahidi aliyehongwa milioni 5 awakaanga ccm singida-chadema hawanunuliki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Apr 5, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  [h=3]Shahidi aliyeletwa NA CCM na inasadikiwa alihongwa milioni 5 kesi ya Lissu awakaanga CCM[/h][h=3]KESI YA LISSU: Shahidi awakaanga CCM. [/h][h=3]Shahidi aomba ulinzi baada ya kutoa ushahidi, jaji aamuru polisi wamsindikize, Abebwa na gari ya RCO[/h][h=3]Shahidi aondolewa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi; [/h][h=3] [/h][h=3]Mahakama kuu ya Singida, inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliomweka madarakani Mbunge wa jimbo la Singida mashariki, jana iligeuka kuwa eneo la kuchekesha baada ya Shahidi wa 22, Husein Msuna Mwangia kusema ukweli toka moyoni, uliopingana kabisa na ushahidi alioufundishwa na wakili wake.[/h][h=3] [/h][h=3]Awali akiongozwa na wakili wa waleta maombi, Bw. Wasonga, Shahidi alihojiwa Jina, na baadhi ya Nyaraka za Vyama vya CHADEMA, CUF, TLP, NCCR NA APPT Maendeleo, alijibu kwa ufasaha, lakini kadiri alivyoendelea kujibu, wakili wa walalamikaji alisema ameshindwa kumwelewa Shahidi kwa kuwa alikuwa anajibu kinyume na kadiri walivyoongea kabla ya kuingia mahakamani.[/h][h=3] [/h][h=3]WAKILI:Mheshimiwa jaji, kabla sijamtangaza shahidi huyu kuwa ‘hostile’ ninashindwa kumwelewa shahidi huyu, maana kabla hatujaingia mahakamani nilipanga maswali 40 ya kumuuliza na tulielewana[/h][h=3]SHAHIDI:Mheshimiwa Jaji naomba kuongea[/h][h=3]JAJI; Utaongea nini wakati yeye ndo anakuongoza, mimi nitaandika nini?[/h][h=3]Wakili: Mheshimiwa jaji, naomba nipate fursa nitoke nje nikaongee tena kidogo na shahidi wangu.[/h][h=3],.................. watu waliguna wakapiga kele...........................................[/h][h=3]Wakili: Mheshimiwa jaji, hii kesi siyo yangu,[/h][h=3] JAJI: Je niandike kuwa hii kesi sio yako[/h][h=3] [/h][h=3]Wakili: Basi naomba iwe ‘off record’ isirekodiwe[/h][h=3]JAJI: Shahidi hii hali imetokeaje mnashindwa kuelewana na Wakili wako? Yeye anasema mlipanga kuja kuongea hapa, wewe unasema hamjaonana. Imekuwaje?[/h][h=3]SHAHIDI: Mheshimiwa jaji, naapa, kabisa mimi huyu sijaonana naye ila hapa Mahakamani. Mimi nilidhani wote mimi nay eye wote tumeitwa na Lissu, namshangaa hapa ananiambia tulionana. Mimi nilidhani nimeitwa na Lissu hayo anayotaka niseme siyajui.[/h][h=3]JAJI: sitangazi huyu shahidi kuwa ‘hostile’ una haki ya kuendelea kumhoji au kuacha ili upande mwingine wawe kumhoji.[/h][h=3] [/h][h=3]Wakili: Katika hali ilivyo siwezi kuendelea, mheshimiwa jaji tuliahidi kufunga ushahidi ila kwa leo na kwa hali ilivyojitokeza naomba ruhusa kuongeza shahidi wengine wawili[/h][h=3]Jaji: Nimekubaliana na Ombi lako tutaahirisha mahakama hadi siku ya Jumanne ijayo.[/h][h=3] [/h]
   
 2. Makete Kwetu

  Makete Kwetu JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Richa ya shahidi kujikanganya live..usishange jaji kutoa maamuzi yake tofauti mwisho wa siku!!!!
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hivi nayo hii ni kesi ? maana tangu mwanzo ashahidi wote hawana cha maana cha kusema
   
 4. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Duh, sikia maajabu sasa utasikia Lissu naye ubunge wake umetenguliwa! Nitakunya hadharani hapa.
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa akili yako baada ya kula viroba na ndumu hatutashangaa ukijiharishia bana kunya anakunya bata kuku anajamba tu!
   
