Shahidi akwamisha kesi Na. 458 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums kuendelea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Kesi ya Jinai namba 458 ya mwaka 2016 ya Jamhuri dhidi ya Maxence Melo na mwenzake Micke William kuhusu kuendesha mtandao nchini bila kutumia Kikoa cha do.TZ na Kuzuia Upelelezi wa Polisi imeshindwa kuendelea na ushahidi leo October 01, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu baada ya shahidi wa upande wa Jamhuri kutofika Mahakamani

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Wakili wa Serikali, Wankyo Saimon mbele ya Hakimu Huruma Shahidi

Wakili wa Jamhuri ameiambia Mahakama kuwa shauri hilo lilikuwa mbele ya Mahakama kwa ajili ya kusikilizwa lakini kutokana na kukosekana kwa shahidi ambaye alikuwa safarini na amerudi ila kwa sasa ni mgonjwa hivyo ameshindwa kufika Mahakamani hapo. Wakili huyu aliomba kupangiwa tarehe nyingine kwani shahidi huyu ni wa mwisho, hivyo ameihakikishia Mahakama watakuja na shahidi huyu kama atakuwa amepona

Wakili wa upanda wa mshtakiwa, ameiambia Mahakama kuwa ni mara zaidi ya 6 sasa Shahidi wa upande wa Mashtaka anakosekana Mahakamani hapo. Wakili ameiomba Mahakama kuchukua hatua kuhusu suala hilo

Hakimu Huruma Shahidi ameutaka upande wa Mashtaka kuhakikisha kuwa kwa tarehe iliyopangwa, wahalikishe Shahidi anakuwepo kwani hii ni mara ya mwisho kesi hiyo itahairishwa kutokana na kukosekana kwa shahidi

Shauri hili, litasikilizwa tena Octoba 18, 2019

Katika shauri hilo lililofunguliwa Desemba 2016 na kuanza kusikilizwa Februari 2017, tayari mashahidi zaidi ya Watatu kutoka upande wa Jamhuri wameshasikilizwa na shahidi wa mwisho kusikilizwa ilikuwa mnamo Novemba 07, 2018. Baada ya hapo shauri limekuwa likiahirishwa huku sababu kadhaa zikitolewa na kubwa ikiwa ni kukosekana kwa shahidi.
 
Back
Top Bottom