 6. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tutazidi kuwaumbua tu. kufa kwa nyani?
   
 7. Non stop

  Non stop Senior Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sijajua kwa haya mashinikizo ya ccm yatatufikisha wapi,.kwa hali hii majimbo yote ambayo chadema ilishinda utasikia yanawekewa pingamizi. Hivi jamani ccm fikeni muda mkubali kushindwa bwana, wabunge wenu mbona wanatukana hadharani tu kisha mnawatetea eti iliku ni jaziba,.acheni bwana wabunge wetu watutumikie na siyo kuwapotezea muda mwingi na kesi zisizokua na kichwa wala miguu mahakamani.,nawasilisha wakuu..
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kunamambo yanatokea Tanzania tu
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kwa mahakama zetu kuna maajabu mengi tutasikia
   
 10. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ccm ******* nasema tena! Mtaniwiaradhi, wanauzi bana!
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi kwanini majimbo mengi ambayo CHADEMA ilishinda kuna kesi za kupinga matokeo? Hii ina maanisha nini? Kama hii ya mheshimiwa Lisu sasa ina maanisha nini? Maana ni aibu tupu. CCM hawajawahi kufikiria namna nyingine ya kufanya mambo yao isipokuwa kutumia vyombo vya kutetea haki ili kuwaumiza wasio na hatia? Mara watumie polisi kuua wasio na hatia, mara watumie mahakama kunyonga haki za watu, hii ni nini sasa?
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Kweli inasisimua na kufurahisha lakni kwa huzuni! ccm ni sikio lakufa....halisikii dawa na ni lazima life.

  Hata kesi ya Lema mashahidi walikuwa weupe na wenye kujichanganya lakini ona jaji kaamua kwa maslah fulani. So we're heading for SOMETHING here
   
 13. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kutujuza.penye ukweli daima mungu husimama.mahakama zetu zina hatarisha haki za watu maskini
   
 14. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania yetu inaharibiwa na wachache! 0 .00000000000 00000000.1%
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kesi nyingine upuuzi mtupu!
   
 16. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania yetu inaharibiwa na wachache! 0 .00000000000 00000000.1%
   
 17. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Jamani mimi hua nawaambia watu, ila hawataki kunielewa, Mahakamani hakuna HAKI mahakamani wanahukumu kwa kutumia uongo na umbea wa watu wachache,(sheria na haki ni vitu viwili tofauti.Sheria haiijui Haki hata kidogo,
   
 18. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  CCM watalipa kila nukta ya uhalifu wanaoufanya kwa gharama kubwa. Wapinzani watarajie mateso na manyanyaso mengi kabla ya zimwi hili kung'oka na kuangamizwa kabisa kama lenziwe la jirani KANU. Haiingii kabisa akilini kwa mtu mwenye wadhifa kama wa mbunge akadhalilishwa na wahuni kukatwa mapanga na kujeruhiwa mbele ya polisi wenye silaha; kesho yake IGP badala ya kutuarifu hatua alizochukua anabwabwaja ati jukumu la ulinzi ni la kila mwananchi! CCM wanatumia asasi zinazogharimiwa na umma kwa faida yao, Polisi, Usalama wa Taifa, Mahakama hadi Tume ya uchaguzi vyote vinawalinda. Hakuna refu lisilo ncha, kwa hiyo kila kukicha taifa linasogelea saa ya ukombozi na uhuru toka kwenye makucha ya utawala katili huu.
  Mungu ibariki Tanzania.

   
 19. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata mashaidi wa ccm wamtetee lisu, magamba wamesha amua kutengua ushindi wa wabunge wote wa CDM. tutakutana kwenye boksi la kura.
   
 20. I

  Itibari Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hiyo ndio Tanzania na wanasheria vihiyo wasiokuwa na uchungu na nchi kama walivyo wadau wa ccm. zama zaja zmbapo tutaanza kuwahukumu waao kabla ya bwana zao. naapa mbele ya mumba nitakuwa shahidi wa hilo.
   
Loading...